Masikini_Jeuri
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 6,829
- 1,303
Mheshimiwa, hivi tukikutaka wewe ujenge hoja tofauti za Prof. Palamagamba kuhusu mgombea binafsi unaweza kutuambiaje kiufasaha hasa? Kama msomi amabye upo tayari kutetea kile anachokiamnini kwa kutumia hoja yakinifu na zenye mantiki. Kwanza tupe concept wewe unavyoelewa, kisheria maana ya mgombea binafsi then Tafadhali weka jamvini mengine....
hana lolote huyo anadanganya tu kwa kujifanya anatetea wa tz kwenye eac,kwani ni kati ya vigogo wa gazeti la mwananchi ambalo linaendeshwa na wakenya ingawa ni la agakhani na anapata hurua kutokana na muingiliano wa eac,kama ana uchungu asingekubali kutumia nguvu zake kuendeleza kampuni ya wakenyawiki kama mbili zilizopita nilikuwa naangalia kipindi cha simbeye pale tbc1, mmojawapo wa wazungumzaji alikuwa ni huyu profesa. Kwa kweli nirifarijika sana jinsi huyu bwana alivokuwa akitetea maslahi ya watanzania (nchi) katika mchakato wa eac na jinsi anavyoona mambo yanavyoharakishwa bila kutoa nafasi ya kudurusu kila hatua tunayomaliza. Hapa nampa heko profesa ingawa tulitofautiana katika suala la mgombea binafsi(labda pia ni kutokana na ufahamu wangu mdogo kuhusu sheria)
huyu profesa ameonyesha kuwa yeye ni msomi yupo tayari kutetea kile anachokiamnini kwa kutumia hoja yakinifu na zenye mantiki. Nilifurahi zaidi kwa vile yeye ni mojawapo wa wawakilishi wa tz katika majadiliano ya eac.
Katika kipindi hicho pia alikuwepo dr kamala, duu jamaa alishindwa kabisa kujenga hoja, kama huyu ndiye anakaa na akina wetangula katika majadiliano basi tz tujue hatuna mtu. Hoja zake siku zote ni dhaifu, hana sauti ya mamlaka, kiingereza chake ni finyu n.k. Hata ukilinganisha hoja zake na za profesa kabudi ungedhani ni mtu wa mwenye shahada ya kwanza anajadiliana na profesa wake....
Kama nchi lazima tuwe tunateua mawaziri ambao wanaweza kujenga hoja za kueleweka, na pia ambao wanaweza kuwasiliana kwa lugha ya kiingereza kwa ufasaha zaidi. Yawezekana kamala ana strenghths zake nyingi tu lakini katika hili la eac anapwaya sana ni kama yeye ni mtu wa kuburuzwa na wakenya na waganda na yeye anafurahia sana hii intergration-sijui kwa maslahi gani. Angejua watz wengi tuko skeptical na hii move asingekuwa anajenga hizo hoja anazojenga sasa kuwa eac ina faida nyingi sana.
Mkuu Palamagamba sijaanza kumsikia leo, na no doubt kuwa ni kichwa. Unajua uzuri wa siasa unaweza kuamua kabisa kubadilisha baya na kupiduapindua maneno na kuliona zuri. Unajua kwa sasa ndani ya CCM kuna watu wengi wanaolia kuhusu kuoza kwa chama, mbali na hao hata wasiojua aaa na bee wanaona kabisa kuwa CCM ya sasa sio ile ya J Nyerere. Sasa ukiona mtu anasimama mbele ya watu wazima na kuanza kutoa hoja za kukisifu chama ambacho hata waliokianzisha wenyewe wanalalamika, au hata kuunga mkono upindishaji wa wazi wa sheria kwa manufaa ya kikundi tu cha watu, then ujue huyu mtu ana tatizo.
Unajua kuna wakati inabidi tuwe tunasema ukweli, it is sometimes very hard to prove the obvious. Hoja ya mgombea binafsi hakuna asiyejua kuwa ni haki ya kikatiba, si mara moja na si mara mbili majaji wamepitia katiba na kuitafsiri kwa lugha nyepesi kabisa kuwa mgobea huru ni halali. Kuna wakati hata Nyerere alikuwa ansema wazi kabisa kuwa mgombea huru ni halali na alikuwa anatoa mfano wa mbunge sarawat, na ni katiba hiyo hiyo tunayoizungumzia iliyomruhusu Sarawat kugombea ubunge na kushinda, ni hiyo hio leo wanasema inazuia. Mkuu hakuna asiyejua kwa sasa kuwa uhai wa CCM upo kwenye kuwanyima watu haki hiyo. Tunaelewa wazi kuwa kuna wabunge wengi wana uwezo wa kuchukua majimbo bila mgongo wa CCM, ikitokea hiyo tu ndio mwisho wa CCM.
Sasa ukiona profesa, tena profesa mwenye akili, anaamua kutetea kitu cha kijinga kabisa, inabidi mtu uwe na mashaka. Kuwa ofisa usalama wa taifa haina maana kuwa usitumie akili zako. haina maana ukisifu chama cha mapinduzi na serikali hata kinapofanya mabaya, haina maana kusifia hata pale sheria zinapokiukwa. kama utakumbuka vizuri waliofichua mauchafu yote ya EPA, Richmond na wizi mwingine ni hao watu wa uslama wa taifa, sasa kwanini yeye awe hopeless agent wa usalama wa taifa? hopeless kuliko hata wasio maprofesa.
Kwa wanasheria ni kawadia kuwatetea wahalifu. Hata kama unajua wazi kuwa huyu jamaa ni mwizi au ni muuaji, unajaribu kujipatia pesa za kumsaidia mhalifu kutafuta loop holes za sheria ili aachiwe huru. Au na yeye anajaribu kuapply hiyo notion kwenye siasa za taifa?
Mkuu this is my opinion, inawezekana kabisa siko sahihi lakini ndio ninavyoona.
"...Baada ya kumaliza High School pale Milambo Secondary School na HGL mwishoni mwa miaka ya sabini (nadhani 1978 au 79), Paramagamba aliajiliwa kama mwandishi wa habari nadhani wa Daily News kwa miaka kama miwili au mitatu hivi kabla hajaenda kusomea LLB hapo UDSM ambapo alipata division ya juu yenye GPA zaidi ya 3.8 out of 5 akaajiriwa kama TA katika kitivo cha sheria (wakati huo), kazi ambayo ameifanya kuanzia katikati na mwishoni mwa miaka ya themanini hadi leo. Kwa hiyo ni vigumu sana kuniamanisha kuwa anatumikia usalama wa taifa hasa ukizingatia kuwa kipindi alichomaliza chuo kikuu kulikuwa na mabadiliko ya uongozi kati ya Nyerere na Mwinyi ambapo usalama wa taifa walioajiriwa na Opiyo waliondolowa wote na kujazwa wengine wapya chini ya Lupia..."
Kichunguu- huyu alimaliza Milambo 1976. Alikuwa mshiriki mzuri wa kile kilichokuwa kinaitwa Senior A Discussion Group ambayo ilijumuisha shule zote za A Level pale Tabora ikiwa ni pamoja na Kipalapala Seminari. Alikuwa msemaji mwenye maneno makali lakini aliyasema kwa upole usio na kifani...namkumbuka sana alivyosambaratisha midahalo ya kiingereza kwa hoja nzito isiyo na jazba--alitumia maneno kama vile wenye kungangania kiingereza ni vibwenyenye, ni wadhanifu wasio na lahaja ya uyakinifu...doh na mengi mengine. Nadhan ule ndio ulikuwa mwanzo wa kifo cha kile kikundi, tulikuwa tukikutana pale Student Centre! HUYU NDIYE MSOMI TANGU ENZI HIZO, LAKINI ANATUMIA USOMI WAKE KUUA MATUMANIO YA JAMII...kwa hali ya kawaida- wahitimu wa Tabora A levels walikuwa na fursa kubwa ya debates ambazo ziliongeza uwezo wao wa lugha ya kiingereza. Na kuhusu Mgombea binafsi - nadhani Mtikila atakuwa na mengi sana ya kumsemea...
Ndiyo ni Msomi kweli kweli lakini unapotumia nguvu za hoja kuangamiza hata zile za wenzio kwa sababu tu ya maslahi mengine....! ah sijui bwana! Nadhani msomi ni yule anayesaidia jamii kwa kutumia utashi aliopewa na Mungu. Wapo watu wenye GPA 4 na Clean Masters na PhD lakini wenda wazimu barabarani...hawasaidii jamii
Aingie rasmi kwenye siasa sasa mchango wake unahitajika pande hii muda huuuu
Udaktari wa kama Kamala na wenzake unapatikana kwa USD 180 tu hapa www.instantdegrees.com