Restless Hustler
JF-Expert Member
- Apr 9, 2017
- 5,150
- 20,025
Kwa kawaida Huwezi Kumlazimisha mtu kuamini kile unachokiamini au kuiacha njia anayoiona yeye ni sahihi alafu wewe umuambie amepote!
Kwa muda mrefu tumekuwa tukiwasikia wanaoenda kwa waganga na kutumainia nguvu za giza. Tukiwauliza wengi wao kwamba wanasema:
1. Mungu amesema nisaidie nikusaidie; kauli hii inashangaza kwani kwenye vitabu vya dini kuu mbili haipo, sasa kama haipo wao waliitoa wapi? Au labda kwa Hinduism na Buddhism?! Hata hivyo, kama hiyo kauli iliandikwa kwenye vitabu vya hizo dini, nakua najiuliza Mungu alishindwa nini hadi aombe msaada kwetu?! Je kwenda kwa mganga na kuzitumaini njia za giza ni kumsaidia Mungu?!
2. Waganga waliumbwa na Mungu ili watusaidie sisi; Hii ni hoja nyingine inayoshangaza kwani hao waganga wanategemea mashetani kuwapa information za wateja na formula za utatuzi wa matatizo yao. Laiti wangemtegemea Mungu ingekuwa rahisi kusadiki kwamba ni Mungu ndiye aliwapa kazi hiyo.
Na Hizo ndizo hoja zao kuu mbili. Kama kuna nyingine tuongeze