Anayebadilisha Mtu ni Mungu halafu kumbuka huyo Mungu unayedai kumuabudu anachukia kuachana. Na ukisoma Biblia haikupi mamlaka ya kuolewa tena unapotengana na mumeo ni kifo tu kinawatenganisha. Kuna laana unapoachana na mke/mume wa ujana wako. Mungu habadiliki jamani hata mimi nilikuwa mlevi lakini hakuna mahali mke aliniacha Mungu ndiye aliyenibadilisha. Kumbuka ndoa yenu ni hadi kifo jump in jump out hutopata utakacho kwakuwa Mungu amekiweka kwa mumeo. Soma
Malaki 2:13-16
[13]Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya BWANA kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia.
[14]Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu BWANA amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.
[15]Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana.
[16]Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.
Zingatia hayo mama zingatia sana usije kujuta mbeleni