Kweli kabisa, kubadili hali ya hewa ni changamoto kwa wafugaji wote, iwe samaki,kuku,nk Kiegea Moro kuna mjeshi mmoja ana ng`ombe balaa, au kama unaweza kwenda Kwa Pm mmoja mstaafu, unaweza pata mbegu na kwa gharama ndogo sana. Najaribu kumtafuta Vert.officer mmoja rafiki yangu, alikuwa anauza hawa ng`ombe na yupo Ubungo. Nikimpata nitaweka data hewani.
Wakuu asanteni sana kwa michango yenu:
Hii nchi yetu haina mipango yoyote ya maana, nd'o maana Malila uliomba uuziwe shamba la Kitulo ili uliendeleze na ulifanyie kazi ya maana.
Pale Kitulo wanatoa pure breed Freishian wanaotoa maziwa 30-40 lts in 24 hours.
Wanapandisha mitamba, wanapima kama imepata mimba kila baada ya miezi mitatu (wale wanaopatikana wana mimba wanagawanywa sehemu mbili, nusu ya kwanza wanabakizwa kwa kuendeleza kizazi, nusu nyingine wanauzwa kulingana na order; japo mtu mmoja anatakiwa kuchukua ng'ombe mmoja tu kwa sababu ni wachache). Aibu hii! Mi' nimeweka order toka August, 2011 ili nichukue November, 201; watapima tena mwezi February, 2012.
Kuna mfugaji mwingine ambaye nilishapewa contacts zake ambaye yeye niliambiwa ni Mkurugenzi sijui wa nini, anashamba kubwa. Nilimtumia email toka August, nikawa nimekata tamaa kwa kutojibiwa, lkn this week alimwomba msimamizi wake anijibu, nikajibiwa kuwa wana ng'ombe 300, lkn wanahitaji wawe 450, kwa hiyo na wao wanatafuta 150 zaidi kwa sababu wameshaanzisha milk processing plant. Hii ni sehemu ya email hiyo: ".....Dear ....,
My name is ...... coordinator of Molomo and Gararagua Farm situated West Kilimanjaro.
Regarding your information of keeping dairy cattle is the good idea
1.0 For the time being we are not able to sell to you our dairy cattlle because our road map shows that we have to increae dairy cattle up to 450 from current 300 dairy cattle
2.0 Concering selling of heifers we cant afford while are looking for heifer to increase our milk production.
For your information we have managed to build our own milk processing plant and we still in trials run.
3.0 The current price of dairy catle in open market it range from 800,000/= to 1,200,000/=
4.0 The minimum and maximum amount of milk production per cow depend on compound meal you feed you dairy cattle and weather
I think you got my concept
Best regards,
............
..........."
Sikukata tamaa nikajikuta najuana na mTz aliyepo Republic of South Africa (through mtandao) akaniambia nicheck
www.investindairycattle.co.za na
www.hooggekraal.co.za. Nikamchokoza huyu jamaa anyepatikana kwenye website ya pili (
www.hooggekraal.co.za) akaniomba namba ya simu ili YEYE ND'O ANIPIGIE aniulize vizuri.
Anasema:
(1)Heifer (mtamba) mmoja mwenye mimba ya miezi 6 anauza kwa 1,550 rands sawa na 3,25,000 Tshs
(2)Hauzi ng'ombe wasio na mimba, mfano: ndama wa umri wa miezi 8-9
(3)Kama ni kusafirisha, KIASI CHA CHINI KABISA anachoweza kusafirisha ni ng'ombe 40 - chini ya hapo hafanyi biashara hiyo.
Mnaona nchi za watu wanavyotupiga bao?
Linganisha na kwetu:
(1)Kupata mtamba bora wenye mimba ni issue
(2)Hata kama wenye mimba wapo hakuna atakayekubali kukuuzia
(3)Serikali yetu haina uwezo wa ku-supply ng'ombe kwa watu kutokana na mahitaji, KIASI CHA JUU KABISA ambacho serikali yetu inaweza kumuuzia mtu ni ng'ombe mmoja (1)!
Kwa sasa nasubiri kang'ombe kamoja toka Kitulo, hopefully nitapata kengine February.
Inamaanisha kuwa nikitaka niwe na ng'ombe 20 kuanzia November, 2011 basi ujue nitafikia lengo hilo November, 2015 wakati huo huo hawa wa mwanzo watakuta walishajichokea! Shame on you Tz!