Hongera Azam FC, lakini...

JFMemba

Senior Member
Joined
Jun 28, 2021
Posts
134
Reaction score
247
Kwa miaka kadhaa sasa watu wengi tumekuwa hatuielewi club ya Azam FC. Na hii ni kutokana na nguvu kubwa wanayotumia kuitangaza na kuboresha miundombinu vs kikosi na matokeo uwanjani.

Hakika timu imekuwa haieleweki na huwezi kuitofautisha na kina Mbeya City, Kagera Sugar, etc.

Mwaka huu tunaona kama wanataka kuwa serious maana tayari kuna sajili nzuri zimefanyika na naamini wataendelea kufanya hivyo maana bado kuna maeneo machache yanapaswa kuongezwa nguvu.

Kwanza upande wa Golikipa. Huyu mganda kama ndiyo mnatarajia kumtumia kama No. 1 msimu ujao basi hapo kuna kasoro. Huyu si mzuri sana hata yule Mghana Abdulrazack Barola anamzidi sana tu. Lazima atafutwe Golikipa wa ukweli wa kuhimili michuano mikubwa ijayo.

Pili bado nina wasiwasi na nafasi ya kiungo mkabaji. Lazima atafutwe mtu mwenye nguvu na kasi.

Kadhalika ongezeka straika mpambanaji ili kutoa ushindani kwa Dube ambaye naona ana kismati cha majeraha.

Mwisho kama Ntibanzonkiza yupo free mchukueni ni mpambanaji mzuri tu na anaweza kusainia kuwa na kikosi kipana na anaweza kutumika kwenye baadhi ya mechi na ASFC.

Kwa miaka hii zaidi ya kumi ambayo mpo ligi kuu mlitakiwa kuwa tayari mmejenga fan base nzuri ila inashindikana sababu mnakuwa kama vile hampo serious. Watoto wanaokuwa wangekuta kuna timu inazinyanyasa Simba na Yanga wale wasingejiunga huko. Na nafasi hiyo mnayo

Kila la kheri.
 
Msimu huu utakua msimu bora tangu ianze Ligi Kuu
 
Itakuwa vema sana tukiwa na angalau timu 4 zenye viwango kama walivyoonyesha Simba msimu/mwaka huu, ili kuleta ushindani wa kutosha kwenye ligi ya ndani na kwenye mashindano ya kimataifa.
 
Itakuwa vema sana tukiwa na angalau timu 4 zenye viwango kama walivyoonyesha Simba msimu/mwaka huu, ili kuleta ushindani wa kutosha kwenye ligi ya ndani na kwenye mashindano ya kimataifa.
Sema Simba na Yanga zote viwango vyao vipo sawa.
 
acha kufananisha Simba na vitu vya kijinga
Vtu vya kijinga wakati ndiyo timu iliyo ku-outplay 1vs1 mwaka huu.
Timu mbili tu ndiyo zimeishinda Simba mwaka huu ukiweka 1vs 1.

Kaizer Chiefs
Young Africans
Uwe unatumia data katika kuwasilisha mawazo yako. Usipende kushikiwa ubongo na Ambangile au Kitenge.
 
kwa hiyo Ruvu na Prison walioifunga Simba viwango vyao vinafanana? Timu ya 12 Afrika unaifananisha na timu la 145?
 
kwa hiyo Ruvu na Prison walioifunga Simba viwango vyao vinafanana? Timu ya 12 Afrika unaifananisha na timu la 145?
unajua maana ya 1 vs 1?
Factors zote ziwe constant, kwa mwaka huu, kwa vikosi hivi Simba na Prisons wamecheza mara ngapi? Nani kamzidi mwenzake mabao?
Simba na Ruvu wamecheza mara ngapi? Nani kamzidi mwenzie mabao?
Halafu ufananishe na Yanga.

Au ukitaka msikilize Ambangile au Shaffi akuhadithie jinsi mlivyoupiga mwingi au biriani au sijui gwaride etc ....
All in all mwaka huu Simba na Yanga wamecheza 4 times Yanga kaibuka mshindi 2 times na Simba ONCE na draw ya chupuchupu.
Tumecheza four times bro, usitongee mambo uchawi, tumia data ku-argue.
 
Simba kakutana mara mbili na Al ahly, moja kashinda moja kafungwa, idadi ya magoli ni sawa, so kwa mfano wako ni sawa na kusema simba iko level sawa na Ahly! Seriously?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…