Homa kali baada ya c-section

swtlady

Senior Member
Joined
Oct 22, 2013
Posts
156
Reaction score
103
Msaada wa kitabibu,nimejifungua kwa operation wiki mbili zimepita napata homa kali na maumivu makali ya tumbo.pia nnaharisha na kutapika.nimerudi hospitali niliyofanyiwa upasuaji majibu ninayopata hayaridhishi.niliongezewa maji ya uchungu chupa nne ndio wanadai yananifanya hivyo kwahiyo ninywe maji ya kutosha maumivu na homa vitaisha.ila naona hali inazidi kila kukicha wenye utaalamu naomba msaada wenu tafadhali.
 
kidonda kikoje, unatokwa na uchafu wowote uken, na unaharu isiyo ya kawaida,.....kama ndio utakuwa umepata sepsis "peuperial sepsis"
ni vzuri kuangalia pia kama hauna UTI au malaria.....
 
Kidonda kimepona na hakuna uchafu wowote zaidi ya normal bleed.malaria na Uti vyote nimepima ni non reactive.
 
Homa baada ya kujifungua sio nzuri. Nenda kaonane na gynecologist haraka, ikiwezekana usiku huu huu. Uko mkoa gani?
 
Pole sana mama...kama umefanya vipimo vyote hivyo na vyote viko normal...inawezekana ni viral septisemia tu ....ambayo inatibiwa na antibiotics....sometimes theatre zetu sio safi sana ndo maana unaweza kupata sepsis kirahisi. Otherwise yaweza pia kuwa ni viral infection ambayo nyingi ni self limiting tu but inabidi utumie dawa za kushusha homa na kuzuia kuharisha.
Maziwa yanatoka vizuri? Hayavimbi?
 
Kidonda kimepona na hakuna uchafu wowote zaidi ya normal bleed.malaria na Uti vyote nimepima ni non reactive.

nakushauri ufike kwa daktari haraka upate uchunguzi zaidi, homa ndani ya siku 40 baada ya.kujifungua sio dariri.nzur
 
Maziwa yanatoka vizuri na mtoto ananyonya vizuri.hata mimi nilidhani nitapata majibu hayo ya infections ila wamenichanganya zaidi na majibu kuwa dripu za uchungu ndizo zinanifanya hivi.nilijaribu kujifungua kawaida ikashindikana ndio nikawekewa dripu nne pia ikashindikana nikaishia huko kwenye scissor baada ya siku mbili za maumivu makali
 
iv drip.za fluid au oxytocin hazina tatizo hilo,
 
Hata mimi nilipotoka kufanyiwa operation ya uzazi siku za mwanzo nlikuwa napata homa kali. Nlitumia panadol na antibiotics nashkuru zilinisaidia. Na sasa nipo fresh.
 

Ulienda hospitali gani
 
Pole sana Mkuu, fuata ushauri na uwahi hospitali haraka. Kila la heri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…