Kwa miaka kadhaa sasa watu wengi tumekuwa hatuielewi club ya Azam FC. Na hii ni kutokana na nguvu kubwa wanayotumia kuitangaza na kuboresha miundombinu vs kikosi na matokeo uwanjani.
Hakika timu imekuwa haieleweki na huwezi kuitofautisha na kina Mbeya City, Kagera Sugar, etc.
Mwaka huu tunaona kama wanataka kuwa serious maana tayari kuna sajili nzuri zimefanyika na naamini wataendelea kufanya hivyo maana bado kuna maeneo machache yanapaswa kuongezwa nguvu.
Kwanza upande wa Golikipa. Huyu mganda kama ndiyo mnatarajia kumtumia kama No. 1 msimu ujao basi hapo kuna kasoro. Huyu si mzuri sana hata yule Mghana Abdulrazack Barola anamzidi sana tu. Lazima atafutwe Golikipa wa ukweli wa kuhimili michuano mikubwa ijayo.
Pili bado nina wasiwasi na nafasi ya kiungo mkabaji. Lazima atafutwe mtu mwenye nguvu na kasi.
Kadhalika ongezeka straika mpambanaji ili kutoa ushindani kwa Dube ambaye naona ana kismati cha majeraha.
Mwisho kama Ntibanzonkiza yupo free mchukueni ni mpambanaji mzuri tu na anaweza kusainia kuwa na kikosi kipana na anaweza kutumika kwenye baadhi ya mechi na ASFC.
Kwa miaka hii zaidi ya kumi ambayo mpo ligi kuu mlitakiwa kuwa tayari mmejenga fan base nzuri ila inashindikana sababu mnakuwa kama vile hampo serious. Watoto wanaokuwa wangekuta kuna timu inazinyanyasa Simba na Yanga wale wasingejiunga huko. Na nafasi hiyo mnayo
Kila la kheri.