Hoja Yangu Leo: Lazima Timu ya Simba ifanye Usajili wa Golikipa

Ni muda mrefu sasa mimi kama mpenzi na shabiki wa mpira wa miguu ambao ni mchezo namba 1 kupendwa sana duniani na Tanzania ikiwemo, nimekuwa nikifuatilia mechi mbalimbali za mpira wa miguu hapa nchini na duniani kwa ujumla. Hakuna ubishi, Timu ya Simba ina kikosi bora katika msimu huu ingawa kwa kiasi fulani kinawavunja moyo na nguvu wanachama, mashabiki na wapenzi wake (Simba Fans) kutokana na kucheza “kifarther” zaidi.

Nikijikita kwenye hoja yangu naomba leo tujadili kuhusu nafasi ya Golikipa katika Timu ya Simba. Binafsi, nimewaangalia Magolikipa wote watatu wa Simba Manula, Munishi na Salim. Bila ubishi katika hao watatu mwenye uwezo mkubwa ni Manula hasa kwa kuangalia takwimu (statitstics) ya aina ya mechi anazocheza ikilinganishwa na wenzake. Nimeuangalia udakaji wa Munishi ni kama vile hayupo sawa kisaikolojia. Maana anadaka mpira as if hayupo uwanjani. Hata anapokuwa amedaka mpira au ameukosa unamwona anasemasema peke yake (refer match ya Mashujaa FC). Huyu mwingine anaitwa Salim ndio hayuko fit kabisa kama mlimwona jana kwenye mechi na Chipukizi ya Pemba alikuwa anababaika sana. Kama usingekuwa uimara wa backline yake nadhani tungeyaona mengine jana.

Sasa basi, kwa muktadha huo unaona kuwa ikitokea iwe kwa bahati mbaya au nzuri Manula asiwepo langoni hali ya Timu ya Simba kimchezo itakuwa tete. Hasa kwenye kipindi hiki ambacho Simba inakabiliwa na Michuano Mikubwa na yenye manufaa kwa vilabu vya Afrika. Ikiwezekana Simba wafanye mazungumzo na Yanga ili wamuongeze Benno Kakolanya kwenye kikosi chao maana naona Yanga ni kama wamemtosa. Hasa katika michuano hii ya Champions League maana timu kwa kipindi fulani huruhusiwa kuongeza wachezaji watatu kama sikosei.

Tofauti na hayo Wana Simba mjiandae kisaikolojia ikiwa Manula hatakuwepo langoni.

Nakaribisha mjadala.
Acha waendelee kuwa na wadaka panzi tu na saiz wameongeza mkata viuno Zena
 
We hujui soka na hata Falsafa za Walimu huzijui. Wako wapi Akina Hussein Javu, Bahanuzi, Malimi Busungu, Paul Nonga, Emmanuel Martin nk nk ambao waliiingia wakiwa fire wakatoka wakiwa mfu kisoka. Tuache ushabiki tuwaachie walimu kazi yao.
Tatizo hawa kandambili wanajisahaulisha sana Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We hujui soka na hata Falsafa za Walimu huzijui. Wako wapi Akina Hussein Javu, Bahanuzi, Malimi Busungu, Paul Nonga, Emmanuel Martin nk nk ambao waliiingia wakiwa fire wakatoka wakiwa mfu kisoka. Tuache ushabiki tuwaachie walimu kazi yao.
Akina Dan Serunkuma wako wapi. Alikuwa on fire akiwa Kenya. Simba kiwango kikafa. Sasa yupo vizuri tena kwao Uganda.
 
Tatizo ni pale unapomweka mtu benchi hadi anapoteza confidence na ability. Na hata Salamba watamuua hivyo hivyo kwa kumbania nafasi ilhali kuna boya mmoja,mcheza hovyo (John Bocco) anapendelewa kupitiliza.
Una maanisha John Boko! Pamoja na madhaifu yake ,hakuna kocha mwenye akili timamu anaweza thubutu kumwacha
 
Ni muda mrefu sasa mimi kama mpenzi na shabiki wa mpira wa miguu ambao ni mchezo namba 1 kupendwa sana duniani na Tanzania ikiwemo, nimekuwa nikifuatilia mechi mbalimbali za mpira wa miguu hapa nchini na duniani kwa ujumla. Hakuna ubishi, Timu ya Simba ina kikosi bora katika msimu huu ingawa kwa kiasi fulani kinawavunja moyo na nguvu wanachama, mashabiki na wapenzi wake (Simba Fans) kutokana na kucheza “kifarther” zaidi.

Nikijikita kwenye hoja yangu naomba leo tujadili kuhusu nafasi ya Golikipa katika Timu ya Simba. Binafsi, nimewaangalia Magolikipa wote watatu wa Simba Manula, Munishi na Salim. Bila ubishi katika hao watatu mwenye uwezo mkubwa ni Manula hasa kwa kuangalia takwimu (statitstics) ya aina ya mechi anazocheza ikilinganishwa na wenzake. Nimeuangalia udakaji wa Munishi ni kama vile hayupo sawa kisaikolojia. Maana anadaka mpira as if hayupo uwanjani. Hata anapokuwa amedaka mpira au ameukosa unamwona anasemasema peke yake (refer match ya Mashujaa FC). Huyu mwingine anaitwa Salim ndio hayuko fit kabisa kama mlimwona jana kwenye mechi na Chipukizi ya Pemba alikuwa anababaika sana. Kama usingekuwa uimara wa backline yake nadhani tungeyaona mengine jana.

Sasa basi, kwa muktadha huo unaona kuwa ikitokea iwe kwa bahati mbaya au nzuri Manula asiwepo langoni hali ya Timu ya Simba kimchezo itakuwa tete. Hasa kwenye kipindi hiki ambacho Simba inakabiliwa na Michuano Mikubwa na yenye manufaa kwa vilabu vya Afrika. Ikiwezekana Simba wafanye mazungumzo na Yanga ili wamuongeze Benno Kakolanya kwenye kikosi chao maana naona Yanga ni kama wamemtosa. Hasa katika michuano hii ya Champions League maana timu kwa kipindi fulani huruhusiwa kuongeza wachezaji watatu kama sikosei.

Tofauti na hayo Wana Simba mjiandae kisaikolojia ikiwa Manula hatakuwepo langoni.

Nakaribisha mjadala.
yule beki wa kulia kweli alitoka Ivory cost au ujanja ujanjanja wa mjini? mbona lizito vileee
 
Back
Top Bottom