Mkuu Palamagamba sijaanza kumsikia leo, na no doubt kuwa ni kichwa. Unajua uzuri wa siasa unaweza kuamua kabisa kubadilisha baya na kupiduapindua maneno na kuliona zuri. Unajua kwa sasa ndani ya CCM kuna watu wengi wanaolia kuhusu kuoza kwa chama, mbali na hao hata wasiojua aaa na bee wanaona kabisa kuwa CCM ya sasa sio ile ya J Nyerere. Sasa ukiona mtu anasimama mbele ya watu wazima na kuanza kutoa hoja za kukisifu chama ambacho hata waliokianzisha wenyewe wanalalamika, au hata kuunga mkono upindishaji wa wazi wa sheria kwa manufaa ya kikundi tu cha watu, then ujue huyu mtu ana tatizo.
Unajua kuna wakati inabidi tuwe tunasema ukweli, it is sometimes very hard to prove the obvious. Hoja ya mgombea binafsi hakuna asiyejua kuwa ni haki ya kikatiba, si mara moja na si mara mbili majaji wamepitia katiba na kuitafsiri kwa lugha nyepesi kabisa kuwa mgobea huru ni halali. Kuna wakati hata Nyerere alikuwa ansema wazi kabisa kuwa mgombea huru ni halali na alikuwa anatoa mfano wa mbunge sarawat, na ni katiba hiyo hiyo tunayoizungumzia iliyomruhusu Sarawat kugombea ubunge na kushinda, ni hiyo hio leo wanasema inazuia. Mkuu hakuna asiyejua kwa sasa kuwa uhai wa CCM upo kwenye kuwanyima watu haki hiyo. Tunaelewa wazi kuwa kuna wabunge wengi wana uwezo wa kuchukua majimbo bila mgongo wa CCM, ikitokea hiyo tu ndio mwisho wa CCM.
Sasa ukiona profesa, tena profesa mwenye akili, anaamua kutetea kitu cha kijinga kabisa, inabidi mtu uwe na mashaka. Kuwa ofisa usalama wa taifa haina maana kuwa usitumie akili zako. haina maana ukisifu chama cha mapinduzi na serikali hata kinapofanya mabaya, haina maana kusifia hata pale sheria zinapokiukwa. kama utakumbuka vizuri waliofichua mauchafu yote ya EPA, Richmond na wizi mwingine ni hao watu wa uslama wa taifa, sasa kwanini yeye awe hopeless agent wa usalama wa taifa? hopeless kuliko hata wasio maprofesa.
Kwa wanasheria ni kawadia kuwatetea wahalifu. Hata kama unajua wazi kuwa huyu jamaa ni mwizi au ni muuaji, unajaribu kujipatia pesa za kumsaidia mhalifu kutafuta loop holes za sheria ili aachiwe huru. Au na yeye anajaribu kuapply hiyo notion kwenye siasa za taifa?
Mkuu this is my opinion, inawezekana kabisa siko sahihi lakini ndio ninavyoona.