Hoja yangu kuhusu Lengai Ole Sabaya aliyekuwa DC wa Hai

Yaani wewe umekuwa biased kama Sabaya mwenyewe. Yawezekana ulikuwa mnufaika wa udhalimu wa Sabaya na "baba" yake alokwenda zake?

Sent from my SM-A705FN using JamiiForums mobile app
 
Kwenye jinai hakuna nilitumwa, you will personally be held accountable
.... tuliwaambia sana humu; wazingatie sheria waache kumuiga aliyekuwa anawatuma. Yeye alikuwa na kinga ya milele hawakuelewa.
 
... huyu ana tofatuti gani na Shetani? Sijui Magufuli alikuwa anayatoa wapi haya majambazi na kuyapa madaraka! Very funny!
 
Naongezea hapo,
Kwanini yeye na siyo wengine wenye kazi kama yake katika mkoa huohuo?
 
Mfumo uliokuwepo uliruhusu na kuwapenda wanaokosea. Sabaya hakujua kuwa kuna mwisho
 
mifumo imetengenezwa na wanadamu na watekelezaji ni wanadamu. Huwezi ukaua watu ukalaumu ruhusa ya mfumo. Mimi ni mkazi wa hai. Nadiriki kusema huyu kijana hana tofauti na majambazi wa silaha au kibaka. Ushahidi uliopo unatosha kufanya wananchi kuchukua sheria mikononi. Nashauri aendelee kuzuiliwa hapa mabatini polisi kwa usalama wake
 
Kuna msemo unasema ukitumwa kafanye ukitumikishwa kataa
Huyu alitumikishwa akafanya leo yuko alone.
Huo mfumo ulikuwa kwa sabaya tu? Mbona zaidi ya asilimia 90 hawako hivyo? Ingekuwa mfumo tungeona zaidi ya ma dc 70 wako hivyo lakini siyo. Hivyo tatizo NI sabaya siyo mfumo
 
Mleta mada akili yako ni ndogo sana kuliko ya Sabaya ! Mfumo ndio ulimtuma kuajiri vibaka na kuwapa silaha!
Kwa elimu aliyonayo Sabaya, alifundishwa wapi au ni sheria ipi inampa DC mamlaka ya kumkamata nakumpiga mtuhumiwa !
Tanzania ina watu wajinga hadi wanatia kinyaa kama huyu mleta mada sijui Ndabila!
Sabaya anavuna alichopanda !
 


Kumbe kuna: KUTUMWA na KUTUMIKISHWA???!🤔
 
Ni vyema ungekaa kimya. Next time akisimamishwa mwingine, kuliko kutoa hoja ya "mfumo" kaa kimya mkuu.
 
Naomba niulize jamani, huyu jamaa anazungumzia mfumo gani ambao ulimfanya huyu jamaa kutenda mambo ya ovyo akiwa kwenye ofisi ya umma?
Anadai kua haoni kosa kwani mamlaka zilizomteuwa ziliyabariki!.
 
Umeandika maneno mengi yenye wazo moja tu ambayo yangebebwa na sentensi mbili za mwisho.

Labda ueleweshwe tu, hakuna mwanasiasa mwenye kuzingatia sheria, utawala bora nk ila lengo lake kuu kuridhisha kundi kubwa la kumuunga mkono kushughulikia jambo fulani linalowagusa na kuwakwamisha wananchi. Pili kutenda kuendana na mvumo wa upepo wa mahitaji ya kisiasa kwa wakati husika.

Safisha anayoitumia SSH kwa sasa ndiyo itakayomchafua asisafishike huko mbeleni na atatamani mrejeo kwenye uchafu alioutoa lakini haitawezekana kwa kuwa uchafu utabadilika kuwa sumu dhidi yake
 

Na waende tu. Watu wameuwawa, wameumizwa, wamepotezwa, wamefilisiwa, wamefungwa na ya namna hiyo. Watu gani hawa?

Hata kama mheshimiwa kabisa Majaliwa naye kahusika, hakuna kumwangalia mtu usoni. Wote hao mama, sukuma ndani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…