Mawazo mazuri sana mkuu. Mimi nina machache yakusema, natumai utaelewa huu ni katika kuelewa zaidi. Swali la msingi la thread ni jee hii mbunge kuwa waziri haileta conflict of interest? Kwa maana mtu akiwa waziri atumikie taifa ua jimbo? Pia mtu akiwa waziri aka fanya vitu fulani jimboni kwake haita onekana upendeleo? Na je aki hudumia taifa akaiacha jimbo lake si ata kuwa kawa angusha wananchi? Wewe umebase sana kwenye uraisu lakini hauja jibu hoja ya kuwa mbunge kuwa waziri ina weza kuleta conflict of interest.
Cha pile ni kwamba je mfumo ukiwa mbovu hi siyo kichocheo cha kupata viongozi wabovu? Kama mfumo ni mzuri haita jenga mazingira ya walau kupata viongozi wengi wazuri hata kama siyo wote. Nakubaliana na wewe kama viongozi ni ovyo basi haki tendeki kitu lakini pia mfumo ukiwa mbaya basi kupata viongozi wazuri ni ndoto.
La tatu na la mwisho ni kwamba hauoni raisi ni tatizo? Je serikali yoyte kutokuwa na checks and balances halita leta tatizo? Umesema mwenyewe kuwa raisi anaweza kuwa hata dikteta. Kwa maana hiyo mayai yote tume weka kwenye kikapu kimoja, raisi akiwa ovya ndiyo basi tena tusha kula hasara. Kuwa na balance of power hauoni ni muhimu kuzuia raisi, mtu mmoja kuwa dikteta? Kwa ulivyo sema wewe basi raisi akiwa corrupt na serikali nzima ita kuwa corrupt.
Kama nilivyo sema mwanzo asante sana kwa maoni yako mkuu.
Mbunge wa kuchaguliwa na wananchi atawajibika kwa wananchi wa jimbo lake. Je akiteuliwa uwaziri ambapo anatakiwa kuwajibika kwa rais aliyemteua Ubunge wake utakuwaje?
La kujiuliza zaidi ni kuwa, je rais anawajibika kwa nani? Ikiwa rais anawajibika kwa wananchi, waziri vile vile atawajibika kwa wananchi. Suala hapa ni wananchi gani wa jimbo lake au wa nchi nzima?
Ndo maana nasema huwezi kujadili hili bila kujadili package nzima. Yaani ikiwa mbunge ameteuliwa kuwa waziri, kazi yake ya uwaziri itatawaliwa na utekelezaji wa sera za serikali inapokuja suala la kuleta maendeleo. Kwanza tukubaliane maendeleo hayaletwi na serikali. Maendeleo huletwa na watu. Mbunge kama muwakilishi analo jukumu la kulobby serikalini kuhakikisha eneo lake linapewa kipaumbele inapokuja kwenye vitu vinavyosaidia kupush maendeleo kama miundo mbinu yaani bara bara, maji, umeme, n.k. Je anapokuwa waziri uwezo wake wa kulobby kwa ajili ya jimbo lake umepunguzwa au umeongezwa? Umeongezwa, hivyo kwa wanajimbo hii ni plus. Lakini kwa nchi nzima je?
Sasa hapa tunajadili mbunge waziri. Je hakuna mkabala wa maslahi katika kulitetea jimbo lake kama mbunge, na kutekeleza sera za serikali kama waziri? Ni kweli kuwa utendaji wa kazi kama waziri utamtaka aangalie picha kubwa zaidi, yaani nchi nzima. Hapa ndo linapoingia suala la urais. Anapotekeleza majukumu yake kama waziri anawajibika kwa rais.
Ikiwa kweli rais ni wa watu wote na anawajibika kwa wananchi wote suala la mbunge waziri kutekeleza vipaumbele vya serikali haliwezi kuleta mgogoro. Wananchi wa jimbo lake hawawezi kulalamikia kupokwa muwakilishi wao na serikali kwani uwezo wake wa kulitetea jimbo umeongezeka. Sasa jee huyu waziri hataweza kulipendelea jimbo lake tuu ukizingatia kuwa watu wa jimboni kwake ndo wanaompa kura za kurudi serikalini (kwani akikosa kura na uwaziri basi)?
Hili litajibiwa na uongozi mzima. Rais akiwa mkuu wa serikali anayewajibika kwa wananchi wote anao wajibu wa kuwa na vipaumbele vya kitaifa ambavyo kutekelezwa kwake husimamiwa na mawaziri. Vipaumbele vya kitaifa vinaweza visiwe kwenye vipaumbele vya jimbo moja moja. Lakini vile vile ni wajibu wa serikali kuhakikisha majimbo yanajua kuwa yenyewe ni sehemu ya Taifa kubwa. Hapo ndipo linapokuja suala la uongozi bora. Uongozi bora unaosimamia masuala yote ya kitaifa kwa vipaumbele kama inavyotakiwa uta-galvanize public trust. Kukiwa na public trust suala la utendaji wa mbunge mmoja mmoja haitakuwa issue. Mafanikio ya serikali yatapimwa kwa jinsi ambavyo imeweza kushughulikia vipaumbele vya kitaifa. Hata kama havitakuwa na matokeo ya moja kwa moja kwa jimbo la mhusika bado hakuna tatizo hapo.
Tatizo linakuja pale ambapo vipaumbele vya kitaifa vimemezwa na udhaifu mkubwa uliomo ndani serikali kiasi cha watu kuamini kuwa bila kuwa na muwakilishi serikalini hakuna kitakachoendelea katika majimbo yao. Hapo ndipo tulipofika. Lakini sasa tukishafika hapo, muwakilishi bungeni hana maana, kwa sababu Bunge halitekelezi vipaumbele. Muwakilishi serikalini ndo anakuwa na maana zaidi.
Kwa kifupi ni kuwa, ikiwa serikali inasimamia na kutekeleza vipaumbele vya kitaifa, whether jimbo lina uwakilishi wa moja kwa moja Bungeni, Au mbunge wao amekuwa waziri haitakuwa na matatizo kwani serikali yenye ufanisi lazima itafika kama si leo kesho.