Unamaanisha hata Nyerere ni gaidi ,kwani alikuwa ni Mzalendo aliejitolea kupigania Freedom, Na CHADEMA kwa sasa kinazungumzia juu ya Uhuru wa mwananchi ndani ya nchi yake,uhuru ambao sasa sio unatiliwa shaka kama haupo bali ni wazi kabisa UHURU huo haupo,leo ukizungumzia tunahitaji Katiba mpya ,unaonekana adui,ukizungumza tozo zinaumiza unaonekana adui,ukizungumza maji umeme elimu hata madawati ndio kabisa umegusa pabaya,Uhuru wa kuzungumza haupo,uhuru wa kuuliza(KUHOJI) haupo .
CHADEMA wanazidi kuwafunua akili na kuwafuta wananchi matongo zaidi kuwaamsha katika usingizi unaopumbazwa na hizi sherehe feki za Uhuru wa Tanzania, Ikiwa Sherehe kama hizi za Uhuru kule Zanzibar zimefutwa,huku upande wa pili wananchi wanadanganywa mchana kweupe,kuwa wanasheherekea sherehe za Uhuru wa Tanzania ,Inajulikana wazi hakuna nchi iliyoitwa Tanzania miaka sitini iliyopita,hakuna !
Sasa hizi sherehe mnazitoa wapi ? Nyie miccm mliojaa humu dadavueni nyie ili mtufahamishe kisheria au hata kimahakama tuone uhalali wake mtuandikie na vifungu vya sheria vinavyoainisha sherehe hizo za uhuru wa Tanzania uliopatikana miaka sitini iliyopita.
CHADEMA simamieni hapo hapo mpaka wananchi waongeze uelewa zaidi maana bado uwazi unahitajika kionekane kilichojificha.
Kama ni nguvu za Jeshi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na maendeleo mingine kuonesha ufanisi ni kwenye sherehe za Muungano ilipozaliwa UNITED REPUBLIC OF TANZANIA na si penginepo.
Hizi sherehe za miaka sitini au za aina hii kila mwaka tokea Nchi ziunganishwe na kupatikana Muungano wa superglue ni sherehe batili.
CHADEMA msichoke hili nalo neno kivuli cha MUUNGANO kiondolewe iwepo Tanganyika.