Hoja za Utanganyika na Uzanzibari ni Hoja Muflis za Ujinga wa Ukosefu Elimu ya Uraia. Tuwatoe Ujinga Huu Kwa Elimu ya Uraia au Tuwaache na Ujinga Wao?

Mkuu P, with all due respect hii 'fallacious article' inakufanya uonekana ' a mendacious person'
Lakini pia ni 'intellectual abuse' kubwa sana kwa jamii ya Watanzania.
Wanabodi
Swali ni jee tuwatoe ujinga hawa vitimbakwiri muflis wanaotaka kutubagua kwa Utanganyika na Uzanzibari kwa kuwaelimisha elimu ya uraia, au tuwaache tuu na ujinga wao kujisikia sifa kujinasibisha na kujivunia Utanganyika na Uzanzibari?.
Je hawa ''stalwart ' wachache ni Vitimbakwiri?
CJ Nyalali na jopo
Dr Salim Ahmed Salim
PM and VP Warioba
Mr J.Butiku
Judge Kisanga

Hivi unataka ulimwengu uamini kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu (AG) , Waziri wa Katiba na Sheria , Waziri Mkuu mstaafu(PM) na Rais wa Bahari za dunia , Mh J.S. Warioba naye anahitaji elimu yako ya Uraia kupitia vipindi vyako ! real?
Kabla ya Muungano, tulikuwa na nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar, hivyo tulikuwa na uraia wa Tanganyika, na uraia wa Zanzibar.
Usisahau maneno hayo
Sheria gani na ya mwaka gani iliyofuta majina hayo. Jina la Tanganyika lilifutwa na sheria gani
OK
Tanganyika haipo nafasi yake imechukuliwa na Tanzania Bara, na Zanzibar japo ipo, ila sio nchi ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye utawala wake wa ndani, lakini hakuna uraia wa Zanzibar, uraia ni mmoja tuu wa Tanzania.
Tanzania Bara ni nchi gani? Rejea maneno yako hapo juu '' nchi zilizoungana ni Tanganyika na Zanzibar''
Hii Tanzania bara umeipata wapi?
2. Muungano wa Federation, ni nchi mbili au zaidi, zinaungano kuwa nchi moja, lakini zile nchi zote mbili zinaendelea kuwa utawala wake wa ndani, na serikali zao, chini ya utawala mkuu wan chi ya federal state, kama Marekani.
Sawa
Pascal unahitaji Elimu ya Uraia ni si kutoa Elimu ya Uraia.
Umesema '' Federation yenye nchi mbili , Tanzania na Zanzibar''
Ukasema zilizoungana ni Tanganyika na Zanzibar. Halafu ukasema nchi hizo zimeunda Tanzania.
Hapa chini unasema zilizoungana ni Tanzania na Zanzibar.

Tanzania is an 'entity' ! ni zao la Tanganyika na Zanzibar na kamwe haiwezi kuungana na mshirika wa nchi hizo mbili wala haiwezi kuwa na ushirika na nchi hizo mbili kwasababu Tanganyika na Zanzibar ni subset za Tanzania. period! haihitaji elimu yoyote ile

Acha upotoshaji na uongo ! please you're better than this ! Unaweza kutafuta vipindi si kwa njia hii.

Nimesoma article na sitairudia na wala sitasikiliza vipindi vyako tena si kwa maana mbaya, ni katika kulinda 'intellectual capacity yangu' . Yaani umefika mahali unatukana weledi na akili za watu bila aibu
Kila la heri na vipindi unavyotafuta 'in a deceitful behavior'' .
Ume ni disappoint sana na sijui editor aliwezaje kuruhusu hiyo article bila ku cheki consistency na facts






 
Mkuu pascal kwa nini mtu akihoji muungano kwa kuwaita wazanzbari "wazanzbari" anaonekana mbaguzi ilihali hata "wazanzbari" hujiita na kujiona "wazanzbari" Kwanza kabla ya kujiona watanzania

Matter of fact, Zanzbar ipo kwa hiyo kuna ubaya gani watanganyika wakiidai Tanganyika na utanganyika wao kama ambavyo wazanzbari hawapo tayari kuupoteza uzanzbari wao?..

Nina maswali mengi lakini sijui kama yatajibika, ila ukinijibu hata hayo nitashukuru
 
ni muhimu zaidi kuwatoa ujinga vitimbakwiri hawa. Kuacha kufanya hivyo ni kuwatelekeza, jambo ambalo si zuri, watazaliana na ujinga wa kibaguzi kudai kitu kisichokuepo utaongezeka zaidi 🐒
 
kuzira, kususa, kugoma tena kwa mihemko na ghadhabu kwa hoja na majadiliano ya kawaida na ya kiungwana namna hii si ndio utimbakwiri wenyewe huu. Sasa unapanic nini na wakati naona una mawazo na hoja nzuri tu?

si utulie upate elimu ya uraia, fatilia vipindi na makala mbalimbali ili kuongeza uelewa na ufahamu zaidi juu ya masuala haya ya Muungano. kughafilika au kupotoka ni mambo ya kawaida tu 🐒
 
Naomba kuheshimu mawazo yako na maoni yako.
Nakushukuru.
P
 
kuzira, kususa, kugoma tena kwa mihemko na ghadhabu kwa hoja na majadiliano ya kawaida na ya kiungwana namna hii si ndio utimbakwiri wenyewe huu. Sasa unapanic nini na wakati naona una mawazo na hoja nzuri tu?
Vitimbakwiri vikibananishwa, vinakuwa vikali kweli kweli!.
P
 
ni muhimu zaidi kuwatoa ujinga vitimbakwiri hawa. Kuacha kufanya hivyo ni kuwatelekeza, jambo ambalo si zuri, watazaliana na ujinga wa kibaguzi kudai kitu kisichokuepo utaongezeka zaidi 🐒
Naunga mkono hoja, kazi ya kuwatoa ujinga vitimbakwiri hawa inaendelea kwa kipindi cha TV kila Jumatano na Jumapili na makala za magazeti ya Mwananchi Jumatano na Nipashe Jumapili.
P
 
Alijisemeaga Magufuli...Mayalla maana yake ni njaa. Mzee sasa ameamua ku kiss a** ili alambe asali kidogo. Kuna baadhi ya wasomi wa Tanzania wanatuangusha sana.
 
Mi naona unaenda mbele na kurudi nyuma. Juzi hapa uliandika vizuri sana, ulipoleta hoja ya kuwa na serikali moja, badala ya hizi mbili zilizopo au Tatu zinazopigiwa kelele na wengi.

Sasa Leo tena unaanza kusema hatuna elimu ya uraia.

Binafsi nadhani nchi hizi hazijaungana ila tuna mikataba ya kushirikiana, na ndipo tukawa na mambo 22 ya muungano.

Kuungana tungeungana kila kitu to disolve tuwe solution moja isiyogawanyika (homogeneous solution), ila siyo kama sasa mara utasikia mafuta siyo ya muungano, mipaka siyo ya muungano, mara utawala siyo swala la muungano, huo sio muungano.

Kila kukicha anaibuka mtu anakuja na lake, tuondoe bara na visiwani, tuwe na rais mmoja na kusiwe na mipaka ndani ya muungano, kama ilivyo sasa Mtanganyika hawezi kumiliki ardhi zanzibar, Kitambulisho cha taifa cha bara na zanzibar tofauti, ili mradi kuchanganyana tu.

Sasa hiyo elimu hata ukiitoa ikiwa mkataba au muungano una mambo 22 tu tuliyoiungana unadhani tutaelewa mkuu?

Ama katiba ifute serikali ya Zanzibar au tuifute kwa nguvu tuwe na serikali moja au ziundwe tatu tujue tumeungana nini na wapi.
 
Kama 2 ni muungano wa federation na kilanchi inaendelea kua na utawala wa ndani sasa je raisi wa tanganyaka yuko wapi?.
Cha kushangaa ni Paskali kudai anatoa elimu ya Uraia lakini hataki kujibu maswali. Pascal Mayalla njoo wajibu watu humu. La sivyo badilisha title. Badala ya kusema unatoa elimu ya Uraia Sema tunatoa mawazo yako kuhusu Muungano.
 
kuzira, kususa, kugoma tena kwa mihemko na ghadhabu kwa hoja na majadiliano ya kawaida na ya kiungwana namna hii si ndio utimbakwiri wenyewe huu. Sasa unapanic nini na wakati naona una mawazo na hoja nzuri tu?
Hata mimi nakubaliana kabisa ni majadiliano ya kiungwana. Nisichokubaliana nacho ni ' exploitation ya sehemu ya jamii yetu' ili kutengeneza mazingira fulani. Ukisoma hiyo article kama si msomaji utakubaliana nayo 100%.
Ukiwa na weledi itakupa ghadhabu kwasababu kinachofanyika ni 'exploitation' tu
si utulie upate elimu ya uraia, fatilia vipindi na makala mbalimbali ili kuongeza uelewa na ufahamu zaidi juu ya masuala haya ya Muungano. kughafilika au kupotoka ni mambo ya kawaida tu 🐒
Ninafuatilia lakini pia siwezi kuendelea kuinajisi akili yangu kwa kuamini kuna 'Federation ya nchi mbili, Tanzania na Zanzibar''. Hapana aisee! Huu upotoshaji wa Tanzania ni nchi tofauti kabisa na Zanzibar ni wa ki-CCM.
kuzira, kususa, kugoma tena kwa mihemko na ghadhabu kwa hoja na majadiliano ya kawaida na ya kiungwana namna hii si ndio utimbakwiri wenyewe huu. Sasa unapanic nini na wakati naona una mawazo na hoja nzuri tu?
Well kama ni utimbakwiri let it be, ninachosema hapa ni kwamba sikubaliani na upotoshaji.
Nafahamu watu wengi wanachanganyikiwa hivyo ni muhimu wale wanaoelewa wasikae kimya
si utulie upate elimu ya uraia, fatilia vipindi na makala mbalimbali ili kuongeza uelewa na ufahamu zaidi juu ya masuala haya ya Muungano. kughafilika au kupotoka ni mambo ya kawaida tu 🐒
Huu muungano unaosema kwamba ni 'adhimu na adimu' bila kujua maana yake unachanganya.
Tunawezaje kusema ni Raia wa nchi moja wakati Raia wa Tanganyika hawana haki Zanzibar.
 
Well narrated
 
Sisi wana CCM tujikite kujibu hoja kuhusu kero za muungano.
Ukweli ni kuwa kuna kero nyingi tu.
Na bila kutatua hizi kero muungano utakuja kuvunjika siku zijazo.
Mfano, kuna serikali ya mapunduzi ya Zanzibar,je ya Tanganyika iko wapi?.
Zanzibar kuna mpaka bendera inayoonesha taifa/nchi, lakini ya Tanganyika iko wapi?.
 
Si kweli, hoja za kibaguzi zimekuwepo muda mrefu , zilinyamaziwa kwasababu wanaosema ni Wazanzibar.
Umesahau mamlaka kamili? Umesahau vitambulisho vya Uzanzibar ukaazi.
Umesahau kwamba waliolitanganza na kuliibua jina la Tanganyika ni Wazanzibar.
Umesahau kwamba wameondoa mambo katika katiba kwa ubaguzi bila kuwashirikisha Watanganyika.

Ubaguzi wa Wazanzibar upo , kinachoonekana sasa ni reactions na kwaville ni 'taboo' kwa Mtanganyika kuusema Muungano, wapotoshaji wanakuja na elimu ya Uraia kwamba hili ni jambo jipya!


Tanzama hapa watoa elimu ya uraia wanavyojjichanganya.

''Majina yalibadilika na kuwa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani'' halafu jina la Zanzibar likaendelea!!!
Yaani majina yalibadilika halafu lile la Zanzibar likaendelea! it does not make sense at all.
Ukibadilisha jina la Paskali kuwa Pascal halafu ukaendelea kutumia Paskali umebadili nini? Ubabaishaji tu

''Sababu za jina llilobadilika la Tanzania Viswani na kisha kubaki kuwa Zanzibar ni kutokana na uadhimu na uadimu wa Muungano wet'' Hakuna mtu anayejua uadimu na uadhimu ni kitu gani.

Kwa sisi tunaosoma katikati ya mistari hiyo ni njia ya kubabaisha watu kwa kutumia maneno ''uadimu na uadhimu'

Again maneno hayo hayajibu hoja ya kwanini jina lililobadilika la Tanzania Visiwani kisha llikabaki Zanzibar ilitokea hivyo. Hakuna majina ni ubababisha tu na hili ndilo tunalipiga vita

Hatuhitaji vipindi ellimu ya namna hii, wala hii si elimu ni ubabaishaji tu
Kinachoshangaza katika media house kuna editorial board, hivi hili hawakuliona!




 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…