Hoja zinazofundua akili: Uwepo wa Mungu na dalili zake

Hoja zinazofundua akili: Uwepo wa Mungu na dalili zake

Travis Walker

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2017
Posts
323
Reaction score
334
TUCHUKULIE KUWA HAKUNA MUNGU
Ikiwa Mungu hayupo mimi, wewe na vinavyotuzunguka as a nature pia vingekuwa havipo kabisa. Na kwanini labda ninasema hivyo. Vizuri, nina hoja muhimu sana. Tuchukulie tunakubaliana na wanasayansi kuwa sisi tulikuwa nyani au sokwe kama ilivyo elezwa kwenye vitabu vyao.

Muda ukatubadilisha taratibu tukawa viumbe wenye maarifa kushinda hata hao masokwe na nyani waliopo sasa ulimwenguni. Ikiwa ni hivyo kuna masuali ya kujiuliza kama kweli sisi tulikuwa sokwe. Jee huyo sokwe wa kwanza alikujaje hapa na alitokea wapi. Alikuta ulimwengu huu tunaoujua au yeye ndiye alileta kila kitu? Na kama sisi sio sokwe, jee binaadamu wa kwanza anatokea wapi na aliletwa na nani?

Hivyo tunapofikiria masuali haya huleta infinity loop yaani muendelezo wa masuali na majibu yasiyofika mwisho yenye kujirejea. Kama vile mfano wa kuku na yai. Kwa akili za binaadamu, baadhi yetu tunazikataa hoja hizi bila ya kupata majibu sahihi na kutengeneza ukomo wa kusema sisi hatuna asili. Na wengine katika sisi tunalazimika kukubaliana kuwa kuna ulazima wa kuwepo chanzo na asili yetu.

TUKIKUBALI KUWA KUNA MUNGU
Tunaposema tunakubali kuna Mungu tunaamini kuwa yupo mwenye ufahamu na ujuzi ambaye yeye hayupo kama sisi na ndiye muhusika wa yote haya kutokea kwa mabilioni ya miaka mpaka sisi tukaja katika uwepo. Hiyo inashawishi kwa namna moja au nyengine kwa sababu ya kwanza ulimwengu ulivyojitengezea mazingira ya ku support wanaoishi humu ikiwemo sisi binaadamu pamoja na viumbe vyengine.

Kwakuwa vitu haiwezekani kuja katika mpangilio ulio-imara kama hivi yaani dunia ina mahitaji ya kila kitu yanayosababisha sisi tuendelee kuishi: chakula, mavazi, hali ya hewa na n.k yote haya yanakuwepo kwa ajili ya kusababisha uwepo wetu uwendelee. Kwasababu hiyo inashawishi kulazimisha kuwa yupo mmoja alietutengeneza na anajua sisi tunahitaji nini ili tuendelee kuishi kama inavyopaswa.

TUNAPOFIKIRIA KUHUSU MUNGU.
Ni kawaida mwanadamu kuwa na hamu na uchu wa kutaka kufahamu kitu kwa undani zaidi. Na ni kwasababu akili ya mwanadamu inajifunza kwa mfumo wa pattern yaani kwa kufikiria na kuigiza. Hivyo baada ya muda huanza kujiuliza masuali baada ya kuamini uwepo wa mungu. Huenda tukawa tunajiuliza kama Mungu yupo sasa huyo na yeye amekujaje na ametokea wapi.

Tukija na masuali haya tunakuwa hatuyakwepi kabisa ila itachukua milele kupata majibu sahihi na kufunga mjadala. Kwasababu tukisema yupo mwengine kabla ya mungu inabidi pia tujiulize na huyo Mungu mwengine na yeye katokea wapi na alikujaje mfumo wa masuali na majibu haya ni paradox ya infinity loop ambayo kamwe hatufungi mjadala hata tukipewa mamilioni ya miaka ya kuishi.

TUKIFIRIA MUNGU KUWA NI MWANZILISHI WA UUMBAJI (FOUNDER OF CREATION)
Katika historia tunawasifu watu wengi kwa mambo waliyofanya ambayo mwanzo hayakuwepo. Kwa mfano TV ama Runinga mwanzo ilikuwa haipo lakini kuna mtu alifikiria na kuileta Runinga na yeye tunamwita mwanzilishi kwasababu awali hakukuwa na TV. Sasa tunapomuamini mungu kuwa ni muanzilishi wa uumbaji inabidi tukubali kuwa yeye sio kiumbe bali ni muanzilishi wa kila kitu.
 
Hapo ni sawa na kupambanisha vitu viwili vinavyokinzana vyenye msimamo tofauti

Revelation vs Science & Human Reasoning

Religion vs Cult

Bible/Qur'an scripture vs Man's Reasoning Scripture

Catholicism vs Freemasonry

Ushaelewa na hio ni vita na sio vita ndogo
 
As for me,kila mtu aamini anachoamini!

Sote tunaopumua leo ipo siku inakuja tutayaona yale waliyoyaona wenzetu walionyamaza so huko kama atakuwepo Mungu au hatokuwepo itakuwa ni juu yangu mimi,wewe yule na yule hakuna haja ya kuumizana akili.
 
Huyo mungu nae katokea wapi? Jiulize na hili ili utokomee kifikra mbele Kwa mbele ukapate majibu mengine
 
@Sir Midabwada akili ya mwanadamu huwa ina limit ya uwezo wa kufikiria.....mungu alikuwepo kabla ya kila kitu kuwepo.elewa hivyo.
Kinachosababisha ni kwamba hatujaanza KufkiriA beyond. Na hapo ndipo majiniazi wanatkeaga. Dhana ya mungu Ina maswali mengi mnoo. Na kadri tunavyozid kuaminishana kuhus mungu ndipo mamb mengine hayaonekani
 
Back
Top Bottom