Uchaguzi 2020 Hoja za Tundu Lissu Bagamoyo ni mwiba mchungu kwa CCM. CCM inapomjibu Lissu anawasha moto zaidi

Uchaguzi 2020 Hoja za Tundu Lissu Bagamoyo ni mwiba mchungu kwa CCM. CCM inapomjibu Lissu anawasha moto zaidi

Mkutano wa Tundu Lissu akiwa Bagamoyo umenikatisha tamaa kwa hoja zake zisizo na majibu bali zinahitaji utekelezaji wa Serikali.

Mosi, Tundu Lissu anasema wananchi wa barabara ya Kimara wengi wamekufa kwa presha baada ya nyumba zao kubomolewa na viongozi wa CCM kupitia mamlaka kuu,Anasisitiza hawakulipwa pesa kosa barabara.

Pili, Tundu Lissu anasisitiza walimu na mapolisi kwa miaka mitano hawajaongezewa kitu chochote ,na wakati wa Mei Mosi hujibiwa kwa kiburi tunajenga barabara.

Tatu, Tundu Lissu amewauliza wananchi hali ya maisha yao na wafanyabiashara wanaonaje,Wananchi wamejibu hali ni ngumu sana

Nne, Anatuhumu kuwa pesa na michango ya Corona imeliwa yote waliyochangisha wana CCM na Mamlaka Kuu. Anasema madaktari na manesi waliahidiwa wakati wa corona kulipwa lakini mpaka sasa hawajalipwa hata senti tano.

Hii ya Bagamoyo leo Tundu Lissu lengo lake ni kumjibu Mama Samia Suluhu kwa hotuba zake Lindi.

Kwa hoja na kauli ngumu kama hizi za Tundu Lissu nani atazijibu?

Mzee Yusuf Makamba amejitokeza leo kujibu lakini utamuonea huruma hana la kujibu wala namna bali kutifurahisha vijana.

Mzee Makamba anasema CCM ndio imejenga uwanja wa Rais Chato na sio Rais kajenga, amesisitiza kuwa Chato ni Tanzania

Mzee Makamba anasema mbuga ya Chato ni ongezeko la vivutio kwani lile pori lilikuwa tupu wanakaa majambazi.

CCM kama chama changu tuache kumjibu huyu mtu majukwaani tuongelee yetu.

Mbona suala la hotuba yake Zanzibar tumekaa kimya na yeye mwenyewe kapotezea, tungejibu ishu ya Zanzibar angetupa taabu sana.
TL mpk leo anajua labda yupo Bungeni, sahizi ni muda wa kumwaga sera na kutuambia tukimpa Nchi atatufanyia nini lkn yy mpk sasa anatuhumu tuhumu kwamba Magufuli hajafanya hiki, mara Risasi nk....aisee bado tuna safari ndefu sana.
 
TL mpk leo anajua labda yupo Bungeni, sahizi ni muda wa kumwaga sera na kutuambia tukimpa Nchi atatufanyia nini lkn yy mpk sasa anatuhumu tuhumu kwamba Magufuli hajafanya hiki, mara Risasi nk....aisee bado tuna safari ndefu sana.
Wewe ndio unasafari ndefu kuufikirisha ubongo wako!
 
TL mpk leo anajua labda yupo Bungeni, sahizi ni muda wa kumwaga sera na kutuambia tukimpa Nchi atatufanyia nini lkn yy mpk sasa anatuhumu tuhumu kwamba Magufuli hajafanya hiki, mara Risasi nk....aisee bado tuna safari ndefu sana.

Wewe ni popoma. Hata shule ulisoma hivi hivi? Au unajitoa ufahamu tu kwa Lissu? Mara ngapi anasema Chadema itafanya hivi na vile?
 
Sidhani kama hoja hizi kuna wa kuzijibu labda ccm watekeleze haya kama njia ya kujibu ILA sio vinginevyo!
 
Uwafikie lakini majibu kwa wenye akili yanatakiwa, kwa nini uwanja wa ndege ujengwe kijijini Chato na pesa yake kutopitishwa na bunge?
Hyo ni minor case Sana kumuondoa gifted leader kama JPM
 
View attachment 1565570
Sawa Bwashehe.....CCM can not waste her time to answer somebody shit, kazi yao ni moja tuu, kuwafikia wapiga kura walipo na kuwatatulia shida zao ..... Hakuna impact yyte ya sera Kwa mda uliobaki... Ni kushikilia ulicho nacho
Kitu ambacho hamkijui CCM..kuna watu ambao huwezi kukuta wana ongelea siasa wala kwenda kwenye mikutano..hao ndio wanaenda kumuangusha Magu...
 
Mkuu, subiri kwenye sanduku ndo utajuwa ulikuwa ni mwiba au kijiti cha nyasi. Na kwa kupitia ndo utaona kama CHADEMA ulikuwa na mgombea wenye faida au kakiingiza chama mkenge? Stay tuned uchaguzi uishe na Magu aapishwe ndo utaikumbuka comment hii.
Kuapishwa au kushinda CCM haina mjadala, ni muda unasubiriwa. Japo ukweli ni aina ipi ya ushindi ndio jambo mara zote linaumiza vichwa vya wapenzi wa chaguzi zilizo huru na haki.
 
Zahanati za kwenye makaratasi hizi. Takwimu za kupika hizi. Our president is a big liar, egoistic and impulsive.
Kweli kuna uongo na kudanganywa! Shule moja Kanda ya ziwa alisema ilikarabatiwa kwa bilioni 700!
 
Magu hajawahi kutaja jina la Lissu hata kwa bahati mbaya ni dalili ya uwoga...hata nchi zilizoendelea wanatajana majina kwenye kampeni..
 
Watumishi wa Umma jamani nawahurumia sana, ikitokea amerudi madarakani huyu jamaa Jiwe, mtamjua yeye ni nani ! si unaona hawaongelei! kwenye kampeni zake! ana lake moyoni! hasa mnaoishi mijini km DSM. anachukia sana!

Atawafuta kazi wote, halafu anawapiga kalenda, mara mjiorodheshe! atawalipa, lipa lipa na wewe! akawii kuwatambia yeye ndiyo mwajiri mkuu!
fanyeni hivi; kwa umoja wenu tu mfuteni kazi yeye kwanza kabla hajawafuta nyie! hana faida nanyi, pateni vitu vipya Lissu hana shukrani yule! nilimpaga zamani lkn sasa sitaki apewe! Gwiji mwizi mkuu wa kura Nape yuko wapi? kimya!! sijui kafia wapi Maskini nape!
 
Hii picha inatrend lakini ni fully photo shop yaan aliyekata Kata na kuunga Hana weledi na kucheza na picha.
Wanaita Aireal pictures,picha moja upande wame zoom kwingine wame minimize original size.Aibu ya uchache wa watu inawatesa mno,hapo kuna wanafunzi,waalimu primary&secondary,watendaji wote wa vijiji na kata pamoja na wafanyakazi wa umma+askari both in combats&pain clothes,usalama na wasiojulikana(Jeshi la Akiba).Unafikiria huo umati wote unapigia kura kweye eneo hilo?
Mzee amekariri vijiji vilivyopata umeme wa REA.ujenzi wa barabara,madaraja,Bwawa la Kufua Umeme,sgr,ujenzi wa Ikulu Chamwino,bila ya kusahau uwanja kimataifa wa ndege Chattle nk.huku watumishi wa umma hawalipwi stahiki zao na hakuna ajira.
Watanzania tuamke,bila kufanya mabadiliko ya utawala huu tutapata shida sana.CCM wanaliharibu Taifa letu ili waendelee kututawala.
 
Zahanati takriban 300 zimejengwa nchi nzima with in 5 yrs , rekodi ya kipekee Sana , wakat kikwete alijenga zahanati 150 Kwa mda wa miaka kumi, zahanati hzo zinasubir watumishi wa afya waajiliwe mwaka ujao wa fedha
Zahanati zisizokuwa na watumishi wa afya?tunasubiri mwaka ujao tuajiri!!!!hivi mnakulaga nini hapo Lumumba?kiasi kwamba akili yote inapotea..?endelea kudanganya akina MUSIBA
 
Back
Top Bottom