Hoja Yangu Leo: Lazima Timu ya Simba ifanye Usajili wa Golikipa

Mawembasa1979

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2015
Posts
2,540
Reaction score
3,333
Ni muda mrefu sasa mimi kama mpenzi na shabiki wa mpira wa miguu ambao ni mchezo namba 1 kupendwa sana duniani na Tanzania ikiwemo, nimekuwa nikifuatilia mechi mbalimbali za mpira wa miguu hapa nchini na duniani kwa ujumla. Hakuna ubishi, Timu ya Simba ina kikosi bora katika msimu huu ingawa kwa kiasi fulani kinawavunja moyo na nguvu wanachama, mashabiki na wapenzi wake (Simba Fans) kutokana na kucheza “kifarther” zaidi.

Nikijikita kwenye hoja yangu naomba leo tujadili kuhusu nafasi ya Golikipa katika Timu ya Simba. Binafsi, nimewaangalia Magolikipa wote watatu wa Simba Manula, Munishi na Salim. Bila ubishi katika hao watatu mwenye uwezo mkubwa ni Manula hasa kwa kuangalia takwimu (statitstics) ya aina ya mechi anazocheza ikilinganishwa na wenzake. Nimeuangalia udakaji wa Munishi ni kama vile hayupo sawa kisaikolojia. Maana anadaka mpira as if hayupo uwanjani. Hata anapokuwa amedaka mpira au ameukosa unamwona anasemasema peke yake (refer match ya Mashujaa FC). Huyu mwingine anaitwa Salim ndio hayuko fit kabisa kama mlimwona jana kwenye mechi na Chipukizi ya Pemba alikuwa anababaika sana. Kama usingekuwa uimara wa backline yake nadhani tungeyaona mengine jana.

Sasa basi, kwa muktadha huo unaona kuwa ikitokea iwe kwa bahati mbaya au nzuri Manula asiwepo langoni hali ya Timu ya Simba kimchezo itakuwa tete. Hasa kwenye kipindi hiki ambacho Simba inakabiliwa na Michuano Mikubwa na yenye manufaa kwa vilabu vya Afrika. Ikiwezekana Simba wafanye mazungumzo na Yanga ili wamuongeze Benno Kakolanya kwenye kikosi chao maana naona Yanga ni kama wamemtosa. Hasa katika michuano hii ya Champions League maana timu kwa kipindi fulani huruhusiwa kuongeza wachezaji watatu kama sikosei.

Tofauti na hayo Wana Simba mjiandae kisaikolojia ikiwa Manula hatakuwepo langoni.

Nakaribisha mjadala.
 
Ulipoandika wamuongeze beno tu Uzi wako ukawa takataka tayari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana ya kujadili ndugu. Hata hivyo, magolikipa ambao wana kiwango bora kwa sasa kwenye ligi kuu bara ni Manula na Kakolanya. Vilevile ndio magolikipa wa Timu ya Taifa (Taifa Stars). Ila si mbaya Mkuu ondoa ya Benno fanyia kazi hayo mengine utauona ukweli ndani yake.
 
Manager wa Beno ni kiongozi wa Simba. Kamshauri Beno agome. Matokeo yake amekaa pembeni.
Hata Simba ikimchukua, yatampata ya Dida. Mchezaji bila mechi na hasa golikipa, kiwango huporomoka haraka.
Simba hawana uvumilivu huo. Itakuwa ndiyo mwisho wake.
 
Kachukueni wa golikipa wa Nkana maana mmefanya figisu mkamdanganye Beno agome sasa mnamzungusha
 
Fikiria Yanga ubingwa mara tatu mfulilizo ingekuwa Mikia. Haji Mzungu angepasuka mdomo
Ingekuwa ajabu kama uzi huu ungefikisha post 20 bila watu kuweka historia na jografia za timu zao
 
Afadhali unalijua hilo.
Liverpool long time hawajachukua ubingwa EPL. Lakini wanafuatia kwa Man U kubeba ndoo za EPL. Hadi leo inawapa jina kubwa duniani.
27 kwa 19 ni parefu sana. Labda karne ijayo tutakuwa sawa.
 
Mimi huwa nina mtazamo tofauti na baadhi ya mashabiki (nimesema baadhi). Kwa timu za nchi zetu za kimaskini kuweza kujiendesha kiendelevu, timu inatakiwa iwekeze ili ivune mamilioni ya CAF. Ili upate mamilioni hayo, lazima ushiriki michuano ya CAF kwa mafanikio. Kwangu mimi, kuchukua ubingwa wa Tanzania kisha kutolewa raundi ya kwanza CAF ni hasara kubwa na kuna siku hela itakata tu. Naamini ubingwa wa ligi ya Tanzania ni tiketi ya kushiriki kwa mafanikio ligi za CAF clubs, na sio kuhifadhi historia halafu unafilisika
 
Tatizo ni pale unapomweka mtu benchi hadi anapoteza confidence na ability. Na hata Salamba watamuua hivyo hivyo kwa kumbania nafasi ilhali kuna boya mmoja,mcheza hovyo (John Bocco) anapendelewa kupitiliza.
 
Manula mipira ya Kona hajui kucheza, alafu anafungwa sana mashuti ya mbali sababu na kimo chake. Kaseja alikuwa hana kimo kirefu lkn alikuwa anajua kuji position.
 
We hujui soka na hata Falsafa za Walimu huzijui. Wako wapi Akina Hussein Javu, Bahanuzi, Malimi Busungu, Paul Nonga, Emmanuel Martin nk nk ambao waliiingia wakiwa fire wakatoka wakiwa mfu kisoka. Tuache ushabiki tuwaachie walimu kazi yao.
 
Tatizo ni pale unapomweka mtu benchi hadi anapoteza confidence na ability. Na hata Salamba watamuua hivyo hivyo kwa kumbania nafasi ilhali kuna boya mmoja,mcheza hovyo (John Bocco) anapendelewa kupitiliza.
Hata kwenye Kombe la Mapinduzi Bocco kiwango chake kipo chini.
 
Manula mipira ya Kona hajui kucheza, alafu anafungwa sana mashuti ya mbali sababu na kimo chake. Kaseja alikuwa hana kimo kirefu lkn alikuwa anajua kuji position.
Hakuna kipa bora kama Manula Tz hii, na hakuna kipa ambae hafungwi. Tatizo la mashabiki maandazi hasa wa Simba kipa akidaka kwa muda mrefu tu tatizo, nakumbuka miaka ya mwisho ya Kaseja simba alivyokua anatukanwa na mashabiki. Kila kipa anafungwa magoli ya kizembe, hata De Gea huwa anafungwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli Simba kuna tatizo la kipa, Manula mzuri ila mashuti ya mbali hasa yale ya adhabu za kutenga huwa anafungwa sana, pia Okwi na bocco naona pia viwango vyao hiviko sawa.
 
Hakuna kipa bora kama Manula Tz hii, na hakuna kipa ambae hafungwi. Tatizo la mashabiki maandazi hasa wa Simba kipa akidaka kwa muda mrefu tu tatizo, nakumbuka miaka ya mwisho ya Kaseja simba alivyokua anatukanwa na mashabiki. Kila kipa anafungwa magoli ya kizembe, hata De Gea huwa anafungwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata katika wodi ya vichaa Kuna mwenye afadhali, Manula si mzuri na hajawahi kukikaribia kiwango cha Kaseja, huo ndio ukweli sisi mpira tunatizama na tunaona, Manula mbovu mipira ya juu na Mashuti hajui kuji position wala timing hana upande wa mashuti. Sasa subirini wenzake wa kwenye kundi wajue weakness yake alafu utaona atakavyotunguliwa.
 
Back
Top Bottom