Hongera CP Hamduni Salum kwa kumpigia simu Elioth Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi

Hongera CP Hamduni Salum kwa kumpigia simu Elioth Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Napenda kutumia fursa hii kumpongeza kwa dhati Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni kwa kumpigia simu mzee Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi.

Mzee Lyimo ni mfanyabiashara ambaye aliporwa TZS 25M na aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya. Inaelezwa kuwa Sabaya alikua na desturi ya kufuatilia akaunti za wafanyabiashara wakubwa na kujua kiasi walichonacho bank.

Baada ya kufuatilia akaunti ya mzee Lyimo na kujiridhisha kuwa ana "mzigo wa kutosha" bank, alimvamia nyumbani kwake akiwa na mabaunsa, pamoja na askari polisi wa kituo cha polisi Bomang'ombe. Askari hao walibaki nje ya geti wakiwa kwenye gari. Inadaiwa Sabaya aliambatana na Juma Rahibu ambaye kwa sasa ni Meya wa Moshi.

Waliingia ndani wakiwa na mabegi mawili. Walitoa silaha na kuwaweka chini ya ulinzi familia nzima. Kisha wakamchukua mzee Lyimo na kuzungumza nae. Sabaya akamwambia "nahitaji 25M sasa hivi, ama nikukabidhi haya mabegi yawe yako"

Akafungua kumuonesha begi moja lina bangi na jingine lina mirungi. Mzee Lyimo akaona anatengenezewa kesi ya madawa ya kulevya ambayo haina dhamana. Na ukizingatia umri wake anaweza kufia gerezani. Basi akakubali kutoa kiasi hicho cha pesa.

Sabaya akaagiza polisi waliokua nje na "difenda" wamsindikize bank, ambapo alienda kutoa kiasi hicho cha pesa na kuja kumkabidhi Sabaya. Matukio yote yalirekodiwa kwenye CCTV za nyumbani kwa mzee Lyimo lakini Sabaya wala hakujali. Alijua mamlaka inayomlinda ni kubwa sana.

Hata hivyo mzee Lyimo hakuridhika na akaamua kutafuta haki yake kimyakimya. Akaenda kuripoti TAKUKURU lakini hawakumsaidia, akaripoti polisi hawakumsaidia. Baadae akamwambia Godbless E.J. Lema ambaye alilifikisha kwa Waziri mkuu lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Sasa baada ya Sabaya kukamatwa, Lema akaamua kuandika tweet ya kukumbushia haki ya mzee Lyimo. Baada ya kuona tweet hiyo mamlaka zimeanza kuchukua hatua. CP Hamduni amempigia simu mzee Lyimo na tayari TAKUKURU Kilimanjaro wameshafungua jalada. Hongera sana Hamduni, naamini mzee Lyimo atapata haki yake.

1623667578618.png
 
unless alikuwa anafaidika nae.
Kabisa mkuu maana ukisikia matendo ya wasaidiz wake yanatia kinyaa Sana na jins hayat alivyokuwa akijipambanua kuwa n mzalendo mtoa haki na haya tunayoyaona na mengne kusikia Kuna shida mahali kwa intelejensia yetu na madaraka ya Rais n makubwa Sana kwa kwel

Kuna mwaka tutachagua chizi kabisa na aiuze nchi na wananchi tutaufyata kabisaa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Magufuli atakuwa alilishwa limbwata na wasaidizi wake haiwezekan mambo kam haya yatokee na awe kimya kias kile dah?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kama yeye ndiye aliyependekeza mfumo huo je,utawalaumu hao wasaidizi kwa kumlisha kinbwata jiwe au utamuonea huruma jiwe kwa kulishwa kimbwata na wasaidizi wake!!??
 
Kabisa mkuu maana ukisikia matendo ya wasaidiz wake yanatia kinyaa Sana na jins hayat alivyokuwa akijipambanua kuwa n mzalendo mtoa haki na haya tunayoyaona na mengne kusikia Kuna shida mahali kwa intelejensia yetu na madaraka ya Rais n makubwa Sana kwa kwel

Kuna mwaka tutachagua chizi kabisa na aiuze nchi na wananchi tutaufyata kabisaa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Alafu Pascal Mayalla mambo kama hayo anayaita uthubutu kiasi cha kupendeza bashite nae awe rais!!
 
Itakuwa busara huyu kiumbe afanywe mfano wa wengine wote wanaojisahau na madaraka. Hukumu yake iwe nzito kiasi kwamba akitokea mpumbavu mwingine akiwaza hata kidogo kuleta dhulma za kijinga awe na case study ya kumtuliza munkari.

Hii ni fedheha kwa nchi inayojisifu kuwa ina utawala wa kidemokrasia.
 
Alafu Pascal Mayalla mambo kama hayo anayaita uthubutu kiasi cha kupendeza bashite nae awe rais!!
Huyo kiumbe Mayalla japo ana upeo mkubwa wa fikra, lakini hajawahi weka kiini macho kwa njaa yake ya uteuzi. Mithili ya jina lake kumaanisha 'njaa' basi ni njaa hiyo hiyo ya uteuzi humtoa akili na kuandika vitu ambavyo nina hakika akikaa huwa anajishangaa hata yeye mwenyewe kama ndie muandishi hasa.
 
Huyu jamaa alikua jambaz sugu

Uuuuwwiiiiiiii mahakama tafadhali tunaomba haki itendeke

Huyu mtu alikua hatariiii

Mbona wenzake hawakufanya huu ujinga?

Huyu alikua na mambo yake binafsi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
System za TZ siyo nzuri- Hivi kwanini mpaka agizo litoke juu kama tukio limetokea katika eneo lako? Kwa mfano jana mama katilia shaka gharama za ujenzi wa jengo BOT Mwanza- Sasa kwa ishu kama ile mpaka mama awaagize tena TAKUKURU?
 
Sabaya alikuwa Ni jambazi, ila magufuli aisee,ona hata waziri mkuu alipelekewa malalamiko juu ya Sabaya, lakini akashindwa kuyafikisha kwa jiwe,aliogopa nayeye asije akapigwa chini, maana Magufuli watu dizaini ya Sabaya na matendo yao,yeye ndio alikuwa chaguo lake
 
Back
Top Bottom