#COVID19 Hoja ya Polepole na hoja ya Gwajima juu ya chanjo ya Covid-19

Ngoja tuanze na hii chanjo ya J&J. Hii chanjo inatumia teknolojia ya zamani. Teknolojia ambayo usalama wake na makandokando yake unajulikana vema. Hivyo chanjo kama hii haihitaji utafiti au majaribio ya muda mrefu kujua madhara na ufanisi wake.

Chanjo hii ni aina ya Viral vector. Hapa kirusi aliyepunguzwa nguvu au aliyeuwawa huchomwa ndani ya mtu. Mwili unagundua uvamizi na kutengeneza kinga. Siku nyingine kirusi chenyewe kikija, kinga inakuwepo tayari. Teknolojia hii inajulikana vema. Wanasema, "hakuna haja ya kugundua gurudumu kwa mara ya pili." Teknolojia imekuwa, vitu vingi vinajulikana. Mambo yanaweza kwenda fasta. Hivyo siyo majaribio, watu wanauhakika wa asilimia nyingi ya kile kinachofanyika.
Yani kwamba haihitaji majaribio ya muda mrefu kuweza kujua hiyo chanjo inareact vp kwa makundi tofauti ya watu?
 
Sasa mbona chanjo pia hazizuii kupata maambukizi na kuambukiza? sasa hapo tutazuia vp hiyo hali ya virusi kubadilika badilika? na kuhusu afrika je kwanini mpaka sasa haijawa kuwa ndio uwanja wa virusi Kumutate kwa sababu tuko nyuma kwenye kuzuia maambukizi na hata kasi ya kuchanja chanjo?
Swali lako la kwanza, chanjo inazuia virusi kuingia kwa mtu kumuambukiza, lakini si kwa asilimia mia, imaweza kuwa 80 nk, na pia ni kwa aina ya kirusi kinachodhibitiwa na chanjo hiyo tu, kama kimebadilika sana, haitafanya kazi. Ndiyo maana aliyechanjwa anaweza kuambukizwa na kuambukiza wengine.

Na njia pekee ya kuzuia kirusi kubadilikabadilika ni kupunguza mazalia yake/watu walioambukizwa. Na hapo inahitajika chanjo na kujikinga

Afrika hatuwezi sema siyo uwanja wa virusi kumutate, maana hata kupima hatupimi. Na Mtu kama Magu ni kama alikataza kupima. Ila watu wanakufa sana huku mitaani.
 
Ambaye hana dalili halazimiki.
Sasa mbona mnajichanganya nyie wenye elimu ya hizi chanjo? wengine wanasema unatakiwa kupima kwanza corona kabla ya kuchanjwa na wengine wanasema kama huna dalili za corona hakuna ulazima wa kupima corona.
 
Yani kwamba haihitaji majaribio ya muda mrefu kuweza kujua hiyo chanjo inareact vp kwa makundi tofauti ya watu?
Sehemu kubwa ya maarifa hayo yapo tayari. Kinachobadilika ni kile kirusi tu. Ingridients zingine zinajulikana na madhara yake kwa watu mbalimbali yanajulikana.
 
Kwa hiyo nikichanja siwezi kuambukizwa corona?,je siwezi kuambukiza wengine?,Je nikichanjwa sitalazimika kuvaa barakoa?,Je, nikichanjwa sitalazimika kujizuia na mikusanyiko?,Je, nikichanjwa sitalazimika kuchanja tena chanjo ya COVID-19?.Ukinijibu hoja hizi vizuri, naenda kuchanja hata Sasa hivi.
Vaccine ya J& J inazalisha kinga ya zaidi ya 70%. Hivyo ukichanja utakuwa umejikinga kwa zaidi ya 70%. Kwanini unatakiwa uendelee kutumia njia zngine za kujikinga kama kuvaa barakoa maeneo yenye mkusanyiko:- ,, ni kwasababu ya hizo asilimia chache zilizobaki chini ya 30%.

Naifananisha hii na mtu ambaye anaifunga nyumba yake milango wakati wa kulala japo si kwamba unaweza zuia wezi kwa asilimia 100. Utajenga ukuta, utaweka nyaya za umeme ,cctv camera, utafuga mbwa wakali yote hayo ni ili kuendelea kujiweka salama zaidi.
Mwenye kinga asilimia 70 yupo salama ziadi ya ambaye hana.

Hata rate ya maambukizi pia hupungua. Ushahidi upo kwa nchi ambazo wamechanja kwa kiasi kikubwa. Maambukizi yameshuka sana kiasi baadhi ya nchi wamelegeza sana masharti ikiwemo uvaaji wa barakoa , au kulazimika kujirejister kabla haujaingia dukani. Na idadi ya vifo imeshuka sana.

Kama una maswali mengine ,nitajitahidi kukujibu kadri iwezekananvyo. Mi nasema elimu sahihi ifike ili mtu aamue kuchanja ama la akiwa anajua.
 
Sasa mbona mnajichanganya nyie wenye elimu ya hizi chanjo? wengine wanasema unatakiwa kupima kwanza corona kabla ya kuchanjwa na wengine wanasema kama huna dalili za corona hakuna ulazima wa kupima corona.
Chanjo inafanya kazi mtu akiwa hana maambukizi, chanjo ni kinga, siyo tiba. kama amepata tayari ugonjwa haisaidii.

Ndiyo lengo hasa la kusema wenye dalili za korona wasichanjwe. Na kama resources zipo unaweza kuwapima wote kujiridhisha kama wanq korona, lakini ka mtu haonyeshi dalili, halazimiki kupima.
 
Vaccine ya J& J inazalisha kinga ya zaidi ya 70%. Hivyo ukichanja utakuwa umejikinga kwa zaidi ya 70%. Kwanini unatakiwa uendelee kutumia njia zngine za kujikinga kama kuvaa barakoa maeneo yenye mkusanyiko:- ,, ni kwasababu ya hizo asilimia chache zilizobaki chini ya 30%.

Naifananisha hii na mtu ambaye anaifunga nyumba yake milango wakati wa kulala japo si kwamba unaweza zuia wezi kwa asilimia 100. Utajenga ukuta, utaweka nyaya za umeme ,cctv camera, utafuga mbwa wakali yote hayo ni ili kuendelea kujiweka salama zaidi.
Mwenye kinga asilimia 70 yupo salama ziadi ya ambaye hana.

Hata rate ya maambukizi pia hupungua. Ushahidi upo kwa nchi ambazo wamechanja kwa kiasi kikubwa. Maambukizi yameshuka sana kiasi baadhi ya nchi wamelegeza sana masharti ikiwemo uvaaji wa barakoa , au kulazimika kujirejister kabla haujaingia dukani. Na idadi ya vifo imeshuka sana.

Kama una maswali mengine ,nitajitahidi kukujibu kadri iwezekananvyo. Mi nasema elimu sahihi ifike ili mtu aamue kuchanja ama la akiwa anajua.
Kabisa, asifanye maamuzi akiwa gizani.
 
Swali lako la kwanza, chanjo inazuia virusi kuingia kwa mtu kumuambukiza, lakini si kwa asilimia mia, imaweza kuwa 80 nk, na pia ni kwa aina ya kirusi kinachodhibitiwa na chanjo hiyo tu, kama kimebadilika sana, haitafanya kazi. Ndiyo maana aliyechanjwa anaweza kuambukizwa na kuambukiza wengine.

Na njia pekee ya kuzuia kirusi kubadilikabadilika ni kupunguza mazalia yake/watu walioambukizwa. Na hapo inahitajika chanjo na kujikinga

Afrika hatuwezi sema siyo uwanja wa virusi kumutate, maana hata kupima hatupimi. Na Mtu kama Magu ni kama alikataza kupima. Ila watu wanakufa sana huku mitaani.
Nachosema ni kwamba chanjo haizuii mtu kupata virusi na kuambukiza wengine ila nachojua chanjo inamsaidia yeye kutoguua au hata akiugua basi hatofikia kuwa na hali mbaya ya kufikia kulazwa kwa sababu ya kinga aliyopata kutoka kwenye chanjo, lakini suala la kupata maambukizi(virusi) na kuambukiza lipo palepale tu, ndio maana nikauliza je hapo tutazuia vp hiyo hali ya virusi kubadilika?

Kuhusu Afrika kusema hatupimi sidhani kama ni sahihi maana sio kila nchi afrika inafanya kama Tanzania, sasa sijui ulitaka kupima kupi huko ambako ndio tungeweza kuona jinsi afrika ni uwanja wa virusi Kumutate?
 
Polepole: Moja, Polepole yeye anasema kuwa corona ni ugonjwa uliotengenezwa na big pharma ili yapige pesa. Kuwa mabeberu wanaachana na kuvamia nchi kuiba mafuta na sasa wanatengeneza magonjwa ili kupiga pesa.

Pili, Anasema kuwa kasi ya kirusi kubadilika(ku-mutate) inatia shaka, si ya kawaida.

Tatu, anauliza chanjo hiyo itamkinga kwa muda gani? Akatolea mfano kuwa chanjo zingine hudumu maisha yote ya mtu, je hii inadumu muda gani? Hapo anamaanisha kuwa atahitajika kuinunua mara ngapi?

Gwajima yeye anasema kuwa chanjo zile zina serial number, kuwa ukichanja zinakusajili. Kwamba ipo kama barcode, itafika wakikuwekea detector itasoma iwapo umechanja au haujachanja. Kuna mahali amewahi husisha chanjo hii na habari za 666 na ujio wa mfumo mpya, ndiyo maana anasema kuwa watu waananunua dhahabu kwa wingi ili kujiandaa na mfumo mpya, mfumo ambao pengine pesa za makaratasi zisiwe na thamani.

Pia anahoji kuwa kama ukichanja bado utatakiwa kuvaa barako, kutumia sanitizer, utaugua na utaambukiza wengine, ya nini kuchanja?

Amewahi kusema kuwa chanjo ya mRNA inabadilisha watu na kuwafanya mazombie, hivyo akashauri kuwa wanajeshi wasichanjwe.

Kifupi hizi ndizo hoja za hawa wabunge wawili walio mbele kupinga uchanjaji.

Mi kwa maoni yangu ni kuwa hawa jamaa hawana hoja za msingi bali ni Conspiracy theorist tu.
Uzuri ni kuwa chanjo ni hiyari, kwa kawaida binadamu hatuwezi wote tukawa sawa, wanaotaka kuchanjwa wasibezwe na wasiyotaka kuchanja wasidharauliwe. Wabongo sisi ni jamii ya walimwengu na ulimwengu unakwenda kasi katika nyanja za sayansi na teknolojia. Hivyo tuwekeze kwenye elimu za sayansi na teknojia siyo kuwekeza katika mambo ya siasa na kila kitu chetu huwa tunafanya siasa tu, tubadilikeni.
 
Chanjo inafanya kazi mtu akiwa hana maambukizi, chanjo ni kinga, siyo tiba. kama amepata tayari ugonjwa haisaidii.

Ndiyo lengo hasa la kusema wenye dalili za korona wasichanjwe. Na kama resources zipo unaweza kuwapima wote kujiridhisha kama wanq korona, lakini ka mtu haonyeshi dalili, halazimiki kupima.
Huyo ambaye ameshapata teyari ugonjwa ndio huyo ambaye anaonesha dalili au hata ambaye hajaonesha dalili?
 
Ngoja tuanze na hii chanjo ya J&J. Hii chanjo inatumia teknolojia ya zamani. Teknolojia ambayo usalama wake na makandokando yake unajulikana vema. Hivyo chanjo kama hii haihitaji utafiti au majaribio ya muda mrefu kujua madhara na ufanisi wake.

Chanjo hii ni aina ya Viral vector. Hapa kirusi aliyepunguzwa nguvu au aliyeuwawa huchomwa ndani ya mtu. Mwili unagundua uvamizi na kutengeneza kinga. Siku nyingine kirusi chenyewe kikija, kinga inakuwepo tayari. Teknolojia hii inajulikana vema. Wanasema, "hakuna haja ya kugundua gurudumu kwa mara ya pili." Teknolojia imekuwa, vitu vingi vinajulikana. Mambo yanaweza kwenda fasta. Hivyo siyo majaribio, watu wanauhakika wa asilimia nyingi ya kile kinachofanyika.
Kirusi aliyedhoofishwa wa Corona na wa Chanjo zingine za hiyo miaka mingi unayoitaja ni sawa?

Na je, madhara ya muda mfupi, ya muda wa kati na ya muda mrefu ni yapi?
 
Uzuri ni kuwa chanjo ni hiyari, kwa kawaida binadamu hatuwezi wote tukawa sawa, wanaotaka kuchanjwa wasibezwe na wasiyotaka kuchanja wasidharauliwe. Wabongo sisi ni jamii ya walimwengu na ulimwengu unakwenda kasi katika nyanja za sayansi na teknolojia. Hivyo tuwekeze kwenye elimu za sayansi na teknojia siyo kuwekeza katika mambo ya siasa na kila kitu chetu huwa tunafanya siasa tu, tubadilikeni.
Ubaya ni kwamba hata kwenye sayansi kuna siasa na kama si siasa pengine hizi chanjo zisingepata mashinikizo yaliyowezesha kupata ruhusa ya kutumika kwa watu wote kwa muda mchache tu hasa ukizingatia hali ya majaribio yake huko ilivyokuwa.
 
Vaccine ya J& J inazalisha kinga ya zaidi ya 70%. Hivyo ukichanja utakuwa umejikinga kwa zaidi ya 70%. Kwanini unatakiwa uendelee kutumia njia zngine za kujikinga kama kuvaa barakoa maeneo yenye mkusanyiko:- ,, ni kwasababu ya hizo asilimia chache zilizobaki chini ya 30%.

Naifananisha hii na mtu ambaye anaifunga nyumba yake milango wakati wa kulala japo si kwamba unaweza zuia wezi kwa asilimia 100. Utajenga ukuta, utaweka nyaya za umeme ,cctv camera, utafuga mbwa wakali yote hayo ni ili kuendelea kujiweka salama zaidi.
Mwenye kinga asilimia 70 yupo salama ziadi ya ambaye hana.

Hata rate ya maambukizi pia hupungua. Ushahidi upo kwa nchi ambazo wamechanja kwa kiasi kikubwa. Maambukizi yameshuka sana kiasi baadhi ya nchi wamelegeza sana masharti ikiwemo uvaaji wa barakoa , au kulazimika kujirejister kabla haujaingia dukani. Na idadi ya vifo imeshuka sana.

Kama una maswali mengine ,nitajitahidi kukujibu kadri iwezekananvyo. Mi nasema elimu sahihi ifike ili mtu aamue kuchanja ama la akiwa anajua.
Ni vp maambukizi yanapungua kwa hizo nchi kuwa hizo nchi zilizochanja watu wengi?
 
Sehemu kubwa ya maarifa hayo yapo tayari. Kinachobadilika ni kile kirusi tu. Ingridients zingine zinajulikana na madhara yake kwa watu mbalimbali yanajulikana.
Ki vp yani hebu fafanua?maana kama ni hivyo basi isingekuwa na haja ya kutumia gharama kubwa kufanya majaribio na kwamba zimeruhusiwa kutumika kutokana hali ya dharura.
 
Nachosema ni kwamba chanjo haizuii mtu kupata virusi na kuambukiza wengine ila nachojua chanjo inamsaidia yeye kutoguua au hata akiugua basi hatofikia kuwa na hali mbaya ya kufikia kulazwa kwa sababu ya kinga aliyopata kutoka kwenye chanjo, lakini suala la kupata maambukizi(virusi) na kuambukiza lipo palepale tu, ndio maana nikauliza je hapo tutazuia vp hiyo hali ya virusi kubadilika?

Kuhusu Afrika kusema hatupimi sidhani kama ni sahihi maana sio kila nchi afrika inafanya kama Tanzania, sasa sijui ulitaka kupima kupi huko ambako ndio tungeweza kuona jinsi afrika ni uwanja wa virusi Kumutate?
Kupima variants, tuna uwezo au tunafanya hivyo? Hiyo ndiyo inakuonyesha level ya mutation. Maana hata kupima tu nchi nyingi ni shida.

Pia elewa kuwa mtu mwenye chanjo si rahisi kumuambukiza mwingine sababu virusi havizaliani ndani yake. Na kwa sababu virusi havizaliani si rahisi kumutate. Na si rahisi kuambukizwa kwasababu kirusi kikiingia kinakutana na kinga ya mwili.

Kuzuia kirusi kumutate unatakiwa kuzuia kizizaliane. Hivyo basi, chanjo na kujikinga ndizo njia.
 
Uzuri ni kuwa chanjo ni hiyari, kwa kawaida binadamu hatuwezi wote tukawa sawa, wanaotaka kuchanjwa wasibezwe na wasiyotaka kuchanja wasidharauliwe. Wabongo sisi ni jamii ya walimwengu na ulimwengu unakwenda kasi katika nyanja za sayansi na teknolojia. Hivyo tuwekeze kwenye elimu za sayansi na teknojia siyo kuwekeza katika mambo ya siasa na kila kitu chetu huwa tunafanya siasa tu, tubadilikeni.
Hiyari ni lugha tu. Si umeona Wachezaji wa Simba wamelazimika kuchanja. Wewe ukitaka kusafiri nje utaulizwa kama umechanja, uhiari gani hapo?
 
Huyo ambaye ameshapata teyari ugonjwa ndio huyo ambaye anaonesha dalili au hata ambaye hajaonesha dalili?
Unaweza pata ugonjwa na ukaonyesha dalili au usionyeshe. Ila mara nyingi tunachukulia asiye na dalili hana ugonjwa. Ndiyo maana asiye na dalili si lazima kupima kwanza.
 
Ubaya ni kwamba hata kwenye sayansi kuna siasa na kama si siasa pengine hizi chanjo zisingepata mashinikizo yaliyowezesha kupata ruhusa ya kutumika kwa watu wote kwa muda mchache tu hasa ukizingatia hali ya majaribio yake huko ilivyokuwa.
Nadhani TZ kwa sasa tunatumia political science katika ku-handle hii hali ya Uviko-19.
Ni kweli hawa wenye nguvu wanatumia nguvu kubwa katika hili jambo la Uviko-19 na tumeachwa na less options katika kuamiliana na ulimwengu.
 
Kirusi aliyedhoofishwa wa Corona na wa Chanjo zingine za hiyo miaka mingi unayoitaja ni sawa?

Na je, madhara ya muda mfupi, ya muda wa kati na ya muda mrefu ni yapi?
Madhara ya kirusi cha korona yamejulikana anapoingia mwilini, huyu aliyedhoofishwa atakuwa na madhara chini ya yule mwenye nguvu zake. Sometimes virusi hawa waliodhoofishwa huwa wanaleta madhara kwa watu wenye kinga dhaifu. Ndiyo maana kuna baadhi ya chanjo kabla hujapata unashauriwa kumueleza daktari iwapo unatumia dawa za kansa, una ukimwi au unatumia vitu vyovyote vya kushusha kinga yako.

Ingridients zingine, zimekuwa Ikitumika miaka na miaka. Madhara yake yanajulikana vema. Nyakati zingine kufanya clinical trials ni formality tu, lakini kwa technolojia na maarifa yaliyopo, vingi vinajulikana.
 
Nadhani TZ kwa sasa tunatumia political science katika ku-handle hii hali ya Uviko-19.
Ni kweli hawa wenye nguvu wanatumia nguvu kubwa katika hili jambo la Uviko-19 na tumeachwa na less options katika kuamiliana na ulimwengu.
Mi nafikiri kipindi cha Magufuli ndiyo ilitumika siasa. Kwa sasa nchi imegeukia sayansi.
 
Back
Top Bottom