Hoja yenye mashiko

Hoja yenye mashiko

Jeef George

Member
Joined
Dec 7, 2019
Posts
47
Reaction score
60
Habrini wana jamii forum wenzangu natumaini hamjambo kwa sababu Mungu yupamoja nasi !

Kuna time najiuliza kuhusu nchi yangu ya Tanzania kwa tathimini yakufikiri sana,
Maisha walioishi mababu enzi za ukoloni na maisha ya sasa kunautofauti mkubwa sana pia changamoto hazikosekani .
Katika maisha nimejifunza mengi mnoo mengine ninapenda kushare nawewe japo kidogo kwa kuleta hoja katika jukwaa hili la siasa.

Maisha yetu ya kila Siku
hatuwezi kuishi bila .bila siasa
Na wanasiasa ndio wamechukua headlines za taifa moja au jingene.

Any way kusu.dio langu haswa sio porojo za hapo juu nimeelezea tu kama utangulizi

TOZO,KODI.,WAMACHINGA

Kuna kiongozi moja amewahi kusema "WAMACHINGA HAWALIPI KODI"

kwa hakili zangu za darasa la saba Leo nataka tufanye hesabu kidogo naomba nieleweke


Lessen zilizokuwa zinalipiwa na wamachinga kwa Tsh20,000/=
Sasa Fanya hivi
20,000×mamachinga 200,000=?
Yaaani Fanya hii hesabu lessen moja ilikuwa inalipiwa 20,000/=
Tanzania kuna watu 60million
Kwa makadilio ya chini tu, na kwahesabu zangu zangu za hivyo hivyo,
Tufanye hivi wamachinga lakimbili
Kisha zidisha kwa elfu 20

200,000×20,000=4billion


Nimesikitihwa na baadhi ya viongozi kudharau kukejeri wamachinga wakati huo wakisemwa vibaya na kudharauliwa wakati kodi wanalipa na kufanya biashara kwa shida huku uonevu umejaaa,
jana wamachinga wamevunjiwa vibanda vyao vigunguti na bidhaa zao kuchukuliwa na maasikari ni nini hatima yao!!


unakuta wanafamilia zao wengine kula kwao ni mala moja kwa Siku tu
Umewavunjia vibanda vyao watakaa wapi ?
Umewapiga na milingu msaada wao waupate wapi?
Bado kuna kodi ya Nyumba bill za umeme na maji,
biashara hakuna wanaishije hao watu?
Bado wanateseka kuvunjiwa vibanda na kunyimwa haki yao ya msingi katika msitakabali wa haki zao za msingi inaumiza sana na inasikitisha sana





unamsikia kiongozi mkubwa katika nchi a.kisema eti kana kwamba WAMACHINGA HAWANA HAKI KUFANYA BIASHARA MAENEO YA MJINI!

Serikari inasababu kwa kina namna ya kuliamgalia hili swala kwa kina na kulitatua kwa jitihada na kwa haki sawa!




leo katika pipita zangu nimemwona mbunge wa morogoro akisema kuna haja ya ya kuweka picha ya Raisi mwanamke na kutengeneza pesa katika hela zet.u ili kumuenzi kuwa raisi wa kwanza mwanamke katika historia ya taifa letu.


nimeshangaaa sana @babutale kuongea hayaaa....



yaani watu wanatumia ushawishi wa nyadhifa zao kupata madaraka ya juu zaidii...


labda niulize kidogo huenda kuna kitu sielewi

wabunge walipokuwa wakiunga mkono swala la tozo za simu hawakuwa wanalijua hili swala kuwa ni zito kwa wananchi na litaleta.msikumo na taswira tofauti?

yaani wananchi waliowapigia kura kwa wingi wako na kutoa muda kuchagua viongozi hasa wabunge mnafika bungeni mnashindwa kuwatetea wananchi wenu wa kila hali mnaunga mkono tu bila kujali .

Duh!!!
kunahaja ya wapinzani Bungeni @bungelajamuhuriyatanzania linahitaji chachu ya wapinzani kabisa.



MWISHO

Kuna haja ya kuwa na katiba mpya yenye malengo ya kubadili sura ya viongozi na wananchi wanao watumikia
Katiba ambayo itakuwa na vitu vifuatavyo....

1.kiongozi yeyote atawajibishwa bila kujali mamlaka na wazifa wake endapo tu hatatekeleza Yale yote aliyoahidi kipindi cha kunadi Sera zake wakati wa kampeni.

2.Raisi kuwajibishwa endapo tu atakeuka wajibu wake na matumizi mabaya ya madaraka yake
Ikiwemo (i?) Rushwa (ili)matumizi mabaya ya fedha na kuhodhi pesa bila mpangilio

3.wananchi kudai haki zao zakimsingi endapo tu wataona kwamba haki zao zinavunjwa na baadhi ya kiongozi au mamlaka husika.

4.Ruksa wananchi kuandamana
Maandamano ya amani na sio ya shali ili kudai haki zao na kutendewa sawa na vile wanahitaji.

5.Marufuku za viongozi baadhi yao iwe wastaafu kusafiri kwenda nje kwa pesa za wananchi .
Yaaani MTU anasafiri kwenda marekani kwa shida zake mwenyewe aaafu serikali igharamike kumsafiriaha maradhi na kila kitu aende na kurudi hiyo iwe ni marufuku yenye kituo kikubwa kama jiwe la mwamba wa maji.

6.Raisi awe na limit kwa ziara zake za nje ndani ya mwaka wa fedha either Raisi ikimlazimu.

Hapa raisi awe na kikomo kwa vijiziara vya hivyo
Unakuta raisi ndani ya miezi mitatu ziara 8 aaafu anatumia Ndege za watanzania walipamabana kulipa KODI kutengeneza nchi yao doooh hii too much.

7.marufuku Raisi kutembea na Ndege kwa ziara za ndani ya nchi endapo itamlazimu atatumia Ndege kwa masirahi ya Tanzania .

8.Marufuku kuvunja muungano wa Tanzania kwa sababu zisizo na mashiko ...
Uhuru na umoja vitumike kuunganisha ngao ya umoja wa watanzania iwe Bara na visiwani
Kama kutakuwa na ulazima wananchi wapige kura na kuridhia kuvunjwa kwa muungano wajamuhuri.
Ikumbukwe kwamba muungano huu sio kwa ajili ya pande moja tu laahasha ni kwaajili ya watanzania wote bara na visiwani..

Katika muungano niongelee jambo muhumu hapa

Muungano una maana kubwa sana katika masirahi mapana ya taifa letu wanaodai kuvunjwa kwa muungano hawana feature za miaka 50ijayo kuna maana nzito katika Muungano.

Ushauri katika Muungano!
Kunabaadhi ya mambo yafuatwe kuweka haki sawa kwa wazanzibari na watanzania upendeleo wa upende mmoja ufe na kurejesha haki sawa mfumo wa mapato ubadilishwe kwani bara na visiwani kuwe na mamlaka sawa mfano!
Zanzibar wakusanye mapato yao ya ndani kuendesha maendeleo yao
Na bara wakusanye mapato yao ya ndani kuendesha maendeleo na uchumi wao kuepusha mkanganyo huo utaepusha muingiliano

Kikubwa Zaidi Uhuru wahaki na wananchi kudai haki iwe ndio siraha pekee ya kuunda katiba mpya yenye manufaa kwa pande zote mbili!

Asante kwa kunisikiliza na kujifunza pamoja nami🙏🙏🙏🙏

Karibu katika Uzi ujao...... Kwaheri!!!!
 
Huenda ukitulia unaweza kuwa na hoja lakini sasa sijui umeandika ukiwa umeghadhabika sana au lah! Rudia mwenyewe kusoma ulichoandika uone kama wewe mwenyewe utaelewa?
 
Hapa ni mwendo wa tengeneza tatizo, kisha tatua tatizo upate kura. Sasa kwa machinga limebuma miji imekuwa kama majalala, kodi za maduka hakuna hawana namna lazima wawaondoe tuu..
Mleta mada umekurupuka duka moja mjini linalipa kodi hadi milioni 10 kulingana na biashara. Hizo milion kumi ni sawa na machinga 500. Hapo bado atalipa paye, sdl, leseni. Hao machinga unaosema hakuna kitu kwa serikali ilikuwa mkurupuko tuu kama kawaida.
 
Pole sana Mmachinga. Ujumbe wako umefika. Utafanyiwa kazi! Ingawa huku mwishoni umevuruga vuruga! Mara Babu Tale, mara Katiba mpya!

Wakati mwingine jikite kwenye ishu moja tu! Mfano Wamachinga kunyanyaswa, basi! Ila hii mambo ya kuchanganya vitu, inasababisha uonekane kama umepaniki sana na huna mpangilio mzuri wa mada zako.
 
Back
Top Bottom