Hongera Clouds radio kumshirikisha mchezaji kipindi cha michezo.

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Kama DStv vile, napenda kuupa hongera uongozi wa CMG kwa uamuzi wao wa kumshirikisha mchezaji mstaafu Amri Kiemba katika kipindi cha michezo cha siku ya Jumapili mchana kuanzia saa saba mchana.
Ukweli japo hawamtumii vilivo katika maoni yake kisoka hasa la kwetu lakini imepunguza blabla za wanaojifanya kulijua soka kwenye "mic" na kipindi kinapendeza.
 

Ila bado ' hajakomaa ' kivile katika ' analysis ' lakini ninavyomuona kwa sasa taratibu anaanza kuwa vizuri na ' with time ' atakuja kuwa bonge la ' Mchambuzi ' na kikubwa ninachokipenda kutoka Kwake Amri Kiemba ni upole wake, heshima na Mtu asiye na makuu wala mpenda Sifa / Shobo. Namtabiria makubwa kote kote kule katika Klabu yake ya REA FC akiwa kama Mkurugenzi wa Ufundi na huku katika ' Sports Analysis ' pia.
 
Nadhani sio vibaya kwa radio nyengine kufuata utaratibu huu.
TBC Taifa wao wameamua kuwa na kocha kiwanjani wakati wa mechi, nalo ni jambo zuri vilevile.
 
Hapa unawasema kiaina wale wazee wa "Namba 9 mgongoni mshambuliaji mwenye misuli na mashuti kama fataki anayesumbua uwanjani balaa" wakiwa nyuma mic.
 
Alikuwa kama mgeni au atakuwepo kweny vipindi vyote vya michezo clouds!!??
 
Alikuwa kama mgeni au atakuwepo kweny vipindi vyote vya michezo clouds!!??
Ni kitambo sasa namsikia akiwa katika kipindi hicho cha michezo cha mchana.
 
Hapa unawasema kiaina wale wazee wa "Namba 9 mgongoni mshambuliaji mwenye misuli na mashuti kama fataki anayesumbua uwanjani balaa" wakiwa nyuma mic.
Hapana mkuu, mbona siwafahamu hao πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…