Ilikuwa siku kama ya leo mwaka 1997 pale kitasa bora kabisa sambamba na mbavu ya kulia ya AC Milan yaani Franco Baresi na Mauro Tassotti walitundika daruga kukiputa klabuni hapo.
Vilio vilitawala, pale mwamba na nahodha wa wakati huo Franco Baresi ambae inasemwa pasi na shaka kuwa ndie kitasa bora kupata kutokea Duniani alipoinua Mkono wake wa kuume na kuipungia Familia ya AC Milan huku wengine wakiwa na mabango makubwa yenye jumbe za kumsifu na kumtukuza mwamba huyo.
Miongoni mwa bango lililokuwa limebebwa hata kuwafunika washabiki wa AC waliokuwa nyuma ya goli maarufu kama Curva Sud lilisomeka *lasciate Sansiro, ma resterete nei nostri cuori* likimaanisha kuwa unaondoka Sansiro lakini utabaki mioyoni mwetu.
Asali ikamwagikia kwenye futari pale zamu ya mlinzi wa kulia wa chama hilo kwa wakati huo Mauro Tassotti alipoinua mkono wake na kuupungia umati wa familia hio tukufu.
Nyimbo za kumsifu mwamba huyu ambae alikuwa nahodha katika fainali ya ligi ya mabingwa mwaka 1994 dhidi ya Barcelona akivaa kitambaa baada ya Baresi kutocheza mechi hio zikaanza kuvurumishwa toka kila kona ya uwanja wa Sansiro, uwanja wenye historia kubwa ya mchezo wa soka Duniani.
Tassotti ndie alikuwa nahodha na Milan siku kizazi cha dhahabu cha Barcelona kilipocharazwa jumla ya magoli 4-0 kwenye fainali hio.
Ikumbukwe kuwa hakuna timu iliobamizwa magoli mengi zaidi ya Barcelona katika mchezo wa fainali ya UCL.
Mpaka anaaga Milan Baresi alikuwa kaichezea klabu hio jumla ya michezo 714 akianzia timu ya vijana mwaka 1972 na baadae timu ya kwanza aliocheza kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1997.
Huku Mauro Tassotti aliichezea klabu hio jumla ya michezo 576 Wataliano hawa wamepewa heshima kubwa, sio ndani ya jiji la fasheni la Milan tu, bali kila kona ya nchi hio.
Forza Milan...
@gang_chomba🇰🇪