Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392
Wana JF,
Kwa sasa macho na masikio ya Watanzania wengi yapo Dodoma ambako vyombo vya juu vya maamuzi vya Chama Cha Mapinduzi, Chama Tawala (CCM) vinaketi ambapo pamoja na mambo mengine vinajadili Rasimu ya Katiba Mpya. Kwa hakika imedhihirisha kuwa CCM ni chama tawala na chama kongwe. Chama hiki kimeonesha kuwa kiko makini kushiriki mchakato wa Rasimu ya Katiba tofauti na vyama vingine. Kwa sasa hata viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani wameacha kueleza yanayoendelea ndani ya vyama vyao na badala yake wanaeleza yanayoendelea ndani ya Kamati Kuu ya CCM hata kama hawajui nini kinajadiliwa.
Wakuu, CCM imewapiga bao la kisigino vyama vingine kutokana na mfumo wake wa uongozi uliokamilika. kutokana na mfumo huo, CCM imeweza kukusanya maoni ya wanachama wake kuanzia ngazi ya balozi wa nyumba 10 hadi Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa urahisi na bila ya kuhusisha gharama kubwa tofauti na vyama vingine. Mathalan, kutokana na chama kikuu cha upinzani nchini, CHADEMA kutokuwa na watu makini mikoani na wilayani, sote tumeshuhudia jinsi viongozi wakuu walivyohangaika kupita maeneo mengi eti kwa lengo la kukusanya maoni ya wanachama wake. ziara hizo si tu hazikukufanikisha lengo bali pia zimesababisha matumizi makubwa ya fedha za chama, gharama ambazo zingeweza kuepukika kama viongozi wa chama hicho wangepanga njia bora ya kukusanya maoni. Pia ziara hizo zimesabaisha viongozi wa CHADEMA wakikiuka masharti ya kufanya mikutano ya hadhara hali iliyowafanya watiwe nguvuni huko Iringa kutokana na kuzidisha muda wa mkutano. haya yote ni madhara ya Chama kuongozwa na watu ambao si tu hawako makini lakini pia hawajui nini cha kufanya.
vyama vingine vya upinzani navyo vimeshindwa kuwa na mfumo kamili wa kukusanya maoni toka kwa wanachama wake badala yake ni viongozi wa juu tu ndio wamekaa na kutoa msimamo wa chama kama vile ambavyo hata CHADEMA wamefanya. Hapa ni vema nikaeleweka kuwa walichokuwa wanafanya CHADEMA si kukusanya maoni ya wanachama wake bali walikuwa wanawaambia wananchi nini msimamo wa chama juu ya Rasimu hiyo ya Katiba. Mathalan, katika mikutano yao yote, walikuwa wananadi Muundo wa Serikali Tatu, Kutumia jina Tanganyika badala ya Tanzania bara, Umri wa mgombea urais kupunguzwa kutoka miaka 40 hadi miaka 18, haki ya kuandamana, haki ya kugoma na uwezekano wa Tanzania kuruhusu ndoa za jinsia moja kwa kigezo cha demokrasia. wanachama wamekuwa hawapati muda wa kutoa mawazo mbadala na badala yake viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakitumia muda mwingi kuhutubia badala ya kusikiliza. hata pale mawazo yalipotolewa ambayo ni tofauti na msimamo wa CHADEMA, mtoa wazo aliishia kuzomewa na kutukanwa na maoni yake hayakurekodiwa popote.
Wakati muda wa mwisho wa kuwasilisha maoni yaani Agosti 31 ukiwa unakaribia, ni CCM pekee ndicho kilichoketi kama chama kupitia Kamati Kuu kuchambua na kujadili maoni ya wanachama wake. vyama vingine vipo kimya na vingine vimekuwa vikiendelea na jitihada za kufanya mikutano. Ni wakati muafaka sasa kwa vyama vingine vikaiga mfumo wa CCM kwa vile umeleta ufanisi na umeokoa gharama. Hakika Mkubwa ni Mkubwa tu na siku zote ukiona vyaelea ujue vimeundwa