Hongera CP Hamduni Salum kwa kumpigia simu Elioth Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi

Huyo kiumbe Mayalla japo ana upeo mkubwa wa fikra, lakini hajawahi weka kiini macho kwa njaa yake ya uteuzi. Mithili ya jina lake kumaanisha 'njaa' basi ni njaa hiyo hiyo ya uteuzi humtoa akili na kuandika vitu ambavyo nina hakika akikaa huwa anajishangaa hata yeye mwenyewe kama ndie muandishi hasa.
Hawezi kubadilika tena age nayo imeenda sasa
 
Jela asubui kuhamka saa 11:30, mtasikia sauti ya nyapala mkuu akisema "kunjaaaaa" basi inatakiwa haraka mwendo wa second 3 ukunjekunje kirago chako na muda uhouho mtafute ndala zenu,

hapo fasta minyororo inafunguliwa kwenye milango ya Chuma, inatakiwa mtoke uku mnakimbia kuelekea nje, wakati mnakimbia mnakuwa mnahesabiwa, ukizembea kukimbia unasikia kofi la shingoni,

Sabaya kazi anayo uko jela, halafu mkiwa mmelala kunguni Ni wengi kupita maelezo, kwenye ukuta, kwenye virago,
 
Mzee Lymo aliibiwa pesa, then akakaa kimya?

Duh?

Nyinyi watu si wa kuwaamini haraka haraka, vyombo vyetu vya usalama vikikuta Sabaya ana hatia nitaamini.
 
Napenda kutumia fursa hii kumpongeza kwa dhati Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni kwa kumpigia simu mzee Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi.

Mzee Lyimo ni mfanyabiashara ambaye aliporwa TZS 25M na aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya. Inaelezwa kuwa Sabaya alikua na desturi ya kufuatilia akaunti za wafanyabiashara wakubwa na kujua kiasi walichonacho bank.

Baada ya kufuatilia akaunti ya mzee Lyimo na kujiridhisha kuwa ana "mzigo wa kutosha" bank, alimvamia nyumbani kwake akiwa na mabaunsa, pamoja na askari polisi wa kituo cha polisi Bomang'ombe. Askari hao walibaki nje ya geti wakiwa kwenye gari. Inadaiwa Sabaya aliambatana na Juma Rahibu ambaye kwa sasa ni Meya wa Moshi.

Waliingia ndani wakiwa na mabegi mawili. Walitoa silaha na kuwaweka chini ya ulinzi familia nzima. Kisha wakamchukua mzee Lyimo na kuzungumza nae. Sabaya akamwambia "nahitaji 25M sasa hivi, ama nikukabidhi haya mabegi yawe yako"

Akafungua kumuonesha begi moja lina bangi na jingine lina mirungi. Mzee Lyimo akaona anatengenezewa kesi ya madawa ya kulevya ambayo haina dhamana. Na ukizingatia umri wake anaweza kufia gerezani. Basi akakubali kutoa kiasi hicho cha pesa.

Sabaya akaagiza polisi waliokua nje na "difenda" wamsindikize bank, ambapo alienda kutoa kiasi hicho cha pesa na kuja kumkabidhi Sabaya. Matukio yote yalirekodiwa kwenye CCTV za nyumbani kwa mzee Lyimo lakini Sabaya wala hakujali. Alijua mamlaka inayomlinda ni kubwa sana.

Hata hivyo mzee Lyimo hakuridhika na akaamua kutafuta haki yake kimyakimya. Akaenda kuripoti TAKUKURU lakini hawakumsaidia, akaripoti polisi hawakumsaidia. Baadae akamwambia Godbless E.J. Lema ambaye alilifikisha kwa Waziri mkuu lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Sasa baada ya Sabaya kukamatwa, Lema akaamua kuandika tweet ya kukumbushia haki ya mzee Lyimo. Baada ya kuona tweet hiyo mamlaka zimeanza kuchukua hatua. CP Hamduni amempigia simu mzee Lyimo na tayari TAKUKURU Kilimanjaro wameshafungua jalada. Hongera sana Hamduni, naamini mzee Lyimo atapata haki yake.!
HALAFU MNAMSIFIA KASSIM MAJALIWA KILA KUKICHA
 
Hakuna haja ya kumpa hongera hiyo ndio kazi yake , na bado kuna wahuni wengi sanaaaa bado wako kwenye system na kuna wengine wamestaafishwa kinyemela lakini ukweli ni kwamba wananchi wanateseka sana na waliteseka sana na utawala wa mwenda zake, mfano limtu kama Dotto bado liko kwenye mautawala you cant imagine mtu kaua kadhulumu kafilisi katishia kateka bado yupo tu, kuna libashite nalo bado linaklula bata tu kwakweli mama kuna mambo mengi sana ya kufanya japo anawaondoa kidogokidogo kama alivyotoa yule mlevi wa Mwanza, bado ana kazi kubwa sana na ngumu
 
Siyo magufuli tu Bali hata waziri mkuu naye anatakiwa kushtakiwa kwani aliripotiwa matukio ya sabaya na hakuchukua hatua zote!
Magufuli nada lakini wasaidizi wake wapo nao washitakiwe kwa kunyamaza kadhia za sabaya kwani waliyajua!
 
Hilo ndio lilikua jembe la mwendazake, mwenyewe anawaambia "chapeni kazi, hii nchi ni tajiri"
 
Sister,,kuanzia Kasim Majaliwa Pm,na hao wengine,waliogopa vibarua vyao visije kuota mchanga, maana jambazi Sabaya alikuwa anapendwa na magufuli
Hivi kweli Kiongozi unaona maovu yanafanyika,unashindwa kukemea au kuchukua hatua,eti unakaa kimya kisa kulinda kibarua chako!? Basi wwe siyo Kiongozi,bali ni Mfanyabiashara mwenye kuaangalia maslai zaidi!!
 
Napenda kutumia fursa hii kumpongeza kwa dhati Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni kwa kumpigia simu mzee Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi.

Mzee Lyimo ni mfanyabiashara ambaye aliporwa TZS 25M na aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya. Inaelezwa kuwa Sabaya alikua na desturi ya kufuatilia akaunti za wafanyabiashara wakubwa na kujua kiasi walichonacho bank.

Baada ya kufuatilia akaunti ya mzee Lyimo na kujiridhisha kuwa ana "mzigo wa kutosha" bank, alimvamia nyumbani kwake akiwa na mabaunsa, pamoja na askari polisi wa kituo cha polisi Bomang'ombe. Askari hao walibaki nje ya geti wakiwa kwenye gari. Inadaiwa Sabaya aliambatana na Juma Rahibu ambaye kwa sasa ni Meya wa Moshi.

Waliingia ndani wakiwa na mabegi mawili. Walitoa silaha na kuwaweka chini ya ulinzi familia nzima. Kisha wakamchukua mzee Lyimo na kuzungumza nae. Sabaya akamwambia "nahitaji 25M sasa hivi, ama nikukabidhi haya mabegi yawe yako"

Akafungua kumuonesha begi moja lina bangi na jingine lina mirungi. Mzee Lyimo akaona anatengenezewa kesi ya madawa ya kulevya ambayo haina dhamana. Na ukizingatia umri wake anaweza kufia gerezani. Basi akakubali kutoa kiasi hicho cha pesa.

Sabaya akaagiza polisi waliokua nje na "difenda" wamsindikize bank, ambapo alienda kutoa kiasi hicho cha pesa na kuja kumkabidhi Sabaya. Matukio yote yalirekodiwa kwenye CCTV za nyumbani kwa mzee Lyimo lakini Sabaya wala hakujali. Alijua mamlaka inayomlinda ni kubwa sana.

Hata hivyo mzee Lyimo hakuridhika na akaamua kutafuta haki yake kimyakimya. Akaenda kuripoti TAKUKURU lakini hawakumsaidia, akaripoti polisi hawakumsaidia. Baadae akamwambia Godbless E.J. Lema ambaye alilifikisha kwa Waziri mkuu lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Sasa baada ya Sabaya kukamatwa, Lema akaamua kuandika tweet ya kukumbushia haki ya mzee Lyimo. Baada ya kuona tweet hiyo mamlaka zimeanza kuchukua hatua. CP Hamduni amempigia simu mzee Lyimo na tayari TAKUKURU Kilimanjaro wameshafungua jalada. Hongera sana Hamduni, naamini mzee Lyimo atapata haki yake.!
"Polisi walimsindikiza bank akaenda kutoa sh 25M" ATM zinatoa sh 2M tu kwa siku, usiku bank zimefungwa 25M alitoaje?
 
Soma Vema Uelewe
Jambo Lilikuwa PCCB,POLICE Mpaka Kwa Waziri Mkuu
Lakini Kimya Maana Ule Mhimili Uliojichimbia Uliharibu Vyombo Vyote
Kweli bro Kwa hiyo jambazi moja tu lilituharibia nchi yetu!!! Wote wakachimbia mikia matakoni!!
 
Mimi naona Sabaya alikuwa anagawa kwa Police Takukuru na hadi kwa WM sio bure wote wawe kimya
 
Napenda kutumia fursa hii kumpongeza kwa dhati Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni kwa kumpigia simu mzee Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi.

Mzee Lyimo ni mfanyabiashara ambaye aliporwa TZS 25M na aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya. Inaelezwa kuwa Sabaya alikua na desturi ya kufuatilia akaunti za wafanyabiashara wakubwa na kujua kiasi walichonacho bank.

Baada ya kufuatilia akaunti ya mzee Lyimo na kujiridhisha kuwa ana "mzigo wa kutosha" bank, alimvamia nyumbani kwake akiwa na mabaunsa, pamoja na askari polisi wa kituo cha polisi Bomang'ombe. Askari hao walibaki nje ya geti wakiwa kwenye gari. Inadaiwa Sabaya aliambatana na Juma Rahibu ambaye kwa sasa ni Meya wa Moshi.

Waliingia ndani wakiwa na mabegi mawili. Walitoa silaha na kuwaweka chini ya ulinzi familia nzima. Kisha wakamchukua mzee Lyimo na kuzungumza nae. Sabaya akamwambia "nahitaji 25M sasa hivi, ama nikukabidhi haya mabegi yawe yako"

Akafungua kumuonesha begi moja lina bangi na jingine lina mirungi. Mzee Lyimo akaona anatengenezewa kesi ya madawa ya kulevya ambayo haina dhamana. Na ukizingatia umri wake anaweza kufia gerezani. Basi akakubali kutoa kiasi hicho cha pesa.

Sabaya akaagiza polisi waliokua nje na "difenda" wamsindikize bank, ambapo alienda kutoa kiasi hicho cha pesa na kuja kumkabidhi Sabaya. Matukio yote yalirekodiwa kwenye CCTV za nyumbani kwa mzee Lyimo lakini Sabaya wala hakujali. Alijua mamlaka inayomlinda ni kubwa sana.

Hata hivyo mzee Lyimo hakuridhika na akaamua kutafuta haki yake kimyakimya. Akaenda kuripoti TAKUKURU lakini hawakumsaidia, akaripoti polisi hawakumsaidia. Baadae akamwambia Godbless E.J. Lema ambaye alilifikisha kwa Waziri mkuu lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Sasa baada ya Sabaya kukamatwa, Lema akaamua kuandika tweet ya kukumbushia haki ya mzee Lyimo. Baada ya kuona tweet hiyo mamlaka zimeanza kuchukua hatua. CP Hamduni amempigia simu mzee Lyimo na tayari TAKUKURU Kilimanjaro wameshafungua jalada. Hongera sana Hamduni, naamini mzee Lyimo atapata haki yake.!
Hivi haya mambo ni ya kweli...?

Hivi huyu jamaa kweli alifanya yote haya anayotuhumiwa..?

Kama ndivyo, basi;

1. Huyu mtu alikuwa jambazi wala siyo kiongozi..!!

2. Huyu mtu alikuwa ni SHETANI katika sura ya BINADAMU...!!

This man deserves to be punished. He deserves to pay for his actions...
 
Huyu Dogo alikua fala sana, alikua anafanya matukio na Anaacha ushahidi
Huyu na Bashite walikuwa wana uhakika kuwa jiwe ndiye kila kitu katika hii dunia hawakujua kuwa kuna siku wataachwa yatima ndiyo maana walikuwa hawajali lolote hata hizo CCTV waliona si lolote mbele ya stone tangawizi. Utakumbuka pia kikaza bashite alipovamia Clouds badala ya kuwajibishwa akawajibishwa Nape

Sent from my TECNO P701 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom