Hoja ya waziri wa fedha ni changa la macho lakini haiokoi jahazi

Hoja ya waziri wa fedha ni changa la macho lakini haiokoi jahazi

geomos

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2014
Posts
625
Reaction score
175
Unajua nimesikiliza waziri Saada Mkuya akihojiwa star TV kuhusu kushuka kwa shilingi kwa dola, alijibu hivi "Ni kweli imeshuka kwa dola, lakini pia tumepanda dhidi ya fedha nyingine kama yenu ya Japan nk." Sasa lugha kama hii inaweza kumfanya mzito kuelewa akatuliza boli.

Lakini ukweli hakuna afadhali yoyote, kwa sababu hata hayo magari ya Japan hayauzwi kwa Yen bali dola, lazima wagande nasi, dollar ni gold standard global middle player in money transaction, halafu wanatuamishia Yen, dinar nk. Ni wangapi wanaonunua Yen hapa nchini au kuagiza kwa Yen nje, zaidi ya wajapan wanaojiuza kimadafu wakizisahau kwenye briefcase zao wanapokuja, watafute njia za kuvuna external currency kwa bidhaa zetu.
 
Huyu sister do bunge likianza naona atakuwa kwenye wakati mgum sana kujibu maswali ya akina kafulila na mbatia
 
huyu dada kiukweli hakufaa kuwa waziri wa fedha... mambo ya uchumi yakijibiwa kisiasa ni hovyo kabisa... angeongea hata na gavana ampe hata hints kujua kwa nini shi imeshuka kitaalamu .... si kutoa hoja jepesi kwenye mambo ya msingi
 
Back
Top Bottom