MWESIGWA ZAIDI
Member
- Mar 7, 2015
- 21
- 1
HOJA ZA KUIKATAA KATIBA PENDEKEZWA HAZINA MASHIKO, MASLAHI YA WANANCHI YAMEZINGATIWA KWA KINA, SI KWELI KWAMBA INAWALINDA VIONGOZI PAMOJA NA CCM
MAKALA NO. 3
Kwa muda mrefu kumekuwepo hoja nyingi hasa kutoka vyama vya siasa, wanaharakati, wanasiasa, wanasheria pamoja na wachambuzi wa masuala ya kisiasa juu ya uhalali na ubora wa rasimu ya katiba inayopendekezwa na bunge maalum la katiba. Kwa ujumla wake hoja nyingi zinagawanyika katika makundi yafuatayo:-
Kwamba, bunge maalum lilikiuka mamlaka yake kisheria na kufanya kinyume cha matakwa ya sheria ya mabadiliko ya katiba (sura ya 83 toleo la mwaka 2014).
Kwamba, maoni ya wananchi katika rasimu ya pili ya katiba yaliachwa na hayakuzingatiwa( hapa hoja nyingi zinajikita katika suala la muundo wa muungano kutokana na takwimu za tume kuhusu maoni ya watu binafsi, vyama vya siasa, taasisi binafsi na za serikali kuhusu muundo wa muungano.
Kwamba, mchakato mzima wa kupatikana katiba pendekezwa ulikuwa na mapungufu mengi Kwamba, katiba inayopendekezwa imejali maslahi ya CCM pamoja na viongozi na siyo maslahi ya wananchi kama rasimu ya pili ilivyokwa imesheheni.
Maoni ya namna hii yamekuwa yakitolewa na watu wengi akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya katiba Mh. Jaji Joseph Sinde Warioba pamoja na baadhi ya waliokuwa wajumbe wa Tume hiyo na hivyo kuwashawishi watu wasiikubali rasimu ya katiba inayopendekezwa.
Hoja ya kwanza inakosa mashiko kabisa kisheria na kiuhalisia. Hoja hizi hazikuzingatia historia pamoja na dhana halisi ya kisheria kuhusu bunge maalum la katiba ( Consituent Assembly) ambayo ni kwamba bunge maalum ni mwakilishi wa mamlaka ( sovereignty) ya watu. Kujitungia katiba yao nikwa nikwa mujibu wa mamlaka ( sovereignty) ya watu. Ifahamike kwamba rasimu yenyewe ya katiba inaweza kuandikwa na kamati iliyoteuliwa na bunge lenyewe ( rejea mchakato wa kuandika katiba ya India ya 1950) au rasimu inaweza kuandaliwa na kuandikwa na Tume ( rejea mchakato wa kuandika katiba ya Uganda 1995). Mifumo yote hii haibadili wala kuondoa dhana au mamlaka ya bunge maalum kama chombo cha wananchi kama ilivo katika vifungu vya 25 (1) na 28(1) vya sheria ya mabadiliko ya katiba sura ya 83 toleo la mwaka 2014 ingawa kisiasa bunge maaalum lililochaguliwa na wananchi moja kwa moja linakuwa na nguvu zaidi kutokana na uwiano wa matabaka na makundi katika jamii.
Kisheria dhana ya bunge maalum haiathiriwi wala kubadilika kwa kuangalia nani niwajumbe wa bunge maalum ilimradi wawe wamepatikana kwa njia halali iliyoainishwa na sheria husika kama ilivyo kwetu hapa Tanzania ni sheria ya mabadiliko ya katiba sura ya 83 toleo la mwaka 2014 katika kifungu cha 22(1) (a)-(c) na (i)-(x). pia angalia David Mukholi (1995) Ugandas Fourth Constitution: History, Politics and Law, kampala: Fountaion Publishers, uk.49), Mahendra p. Singh, V.N. Shuklas Constitution of India 9[SUP]th[/SUP] Edn. Lucknow: Easten Book, uk.A-24-A-25.
Kwabahati mbaya sana pia wapo wanasheria wenye mlengo kama huu yakwamba bunge maalum halikuwa na mamlaka ya kurekebisha rasimu yapili ya katiba, bila yashaka nikwa sababu ya mapenzi ya vyama vyao pamoja na ushabiki wa kisiasa pasipokujali misingi ya taaluma yao ikiwemo kuwa waadilifu na kusema ukweli. Wamekuwa wakitoa tafsiri potofu juu ya mamlaka ya bunge maalum la katiba kwamba halikuwa na mamlaka yakile bunge maalum lilichofanya kurekebisha na kuboresha misingi ya rasimu ya pili iliyopendekezwa. Natumia furusa hii kuwaelimisha kwamba kifungu cha 25(1) kinasomwa pamoja na kifungu cha 28(1) ndipo mantiki sahihi ya mamlaka ya bunge maalum la katiba yanapatikana.
Kwa kwamujibu wa kifungu cha 28(1) bunge maalum lilikuwa na kazi ya kutunga katiba inayopendekezwa wala siyo kupitisha rasimu ya Tume kama inavyoelezwa na baadhi ya watu. Bila shaka bunge maalum lilikuwa namamlaka ya kutunga rasimu ya katiba inayopendekezwa bila kufungwa na rasimu yapili ya Tume.
Baadhi ya tafsiri potofu zinazotolewa zinaonesha kama vile Tume ndiyo ilikuwa na mamlaka ya kutunga katiba inayopendekezwa ambapo siyo kweli. Tume haikuwa na wawakilishi wa wananchi, ilikuwa na watu wenye weledi wa kukusanya maslahi tofauti ya wananchi ili yawasilishwe kwenye bunge maalum. Bunge maalum ndicho chombo kilichokuwa kimesheheni wawakilishi wa wananchi na ndiyo maana bunge maalum likapewa mamlaka ya kutunga katiba inayowafaa wananchi nasiyo kubariki yaliyoletwa na Tume.
Kuhusu hoja yakwamba maoni ya wananchi yameachwa siyo ya kweli kabisa ni uzushi tu wakisiasa kwa kuzingatia maelezo pamoja na tafsiri niliyotoa hapo juu kuhusu mamlaka pamoja na ukomo wa mamlaka ya bunge maalum la katiba. Hoja yakwamba wananchi waliowengi walipendekeza muundo wa serikali tatu siyo sahihi na haithibitiki kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa na Tume yenyewe kwa ushahidi ufuatao: ukiangalia kwa makini takwimu zilizotolewa na Tume yenyewe ( angalia jedwali 3,uk.9) kwamba, waliotoa maoni mbele ya tume ni watu 351,664 kati ya hao, 47,820 tu (asilimia 14) ndio waligusia muundo wa muungano. Asilimia 86 hawakuzungumzia muundo wa muungano kwa maana yoyote iwe ya serikali moja, mbili, tatu au muungano wa mkataba. Wao walikuwa na mambo tofauti kabisa kuhusu maisha yao. Isitoshe, kati ya waiogusia muundo wa muungano, asilimia 30 walitaka serikali mbili, asilimia 37 walipendekeza serikali tatu, na asilimia 25 walitaka muungano wa mkataba, asilimia nane walitaka serikali moja.
Kwahiyo waliopendekeza serikali tatu ni theluthi moja tu ya waliogusia muundo wa muungano na ni asilimia 5 tu walitoa maoni, waliotaka serikali mbili na muungano wa mkataba ni asilimia 55, yaani zaidi ya nusu ya waliotoa maoni juu ya muundo wa muungano. Hata ukichanganya waliotaka serikali moja na serikali mbili ni asilimia 38, inazidi kidogo wale waliotaka serikali tatu. Kwa takwimu hizi za Tume usahihi wa kwamba wananchi waliowengi walitaka muundo wa serikali tatu uko wapi? Hoja hii haina mashiko wala ushahidi wa maana, na kuendelea kwa waliokuwa watumishi wa Tume kwamba serikali tatu ndizo zilitakiwa na wananchi wengi itakuwa nikutwambia kwamba wao wenyewe ndiyo wanataka muundo wa serikali tatu ila wasitumie mgongo wa Tume maana kwenye takwimu za Tume mahitaji ya serikali tatu kwa wananchi waliowengi hayathibitiki kabisa.
Pia nivema ifahamike kwamba haikuwa makusudio ya sheria ya mabadiliko ya katiba wala siyo dhana ya bunge maalum la katiba kwamba kila hoja iliyowasilishwa na Tume ilikuwa lazima kupitishwa na bunge maalum na kama bunge lingefanya hivyo lingekuwa limepoteza maudhui yake na ikumbukwe kwamba Tume iliyasahau mengi muhimu ya wananchi na ndiyo umaalum wa bunge la katiba unapatikana kwa kurekebisha, kuboresha, kupitisha na kutunga katiba inayowafaa wananchi kulingana na mahitaji pamoja na mazingira ya nchi.
Nafasi ya bunge maalum niyakipekee kabisa katika mchakato wa kutunga katiba mpya. Nafasi yake ni nzito kuliko ile ya Tume na muhimu kuliko kura ya maoni nikwa sababu bunge maalum ndiyo chombo cha kufanya maamuzi mazito, siyo Tume.Ningelishangaa sana kama bunge maalum lingebariki baadhi ya misingi iliyokuwa imewekwa na Tume kwenye rasimu ambayo ingepitishwa na bunge maalum na kisha kupitishwa na wananchi ingeleta balaa na maangamizi kwa Watanzania hasa ule muundo wa serikali tatu. Bunge lilikuwa na kazi ya kuhakikisha kwamba inapitisha mambo ambayo hayawezi kuzaa vurugu, kuvunja utulivu, amani pamoja na mshikamano na umoja wananchi,( National and territorial integrity).
Kuhusu hoja ya kwamba mchakato wa kupatikana katiba pendekezwa hauna uhalali na kwamba katiba pendekezwa siyo halai, naomba kuwauliza wanaotoa kauli hii kwamba nikipi si halali kati ya haya yaliyopelekea kupatikana kwa katiba pendekezwa, Ni sheria ya mabadiliko ya katiba? Ni wajumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba? Ni Tume yenyewe? Ni rasimu ya Tume? Ni bunge maalum? Ni kanuni za bunge maalum? Au ni rasimu ya katiba pendekezwa. Iwapo maswali haya yatajibiwa kwa kuzingatia hoja na uchambuzi niliofanya pamoja na uhalisia wa matakwa ya kisheria na siyo ya maslahi ya vyama vya siasa au kundi Fulani la watu itakuwa wazi kwamba rasimu ya katiba inayopendekezwa unao uhalali wote wa kupigiwa kura na wananchi kwa kadri watakavoona wao.
Hoja nyingine inayotolewa sana ambayo kwa upande wangu ninasema nidhaifu na haina mashiko ni ile yakwamba katiba pendekezwa imejali zaidi maslahi ya CCM pamoja na viongozi na siyo maslahi ya wananchi. Wanaosema hivi hawajaisoma na kuilewa katiba inayopendekezwa na badala yake wanaongozwa ima na hisia tu au ni wale vinganganizi wa rasimu ya pili au niwale wenye tamaa ya kuiona Tanzania inavurugika ili watimize ndoto zao za kuwa viongozi wakati watanzania wakipata shida. Katika sura ya pili sehemu kwanza ya katiba inayopendekezwa Ibara ya 11(1) inabainisha wazi kwamba lengo la katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha, haki, usawa, udugu, amani, umoja na utangamano wa wananchi wa jamhuri ya muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenye democrasia, utawala bora, maendeleo endelevu na kujitegemea na ibara ndogo ya 3 imetaja malengo makuu ya katiba hii kitaifa ambayo yamezingatia mahitaji muhimu ya watanzania wote. Imetajwa kwamba lengo kuu la katiba hii kitaifa ni kuboresha maisha ya watanzania katika Nyanja zote za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kimazingira. Seheme ya pili, Ibara ya 12(1) imetaja wazi kwamba katiba hii inalengo la kisiasa na nilengo la kitaifa na kwamba serikali itahakikisha inadumisha democrasia, na kuondoa ubaguzi wa aina zote pia katika ibara ndogo ya 2(a), (b) na (c) katiba pendekezwa imeweka wazi kwamba litakuwa nijukumu la serikali kuchukua hatua ambazo zimeainishwa ndani ya ibara hii kuhakikisha lengo la katiba hii kisiasa linafanikiwa kwa watanzania pia bunge limetakiwa kutunga sheria zitakazowezesha lengo hili muhimu linafikiwa.
Katika sehemu ya tatu ya katiba pendekezwa inataja malengo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kuwa malengo ya kitaifa ambapo katika ibara ya 13(1) lengo la Taifa kiuchumi imetajwa kuwa serikali itahakikisha Taifa linajenga uchumi wa kisasa utakaowawezesha wananchi na Taifa kujitegemea kwa kuzingatia matumizi ya elimu ya sayansi na technolojia katika Nyanja zote za uzalishaji mali kwa kuhimiza mapinduzi ya kilimo, ufugaji na uvuvi, mapinduzi ya viwanda na kujenga sekta muhimu ya nishati na mwasiliano na miundo mbinu ambapo katika ibara ndogo ya 2(a)-(g) katiba inatoa jukumu kwa serikali kuhakikisha inachukua hatua stahiki ambazo pia pia zimetajwa kuhakikisha lengo la Taifa kiuchumi linakamilika pia bunge limetakiwa kutunga sheria zitakazowezesha lengo hili muhimu linafikiwa.
Ibara ya 14(1) imeweka lengo la Taifa kijamii kwamba serikali itahakikisha inajenga jamii yenye ustawi na uwezo wa kushiriki katika shughuli za kimaendeleo katika Nyanja mbalimbali ambapo ibara ndogo ya 2(a)-(f) Serikali ina jukumu la kuchukua hatua stahiki ili kufikia lengo hili na pia bunge litatunga sheria kuhakikisha lengo hili muhimu linafikiwa.
Ibara ya 15(1) imetaja lengo la Taifa kiutamaduni kwamba nikukuza, kudumisha, na kuhifadhi utamaduni wa Taifa pia wa wananchi ambapo katika ibara ndogo ya 2(a)-(e) serikali imetakiwa kuchukua hatua stahiki ili kuhakikisha lengo hili muhimu la kitaifa linafikiwa.
Hivi kweli malengo makuu na muhimu ya katiba hii kitaifa yaliyotajwa katika ibara za 11,12,13,14 na 15 nikwa ajili ya CCM na viongozi? Au jamii inamahitaji mengine nje ya haya yaliyotajwa katika katiba hii pendekezwa? Kuna kosa gani iwapo hawa wanaosema katiba hii pendekezwa ni mbaya, haikujali maslahi ya wananchi na inalinda CCM na viongozi wa nchi nikiwaita wazushi? Katiba pendekezwa ni nzuri sana. MWANASHERIA.
MWESIGWA ZAIDI SIRAJI.
0784 646220