Centrehalf
JF-Expert Member
- Jun 9, 2013
- 509
- 145
Salaam kwa wote.napenda kuchukua nafasi hii kulipongeza bunge la katiba kwa kazi nzuri waliofanya kwa moyo wote na nguvu zao zote mpaka kukamilisha zoezi la kutengeneza kanuni.ni katika mchakato huu watanzania tumeweza kupata picha halisi ju ya ufahamu/uelewa wa baadhi ya wajumbe wa hili bunge la katiba.maana tumeshuhudia baadhi ya wajumbe kukosa staha na wengine kukosa aibu mpaka kudiliki kufanya mambo ya hovyo kabisa ndani ya bunge tukufu na la kihistoria.mbali na wajumbe tumeshuhudia jinsi baadhi ya vyama vya siasa kutaka kuhodhi mamlaka ya bunge la katiba kwa kutumia mbinu mbalimbali lakini bila mafanikio.kwangu mimi naona kama bunge la katiba limesheheni watu wasomi.makini,waadilifu na wazalendo.nikianza na kamati ya kanuni iliyo kua chini ya prof costa mahalu akisaidiwa na tundu lissu ,bakari hamisi na wajumbe wengine wamefanya kazi nzuri ya kuhakikisha hakuna kanuni itakayotungwa kwa ajili ya kunufaisha kundi fulani au chama fulani bali kwa ajili ya manufaa ya watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa au dini.ju ya yote ni kwa mwendo huohuo nategemea kuona wabunge nao wakipitisha mambo ndani ya rasimu kwa kujali taifa badala ya vyama vyao vinavyoweza kufutika wakati wowote.pamoja na kelele zote zakutofautiana ndani ya bunge mwishowe tumepata kanuni nzuri naomba hata katiba iwe nzuri ili historia iwakumbuke kwa hili.nawasilisha.