Zanzibar 2020 Hoja za Dkt. Hussein Mwinyi zinatosha kumpa nchi Oktoba 28

Zanzibar 2020 Hoja za Dkt. Hussein Mwinyi zinatosha kumpa nchi Oktoba 28

Nitajie shule gani kasoma Zanzibar madrasa gani kawahi kusoma na jee hapa Zanzibar kwao nikijiji gani utakapo nijibu hill kuna jengine nakuongezee tangu alipo kuwemo ndani ya bunge umemsikia lini akiitetea Zanzibar na jee ni waziri wa ulinzi na usalama umemsikia lini kuwatetea wale mashekhe wa uamsho huu ni mwaka 8 anawasulubu nijibu MASWALI yangu

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Hoja zake ndizo linapelekea watu kumuamini anastahili na anauwezo wa kuiongoza Zanzibar
1600932961882.png
 
Tatizo viongoz wa ccm Zanzibar baada tu ya kuchaguliwa hawana Tena mamlaka ya kufanya llte wanakuwa Kama wanaendeshwa kikubwa ni Kuna Mali na ardhi na kujimilikisha wenyewe huyo mwinyi nae Hana jipya anakuja kuongeza maeneo aliyaacha babakee wazidu kula Bata hi ndio Zanzibar bwana hapa kwangu ndio Sera ya vusiwa hivi mnyonge Hana thamani huo ndio ukwel Zanzibar kwa heri ile inaelekea kisarawe
 
wazanzibari wanataka raisi wao wanamtaka sio raisi wakuletewa kutoka Dodoma. Hata Mwinyi akisema atatuletea mwezi hapa chini, hilo haliwezekani kubadilisha mioyo yetu wazanzbari. Usishituliwe na kauli za majukwaani. Juzi Dr. Shein amelazimisha wafanya kazi wote wapeleke vitambulisho vyao vya ukaazi na vya kupiga kura. Asiefanya hivo atawachishwa kazi. Sasa kauli kama hii inatoa ishara gani?.
Ishara yai udikteta
 
Bado mtoto was balozi nae kugombania Zanzibar hahahahah
Zanzibar aslili yake no usultan Sasa ndio tunafata mfumo huo
 
HOJA ZA DK HUSSEIN MWINYI ZINATOSHA KUMPA NCHI OKTOBA, 28

Dkt. Hussein Mwinyi mgombea wa nafasi ya Urais Zanzibar anastahili kuchaguliwa kwa kura za ndio nyingi na kupewa nchi ili awaongoze Wazanzibar, nimefatilia mikutano yake ya kampeni na kubaini kuwa ni miongoni mwa wagombea bora wenye kujenga hoja zinazo mulika kutatua matatizo ya Wazanzibari, Mwinyi anaendesha siasa za hoja na ahadi mpya za kutatua kero wala si mashambulizi kwa wenzake, Pia hoja zake zinajikita kwenye ubunifu wa vyanzo vipya vya ajira kwa Wazanzibari.

Aidha Mwinyi anaguswa fika kizalendo na changamoto za Wazanzibari na ndio maana yupo tayari kuziishi na kuzitatua kwa vyovyote vile.

Mpaka sasa nimegundua Dkt. Mwinyi ana uwezo wa kipekee wa kujenga hoja za Kiuchumi dhidi ya watu na vitu aidha ni mwanaujamaa anayeamini katika falsafa ya kuwakomboa watu wa rika la chini ambao ndio wenye huitaji zaidi, Kwa kutumia jicho la tatu Zanzibar iliyostawi chini ya Mwinyi inarejea mikononi mwa Wazanzibari, Ni rai yangu kuomba Wazanzibar kuitumia fursa hii ya kumchagua kwa wingi Dkt. Mwinyi ili aweze kutimiza ndoto zao, ni nadra sana taifa kuwapata viongozi wenye kariba ya Mwinyi, hivo tuitumie vema fursa hii.

Ndoto za Dkt. Mwinyi kwa Wana-Zanzibar ni ndoto za kizalendo ambazo uwezi kuzisikia kwa kiongozi mwingine kati ya wanaogombea urais visiwani humo.

Yani upo kwenu Mkuranga unalima Mtama unawapangia Wazanzibari nani wa kumchagua?
 
wazanzibari ebu achene undina, mtachaguliwa raisi adi lini?
 
Naungana na mleta mada,

Jamaa anafanya siasa safi , za hoja yakinifu.

CCM kwa ujumla wake hawamshambulii mtu wanakwambia wamefanya nini na watafanya nini.

Mwinyi ni mtu sahihi kwa Zanzibar, wazanzibari msiipoteze nafasi hii adhimu ya kufikia aina ya maendeleo mnayoyataka.
Huyu ni tourist hawezi kupewa nchi kule znz.. Hana public visibility. ni mgeni kule.
 
Huyu ni tourist hawezi kupewa nchi kule znz.. Hana public visibility. ni mgeni kule.
wakati wamekwisha iba wagombea wa uwakilishi 11 bado munasema kuwa wako sawa. Kwanza warekebishe walio yafanya. demokrasia katiba na sheria za nchi zinavunjwa na CCM na bado baadhi yetu wanaongea kama vile hawaoni hatari ilioko mbele ya macho yetu.
 
Back
Top Bottom