Hongera CCM Mabaraza ya Katiba. Vyama vingine igeni mfano

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,895
Reaction score
20,392
Wana JF,

Kwa sasa macho na masikio ya Watanzania wengi yapo Dodoma ambako vyombo vya juu vya maamuzi vya Chama Cha Mapinduzi, Chama Tawala (CCM) vinaketi ambapo pamoja na mambo mengine vinajadili Rasimu ya Katiba Mpya. Kwa hakika imedhihirisha kuwa CCM ni chama tawala na chama kongwe. Chama hiki kimeonesha kuwa kiko makini kushiriki mchakato wa Rasimu ya Katiba tofauti na vyama vingine. Kwa sasa hata viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani wameacha kueleza yanayoendelea ndani ya vyama vyao na badala yake wanaeleza yanayoendelea ndani ya Kamati Kuu ya CCM hata kama hawajui nini kinajadiliwa.

Wakuu, CCM imewapiga bao la kisigino vyama vingine kutokana na mfumo wake wa uongozi uliokamilika. kutokana na mfumo huo, CCM imeweza kukusanya maoni ya wanachama wake kuanzia ngazi ya balozi wa nyumba 10 hadi Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa urahisi na bila ya kuhusisha gharama kubwa tofauti na vyama vingine. Mathalan, kutokana na chama kikuu cha upinzani nchini, CHADEMA kutokuwa na watu makini mikoani na wilayani, sote tumeshuhudia jinsi viongozi wakuu walivyohangaika kupita maeneo mengi eti kwa lengo la kukusanya maoni ya wanachama wake. ziara hizo si tu hazikukufanikisha lengo bali pia zimesababisha matumizi makubwa ya fedha za chama, gharama ambazo zingeweza kuepukika kama viongozi wa chama hicho wangepanga njia bora ya kukusanya maoni. Pia ziara hizo zimesabaisha viongozi wa CHADEMA wakikiuka masharti ya kufanya mikutano ya hadhara hali iliyowafanya watiwe nguvuni huko Iringa kutokana na kuzidisha muda wa mkutano. haya yote ni madhara ya Chama kuongozwa na watu ambao si tu hawako makini lakini pia hawajui nini cha kufanya.

vyama vingine vya upinzani navyo vimeshindwa kuwa na mfumo kamili wa kukusanya maoni toka kwa wanachama wake badala yake ni viongozi wa juu tu ndio wamekaa na kutoa msimamo wa chama kama vile ambavyo hata CHADEMA wamefanya. Hapa ni vema nikaeleweka kuwa walichokuwa wanafanya CHADEMA si kukusanya maoni ya wanachama wake bali walikuwa wanawaambia wananchi nini msimamo wa chama juu ya Rasimu hiyo ya Katiba. Mathalan, katika mikutano yao yote, walikuwa wananadi Muundo wa Serikali Tatu, Kutumia jina Tanganyika badala ya Tanzania bara, Umri wa mgombea urais kupunguzwa kutoka miaka 40 hadi miaka 18, haki ya kuandamana, haki ya kugoma na uwezekano wa Tanzania kuruhusu ndoa za jinsia moja kwa kigezo cha demokrasia. wanachama wamekuwa hawapati muda wa kutoa mawazo mbadala na badala yake viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakitumia muda mwingi kuhutubia badala ya kusikiliza. hata pale mawazo yalipotolewa ambayo ni tofauti na msimamo wa CHADEMA, mtoa wazo aliishia kuzomewa na kutukanwa na maoni yake hayakurekodiwa popote.

Wakati muda wa mwisho wa kuwasilisha maoni yaani Agosti 31 ukiwa unakaribia, ni CCM pekee ndicho kilichoketi kama chama kupitia Kamati Kuu kuchambua na kujadili maoni ya wanachama wake. vyama vingine vipo kimya na vingine vimekuwa vikiendelea na jitihada za kufanya mikutano. Ni wakati muafaka sasa kwa vyama vingine vikaiga mfumo wa CCM kwa vile umeleta ufanisi na umeokoa gharama. Hakika Mkubwa ni Mkubwa tu na siku zote ukiona vyaelea ujue vimeundwa
 
Hongereni CCM. Hakika nyie ni chama makini na mnatetea maslahi ya taifa. Vvyama vingine vina ajenda ya kusambaratisha taifa hili
 
Hakuna cha maoni hapo wanacho kifanya ni kuwaandalia wananchi katiba badala ya kuwaachia wananchi wajiandalie katiba yao kwa kupitia tume yao waliyoichagua.
 
Mkuu hapa Swali la muhimu ni lini Hawa wanachama Wenu Wa CCM wamekutana kama mabaraza na kutoa maoni yao juu ya rasimu ya katiba.

Lini haya mabaraza yalitangazwa Na yalifanyika lini Na kwa utaratibu upi. Kina nani walioshiriki Kama ni wanachama wote Au ni viongozi Wa chama
 
YANI WE KM JINA LAKO UNGETOA HERUFI LU..UKAWEKA. KI. JINA LAKO INGEKUWA LINAKUFAA..WEWE ACHA KUDANGANYA WANANCHI WE ARE NOT STUPID AS YOU THINK GO WITH YOUR EGO--TRIP
There are two ways to live: you can live as if nothing is a miracle; you can live as if everything is a miracle.
Albert Einstein
 
Mkuu, Tume ya Katiba chini ya jaji Warioba ndiyo mwamuzi wa mwisho. si ccm wala chadema ambacho kitajinasibu kuwa ndicho kilichofanikisha katiba hiyo. kumbuka, Tanzania ni zaidi ya CCM na CHADEMA. kuna wadau wengi wametoa maoni yao na si vyama vya siasa tu
 
kama wewe unaona inafaa kiweka Ki badala ya Lu, hiyo ni tafsiri yako. mie sipo katika kutukanana kwani matusi hayajengi na sijazoea. labda kama wewe ndivyo ulivyolelewa hivyo
 
Wana JF,

Kwa sasa macho na masikio ya Watanzania wengi yapo Dodoma ambako vyombo vya juu vya maamuzi vya Chama Cha Mapinduzi, Chama Tawala (CCM) vinaketi ambapo pamoja na mambo mengine vinajadili Rasimu ya Katiba Mpya. Kwa hakika imedhihirisha kuwa CCM ni chama tawala na chama kongwe. Chama hiki kimeonesha kuwa kiko makini kushiriki mchakato wa Rasimu ya Katiba tofauti na vyama vingine. Kwa sasa hata viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani wameacha kueleza yanayoendelea ndani ya vyama vyao na badala yake wanaeleza yanayoendelea ndani ya Kamati Kuu ya CCM hata kama hawajui nini kinajadiliwa.

Wakuu, CCM imewapiga bao la kisigino vyama vingine kutokana na mfumo wake wa uongozi uliokamilika. kutokana na mfumo huo, CCM imeweza kukusanya maoni ya wanachama wake kuanzia ngazi ya balozi wa nyumba 10 hadi Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa urahisi na bila ya kuhusisha gharama kubwa tofauti na vyama vingine. Mathalan, kutokana na chama kikuu cha upinzani nchini, CHADEMA kutokuwa na watu makini mikoani na wilayani, sote tumeshuhudia jinsi viongozi wakuu walivyohangaika kupita maeneo mengi eti kwa lengo la kukusanya maoni ya wanachama wake. ziara hizo si tu hazikukufanikisha lengo bali pia zimesababisha matumizi makubwa ya fedha za chama, gharama ambazo zingeweza kuepukika kama viongozi wa chama hicho wangepanga njia bora ya kukusanya maoni. Pia ziara hizo zimesabaisha viongozi wa CHADEMA wakikiuka masharti ya kufanya mikutano ya hadhara hali iliyowafanya watiwe nguvuni huko Iringa kutokana na kuzidisha muda wa mkutano. haya yote ni madhara ya Chama kuongozwa na watu ambao si tu hawako makini lakini pia hawajui nini cha kufanya.

vyama vingine vya upinzani navyo vimeshindwa kuwa na mfumo kamili wa kukusanya maoni toka kwa wanachama wake badala yake ni viongozi wa juu tu ndio wamekaa na kutoa msimamo wa chama kama vile ambavyo hata CHADEMA wamefanya. Hapa ni vema nikaeleweka kuwa walichokuwa wanafanya CHADEMA si kukusanya maoni ya wanachama wake bali walikuwa wanawaambia wananchi nini msimamo wa chama juu ya Rasimu hiyo ya Katiba. Mathalan, katika mikutano yao yote, walikuwa wananadi Muundo wa Serikali Tatu, Kutumia jina Tanganyika badala ya Tanzania bara, Umri wa mgombea urais kupunguzwa kutoka miaka 40 hadi miaka 18, haki ya kuandamana, haki ya kugoma na uwezekano wa Tanzania kuruhusu ndoa za jinsia moja kwa kigezo cha demokrasia. wanachama wamekuwa hawapati muda wa kutoa mawazo mbadala na badala yake viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakitumia muda mwingi kuhutubia badala ya kusikiliza. hata pale mawazo yalipotolewa ambayo ni tofauti na msimamo wa CHADEMA, mtoa wazo aliishia kuzomewa na kutukanwa na maoni yake hayakurekodiwa popote.

Wakati muda wa mwisho wa kuwasilisha maoni yaani Agosti 31 ukiwa unakaribia, ni CCM pekee ndicho kilichoketi kama chama kupitia Kamati Kuu kuchambua na kujadili maoni ya wanachama wake. vyama vingine vipo kimya na vingine vimekuwa vikiendelea na jitihada za kufanya mikutano. Ni wakati muafaka sasa kwa vyama vingine vikaiga mfumo wa CCM kwa vile umeleta ufanisi na umeokoa gharama. Hakika Mkubwa ni Mkubwa tu na siku zote ukiona vyaelea ujue vimeundwa

Kwa swala la umakini hakuna anayebisha, ndio maana umakini umetuletea maisha bora kwa kila Mtanzania,
Ndio maana Umakini umekomesha ufisadi, Ndio maana umakini Mdawa ya kulevya hayapo Tanzania, ndiyo maana kwa umakini hakuna mtu yeyote anayetekwa wala kutolewa kucha na macho, Ndiyo maana kwa umakini sasa sukari na mfumuko wa bei ya vyakula umeshuka, ndiyo maana kwa umakini sasa Tanzania inamiliki hisa kwenye makampuni ya madini, Ndiyo maana kwa umakini hata vyombo vya usalama vinafanya kazi yake kwa umakini, ndiyo maana kwa umakini hata magazeti na redio zilizofungiwa zimefunguliwa.

Yaani wa sababu za Umakini wa CCM tulipata mchakato wa Katinba ambao hata haukuwa kwenye Ilani yake, Kwa sababu ya Umakini wa CCM VIJANA WA FORM FOUR HAWAKUFELI, KWA SABABU YA UMAKINI WA ccm pesa za EPA hazikuibiwa, kwa sababu ya umakini wa CCM lowasa hakujiuzulu kwa kashfa ya Richmond
. Kwa sababau ya Umakini wa CCM vijana wa Kitanzania hawakamatwi na madawa ya kulevya huko ughaibuni.

VIVA! CCM VIVA!
 
Mkuu hapa Swali la muhimu ni lini Hawa wanachama Wenu Wa CCM wamekutana kama mabaraza na kutoa maoni yao juu ya rasimu ya katiba.

Lini haya mabaraza yalitangazwa Na yalifanyika lini Na kwa utaratibu upi. Kina nani walioshiriki Kama ni wanachama wote Au ni viongozi Wa chama

Mkuu, CCM kama baraza la kikatiba linaketi huko Dodoma. labda ungeuliza wamekusanya lini na kwa utaratibu upi maoni ya wanachama wake. hata walichofanya CHADEMA si mabaraza bali walikuwa wananadi kwa wanachama wao msimamo wa chama. uliza uelimike na si uliza upate cha kubishana. kuhusu lini na kwa utaratibu gani ccm walikusanya maoni kwa wanachama wake, mie si msemaji wa chama. hayo kamuulize Nape. yeye ndiye atakudadavulia kila kitu.
 
Kinachojadiriwa na Maccm unakifahamu?? kwani pia hoja ya Katiba Mpya nayo ilikuwa ni moja ya ilani ya uchaguzi kwa maccm 2010??!! Wewe Lusewe ni kilaza tu.
 
Kwa swala la umakini hakuna anayebisha, ndio maana umakini umetuletea maisha bora kwa kila Mtanzania,
Ndio maana Umakini umekomesha ufisadi, Ndio maana umakini Mdawa ya kulevya hayapo Tanzania, ndiyo maana kwa umakini hakuna mtu yeyote anayetekwa wala kutolewa kucha na macho, Ndiyo maana kwa umakini sasa sukari na mfumuko wa bei ya vyakula umeshuka, ndiyo maana kwa umakini sasa Tanzania inamiliki hisa kwenye makampuni ya madini, Ndiyo maana kwa umakini hata vyombo vya usalama vinafanya kazi yake kwa umakini, ndiyo maana kwa umakini hata magazeti na redio zilizofungiwa zimefunguliwa.

Yaani wa sababu za Umakini wa CCM tulipata mchakato wa Katinba ambao hata haukuwa kwenye Ilani yake, Kwa sababu ya Umakini wa CCM VIJANA WA FORM FOUR HAWAKUFELI, KWA SABABU YA UMAKINI WA ccm pesa za EPA hazikuibiwa, kwa sababu ya umakini wa CCM lowasa hakujiuzulu kwa kashfa ya Richmond
. Kwa sababau ya Umakini wa CCM vijana wa Kitanzania hawakamatwi na madawa ya kulevya huko ughaibuni.

VIVA! CCM VIVA!

inaelekea nilichoandika umekielewa ila unajaribu kupotosha kwa kuingiza mambo ambayo si msingi wa Rasimu ya Katiba
 
Kinachojadiriwa na Maccm unakifahamu?? kwani pia hoja ya Katiba Mpya nayo ilikuwa ni moja ya ilani ya uchaguzi kwa maccm 2010??!! Wewe Lusewe ni kilaza tu.

Mkuu, mimi sijaeleza kinachojadiliwa na CCM bali nimeonyesha jinsi CCM walivyo makini katika kujadili Rasimu ya Katiba tofauti na vyama vingine. haijalishi kuwa jambo la katiba mpya lilikuwa kwenye Ilani ya CCM au la lakini Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye Rais wa nchi ndiye aliyefanikisha hilo. vima CCM viva KIKWETE
 
inaelekea nilichoandika umekielewa ila unajaribu kupotosha kwa kuingiza mambo ambayo si msingi wa Rasimu ya Katiba
Mkuu, hizo ndo akili za Bavicha. Kila kitu wanafikiri kinyumenyume tu
 
Wewe lini umewasikia ccm wakipita mtaani kukusanya maoni kwa wananchi kama sio kudanganya taifa huko ninini? Lazima ifike mahali nyie magamba muwe na akili sio kuendekeza njaa tu. Hayo ndio matoleo yakushikiwa akili.
 
Mkuu, yaelekea kabisa hujui na wala huelewi mchakato wa katiba mpya upo katika hatua gani. kwa kukusaidia tu ni kuwa Baada ya mchakato wa kukusanya maoni kutoka kwa wananchi, mchakato ambao uliratibiwa na Tume ya Katiba, Rasimu ya Katiba iliandaliwa. Kwa sasa kinachofanyika ni wadau kujadili Rasimu hiyo. kwa kurahisisha tume imeunda mabaraza ya katiba. pia taasisi ambazo zina malengo yanayofanana kama vile vyama vya siasa ni mabaraza ya katiba. hivyo ccm kama chama imekusanya maoni kwa wanachama wake kwa utaratibu ambao imeona unafaa. CHADEMA wao kwa kutoelewa, wakaitisha mikutano ya hadhara ambapo watu wanaoenda kuhudhuria hawana malengo yanayofanana. huo ndio upunguani wa viongozi wa CHADEMA.
 
hongereni ccm. Hakika nyie ni chama makini na mnatetea maslahi ya taifa. Vvyama vingine vina ajenda ya kusambaratisha taifa hili
hongereni ccm kwa kutokukabiliana ipasavyo na wauza madawa!
 
Mkuu, Tume ya Katiba chini ya jaji Warioba ndiyo mwamuzi wa mwisho. si ccm wala chadema ambacho kitajinasibu kuwa ndicho kilichofanikisha katiba hiyo. kumbuka, Tanzania ni zaidi ya CCM na CHADEMA. kuna wadau wengi wametoa maoni yao na si vyama vya siasa tu

Kama CCM wanaithamini tume ya Walyoba kwanini Nape anawakejeli kuwa ni wazee wanaosubiri kufa?.CCM ni waumini wa sekali 2 katika rasimu ya katiba kuna mapendekezo ya serekali3 maoni ambayo yametokana na wananchi kwa mjibu wa Nape wenye akili ni wale wanaotaka sekali2 kwa maana hiyo kama huungi mkono serekali 2 wewe huna akili.Iweje leo CCM iyaone maoni ya wananchi kuwa ya maana mpaka ianze kuyajadili wakati walisha sema kuwa hawana akili?.Kama mzee butiku ambae ni miongoni mwa vikongwe wa chama cha mapinduzi amesha tamka wazi kabisa kuwa angejua kuwa chama cha mapinduzi wangeingilia mchakato wa katiba hangekubali kuwepo kwenye tume ya katiba.kwa kauli tata hizo kunahaja ya kuendelea kukiamini chama cha mapinduzi?.
 
What?Spoon feeding your members what to say you call it collecting views on Katiba?You are wasting your time.People have already said what they want.
 
eti umakini wa ccm, upi?kujifungia dodoma na kuja na maoni ya kifisadi?wanaccm huku kwetu wanalalamika kutokushirikishwa
 
Back
Top Bottom