#COVID19 Hoja za Askofu Gwajima kuhusu chanjo ya Corona hazina mashiko, isipokuwa zina agenda nyingine nyuma yake

Binafsi yangu, bado kidooogo kuiamini hiyo chanjo iliyotiliwa mashaka na pia kumwamini kajima lkn AMANI ya MOYO wangu ikiamua nitachanja saaana tu.
 
Wewe umekuja na porojo zaidi nafuu ya Gwajima, nilitegemea uje na majibu ya kisayansi mwenzetu Labda wewe umebobea zaidi kujua long term side effects anazouliza Gwajima kuanzia Labda miaka 5.

Hivyi ni research ipi ulitaka Gwajima athibitishe kwa data wakati chanjo huchukua miaka kadhaa kujua hizo long term effects? Si ndo hofu yake ilipo?
Wewe ndo tuthibitishie Kama unazo data.

Eti Anamchonganisha rais na wananchi,hivyi Gwajima ni wa Kwanza kueleza chanjo Zina madhara? JPM si ndo alikuwa wa Kwanza? Hivyi JPM na wewe na viongozi unaowajua Nani anamfikia JPM kwa kuwa na uchungu na maisha ya Watanzania?.

Ni nchi gani tupe data waliochanjwa hawaambukizi Wala kuambukizwa!

Ni nchi gani watu wake hawafi na Corona baada ya kuchanjwa? Labda Ulaya wanakotengeneza chanjo hawafi?
Unaweza kutupa data?

Je tangu Corona iingie nchini zaidi ya mwaka tumeishi vipi!? Nchi zilizochanjwa wametuzidi Nini?
Zaidi ya lockdown na kuongezeka visa?

Unamtuhumu mtu aliyesema ukweli na Bungeni aliwahi hoji?
Umetumwa na Nani wewe kwa faida ya Nani? Unauchungu na maisha ya watu au ni tumbo lako? Au kicheo chako?
 
Dawa zenyewe zipo kwenye majaribio ndo research yenyewe inafanyika Sasa.
Ndo maana watu walipoanza kuganda damu nchi zilianza kusitisha matumizi ya haadhi ya chanjo.

Au wewe mwenzetu unazo hizo research?
 
Hoja ya chanjo ni vita vya makampuni ya chanjo kuharíbiana
 
Kuna watu nafsi yangu iliwakataa toka day 1 nilipowasikia watu wakiwaongelea na sijawahi kuwakubali kabisaaa. Kwa haraka, baadhi ya watu hao ni:

Edward Lowassa (hata kabla ya tuhuma akiwa Waziri Mkuu)
Humphrey Polepole (hata toka akisifiwa kwenye mijadala ya katiba)
Josephat Gwajima (hata kipindi yuko karibu na CHADEMA)
Mwigulu Nchemba

Najaribu sana kuisikiliza sauti ya kutoka ndani ya nafsi yangu.
 
Sasa kwa vile Serikali haina uhakika na usalama wa hizi chanjo, ndiyo maana imesema KUCHANJA/KUCHANJWA SI LAZIMA. Yaani kila mtu afanye uamuzi wake kwa hiari yake mwenyewe; kwa lugha nyingine nyepesi ni kwamba KILA MTU ABEBE MSALABA WAKE! Serikali haina muda, vifaa wala wataalam wa kufanya hilo unalotaka - la kukuthibitishia usalama wako kwenye hii CHANJO YA UVIKO - 19!
 
Askofu Rashid Gwajima kaupiga mwingi sana,kaishika CCM na Serikali yake pabaya wamebakia kubweka bweka tu lakini hawana cha kumfanya. Gwajima ana'watu'.
 
 
hazina mashiko kwa sababu HAUNA AKILI wewe ni kiranja wa shetani.
 
MWAISEMBA CR najua wewe umeokoka (kama hujaacha bado)
Basi kwa utulivu naomba upitie hii Fact Sheet ya Janssen Covid 19 vaccine. Halafu utakuwa na nafasi pana zaidi ya kuboresha andiko lako.
Usisahau hivi vipengele:

The Janssen COVID-19 Vaccine may prevent you from getting COVID-19. There is no U.S. Food and Drug Administration (FDA) approved vaccine to prevent COVID-19.

WHAT IS THE JANSSEN COVID-19 VACCINE?
The Janssen COVID-19 Vaccine is an unapproved vaccine that may prevent COVID-19. There is no FDA-approved vaccine to prevent COVID-19.

HAS THE JANSSEN COVID-19 VACCINE BEEN USED BEFORE?
The Janssen COVID-19 Vaccine is an unapproved vaccine. In an ongoing clinical trial, 21,895 individuals 18 years of age and older have received the Janssen COVID-19 Vaccine.

WHAT ARE THE BENEFITS OF THE JANSSEN COVID-19 VACCINE?
In an ongoing clinical trial, the Janssen COVID-19 Vaccine has been shown to prevent COVID-19 following a single dose. The duration of protection against COVID-19 is currently unknown.

Mengine utayasoma humo. Unaweza tafuta Fact Sheet za chanjo nyingine pia ukaona yaliyomo. Naamini kwa haya machache utaboresha zaidi bandiko lako ili huu mjadala uwe wa kitaalam zaidi ya kisiasa na malumbano.

Niwasihi Watanzania, tutumie hiyari yetu kufanya maamuzi yale tunaona ni sahihi. Hakuna haja ya kutukanana wala kulazimishana. Kama unadhani una sababu za msingi basi ziseme bila kuwaudhi wala kuwaona wapinzani wa muono wako ni wadudu. Sisi bado ni taifa moja hata katikati ya kutokubaliana kwetu.

Mungu wa mbinguni awabariki. Mungu aibariki na kuitunza Tanzania yetu!

Fact Sheet: https://www.fda.gov/media/146305/download
 
Gwajima akigombea urais anapita mapema kabisa, kura yangu tayari ameshaa ipata.

Wiki lijalo naenda kumuondoa mwanangu shule ili nimfundishie nyumbn wasije wakamdunga hayo matakataka yao.!
 
Ww nenda
Ww nenda kakojoe ulale, huu mziki ni mkubwa sana kwako! Upeo wako ni mdogo sana, huwezing'amua hata tukikesha tunakuelewesha! Hivyo kaa utulie na ujielewe tu akili zako ktk hili hazina akili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…