Hoja ya Spika Ndugai: Nitawafukuzaje wabunge ambao Rufaa zao hazijasikilizwa na Baraza kuu kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA?


Maelezo yako yana mantiki, possibly ndicho Chadema wanacho kikwepa.

Maana mahakama ikizuia utekelezaji wa kuvuliwa uanachama, baadhi ya covid-19 ambao ni wajumbe wa kamati kuu waendelee kuhudhuria vikao vya chama kama kawaida huku wakiwa mguu mmoja CCM na mguu mwingine CDM.
 
Ndungai anajichanganya kwa kudai muhtasari wa kikao kilicho wasimamisha Halima na wenzake,lakini hazungumzii muhtasari wa kikao cha Chadema kilichowateua.
Aidha Ndungai anajulikana kwa dharau zake na upindishaje wa wazi wa sheria za nchi,sote ni mashahidi pale alipomrudisha bungeni mbunge Mwambe ambaye alikuwa amepoteza ubunge wake baada ya kujiunga na CCM akitokea Chadema.
 
Hao chadema wako very very selfish Yani wew mwanaume unapigania mwanamke afukuzwe kazi yake kisa wew huna that's very foolishness and stupidity, Spika kawajibu kwa hoja sana sana huwezi tu kumfukuza kazi mtu hivi hivi bila a fair justice never..
Wameshtuka sasa hivi wanatumika Bawacha ya Mbeya....wanasoma tamko lenye mwandiko wa kiume
 
Kipi kinatangulia kati ya kuvuliwa Ubunge na kusikilizwa rufaa?
Hapo kinachotangulia ni majina ya waliopendekezwa na kamati kuu ya Chadema kupelekwa kwenye Tume ya uchaguzi.
Kitu ambacho hakikufanyika,badala yake taasisi za serikali zikafanya uhuni wa kugushi nyaraka.
 
Spika Ndugai yuko sahihi.

Moja ya Haki za Mwanachama kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA (2016):5.2.4 Kujitetea, kusikilizwa na kukata rufaa anaposhitakiwa ama kuchukuliwa hatua za kinidhamu kichama.

Wanaodaiwa kufukuzwa walikata rufaa ambayo hadi sasa haijasikilizwa. Na kwa kuzangatia Viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakidai demokrasia, ni wakati mwafaka wa wao kuonyesha demokrasia ndani ya chama.

Kwa sababu hizo hao bado ni wanachama halali wa CHADEMA hadi hapo rufaa yao itakaposikilizwa.
 
Nimekuelewa bwashee!
 
Bwasheee buku 7 tangu uzikose umekua hufikirii kabisa. Issue kubwa sio rufaa wala nini. Issue ni...walipelekwaje huko bungeni na kuapishwa. List ilitoka wapi? Walijichukulia uamuzi na kushirikiana na serekali dhaifu wakatengeneza list yao hao ma covid 19. Wamefukuzwa hasa hasa kwa hilo. Na huo ndio mzizi wa fitna. Nani aliwapitishaaaaaaaaa???? this is the stem of the problem in hand that led to their being fired.
 
Spika aache blabla, Rufaa haitengui hukumu hadi hapo Rufaa itakapo elekeza vinginevyo.

Alipe GHARAMA ZA KIBURI CHA MADARAKA.
 
Sehemu yoyote ile ya kazi, ukifukuzwa inabidi uondoke hapo sehemu ya kazi - iwe kufukuzwa kwako kumefuata utaratibu au la - na kama mhusika ataona utaratibu wa kufukuzwa haukufuatwa, atakata rufaa na kukata rufaa huwa hakuna maana kwamba mgogoro umeisha, bali ni fursa kwa mwathiriwa kujiridhisha kama ABC za kufukuzwa kwake zimefuata utaratibu au la. Siyo desturi ya mtu kufukuzwa sehemu na kung'ang'ania kubaki hadi hapo rufaa yake itakaposikilizwa. Kwa upande wa hao wabunge 19 waliofukuzwa na chama chao, ilibidi waheshimu uamuzi wa chama chao na wakate rufaa kama walivyofanya - na kukata rufaa ina maana kwamba wanakiri kuwa walishafukuzwa na kama walishafukuzwa na wamakiri hivyo kwa kukata rufaa, then wamekosa sifa za kuwa wabunge na ilibidi wasiwepo bungeni kama wabunge, otherwise hakuna mantiki ya wao kukata rufaa kama chama hakijawafukuza na hakuna mantiki ya kubaki bungeni kama walishafukuzwa na kuonyesha kwamba wamefukuzwa wamekata rufaa.
 
Hivi kwani Chadema wakiteua wabunge na kuwapeleka Bungeni badala ya waliopo kuna tatizo gani?
Je ni lazima kina Halima na kundi lake ndio lazima wawe wao tu ?
Ina maana kina Halima na kundi lake ni wakubwa kuliko Katiba ya Chadema?
Ina maana kanuni,taratibu za Bunge pamoja na katiba za vyama vya siasa ni kubwa /muhimu kuliko Katiba ya nchi?
 
Iblis namba moja ameshatangulia yy namba mbili hv punde tu atafuatia
 
Unakuwa mbunge baada ya kuapishwa na Spika. Chadema hata wakiteua wengine na NEC wakayapeleka majina kwa Spika, Spika akigoma kuwaapisha ndio basi tena.

Ukimya wa NEC baada ya kukiri kuwa hawajapokea barua kutoka Chadema speaks volume. Wangekuwa huru wangeweza kumaliza mgogoro huu kwa kuweka wazi barua waliotumia kupeleka majina kwa Spika au wangesema hawajapeleka majina yeyote kwa Spika.

Amandla...
 
Kuthibitisha km waliteuliwa ama hawakuteuliwa ni kazi ya tume na sii spika wala bunge,
 
CDM hawaelewi nini wanataka

Ukishindwa kudai haki yako kwa njia sahihi/ kufuata taratibu stahiki hutoipata na utajihisi unaonewa, kumbe wewe mwenyewe ndio unajionea pasipo kujua
 
Mnyikia ni mhuni halafu hajui kuwa mbowe anajuwa ishu yote ndiyo maana kakaa kimya amebakiyeye na BAWACHA.
Huu ni msigano wa makundi mawili hasimu ndani ya chadema. Kundi la mbowe ambalo ndilo liliridhia huo uteuzi kwa kulizunguka kundi la lisu ambalo lilitaka kila kitu kisusiwe baada ya matokeo ya uchaguzi. Mnyika yuko kundi la lisu!
 
CDM hawaelewi nini wanataka

Ukishindwa kudai haki yako kwa njia sahihi/ kufuata taratibu stahiki hutoipata na utajihisi unaonewa, kumbe wewe mwenyewe ndio unajionea pasipo kujua
Wanajielewa sana. Wanafanya hivi kutokana na experience yao. Wamefuata njia sahihi ya kumuandikia Spika nini kimetokea na wamepata nini?
Mara nyingi mtu ambae una uhakika amekudhulum akikuambia fuata njia fulani ili upate haki yako ujue kuwa hiyo njia anaimiliki na ana jua hutafika popote.

Ni bora waendelee kufanya wanachofanya kuliko kuingia gharama za kufungua mashtaka ambayo hatma yake wanaijua.

Amandla...
 
Huu ni msigano wa makundi mawili hasimu ndani ya chadema. Kundi la mbowe ambalo ndilo liliridhia huo uteuzi kwa kulizunguka kundi la lisu ambalo lilitaka kila kitu kisusiwe baada ya matokeo ya uchaguzi. Mnyika yuko kundi la lisu!
Wahusika wanaku - zoom tuu mkuu
 
hawajaambiwa wafungue mashtaka, wameambiwa wapeleke viambatanishi vya madai yao & hiyo ni kwa mujibu wa katiba yao
 
hawajaambiwa wafungue mashtaka, wameambiwa wapeleke viambatanishi vya madai yao & hiyo ni kwa mujibu wa katiba yao
Katiba ambayo Spika haijui maana ametaka apelekewe nakala? Hamna Katiba ya Chadema inayozungumzia viambatishi. Na Chadema hawajampelekea Spika madai bali wamempa taarifa. Wanachokidai sasa ni afuate Katiba ya nchi ( sio ya CDM) inavyosema kuhusu sifa ya mbunge.

Amandla..
 
Pia anashangaa wao kufukuzwa na chama wakati yeye alikuwa akiwafukuza baadhi yao bungeni na kutohudhuria vikao vya bunge miezi kadhaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…