#COVID19 Hoja ya Polepole na hoja ya Gwajima juu ya chanjo ya Covid-19

Wataalamu wanasema kama kirusi kimekupata halafu ukaenda kuchanja haitakusaidia. Unashauriwa upime kwanza na ndipo uchanje, ili kwamba kama umeambukizwa itabidi utibiwe hadi upone halafu ndipo uchanjwe.

Na J&J inazalisha kinga kwa 70%. Inamaana uwezekano wa kukinga sio 100%. So possibility ya kuambukizwa na pengine kupoteza maisha bado ipo kwasababu vaccine siyo kinga ya kifo.

Nadhani nimekujibu kitu.
 
Umeona eenhh???!!!.Mimi sichanji km ni kufa nitakufa kifo kilichoamriwa na Mwenyezi MUNGU.
Hauko peke yako, mpo wengi. Hata chanjo za zamani pia ni wengi tu hawakuchanja. Ila corona ukimpeleka nyumbani kwako si rahisi kumalizana na wewe peke yako. Atakamata na wengine pia.
 
Hata kama chanjo ni ya majaribio?
 
Yani kwamba hata mtu ambaye hana dalili zozote za corona akitaka kuchanja anashauriwa akapime kwanza na akionekana hana corona ndio aje kuchanjwa?
 
Hauko peke yako, mpo wengi. Hata chanjo za zamani pia ni wengi tu hawakuchanja. Ila corona ukimpeleka nyumbani kwako si rahisi kumalizana na wewe peke yako. Atakamata na wengine pia.
Kwa hiyo nikichanja siwezi kuambukizwa corona?,je siwezi kuambukiza wengine?,Je nikichanjwa sitalazimika kuvaa barakoa?,Je, nikichanjwa sitalazimika kujizuia na mikusanyiko?,Je, nikichanjwa sitalazimika kuchanja tena chanjo ya COVID-19?.Ukinijibu hoja hizi vizuri, naenda kuchanja hata Sasa hivi.
 
Hata kama chanjo ni ya majaribio?
Ngoja tuanze na hii chanjo ya J&J. Hii chanjo inatumia teknolojia ya zamani. Teknolojia ambayo usalama wake na makandokando yake unajulikana vema. Hivyo chanjo kama hii haihitaji utafiti au majaribio ya muda mrefu kujua madhara na ufanisi wake.

Chanjo hii ni aina ya Viral vector. Hapa kirusi aliyepunguzwa nguvu au aliyeuwawa huchomwa ndani ya mtu. Mwili unagundua uvamizi na kutengeneza kinga. Siku nyingine kirusi chenyewe kikija, kinga inakuwepo tayari. Teknolojia hii inajulikana vema. Wanasema, "hakuna haja ya kugundua gurudumu kwa mara ya pili." Teknolojia imekuwa, vitu vingi vinajulikana. Mambo yanaweza kwenda fasta. Hivyo siyo majaribio, watu wanauhakika wa asilimia nyingi ya kile kinachofanyika.
 
Njia nzuri ni kujenga uwezo wa wataalam katika kufanya utafiti ili kupunguza utegemezi
 
[ Hata Gwajima ana hoja hiyo. Nenda post number nne usome paragraph ya mwisho.
 
Wewe nenda kachanje
 
Hoja yangu ni kuwa, hoja za Gwajima na Polepole hazina mashiko na kuchanja ni jambo la akili.
Utajiandaa kuchanja mara ngapi maana kama wanatengeneza wataendelea kutengeneza zaidi na zaidi
 
Yani kwamba hata mtu ambaye hana dalili zozote za corona akitaka kuchanja anashauriwa akapime kwanza na akionekana hana corona ndio aje kuchanjwa?
Ambaye hana dalili halazimiki.
 
Utajiandaa kuchanja mara ngapi maana kama wanatengeneza wataendelea kutengeneza zaidi na zaidi
Kama kirusi kitaendelea kubadilika badilika itatubidi kuchanja mara nyingi tuwezavyo. Chanjo ya Typhoid huchanjwa kila baada ya miaka 5 kamq sijakosea.

Lakini watu wengi wakichanjwa, tunapunguza mazalia ya virusi kubadilikabadilika, na inawezekana kukitokomeza kamq polio au ndui.
 
Yap, kama hivyo. Kuwa delta, Mu nk.
Sasa mbona chanjo pia hazizuii kupata maambukizi na kuambukiza? sasa hapo tutazuia vp hiyo hali ya virusi kubadilika badilika? na kuhusu afrika je kwanini mpaka sasa haijawa kuwa ndio uwanja wa virusi Kumutate kwa sababu tuko nyuma kwenye kuzuia maambukizi na hata kasi ya kuchanja chanjo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…