Hongera CP Hamduni Salum kwa kumpigia simu Elioth Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi

1623924480582.png
 
Ni mapema mno kumpongeza kwani nina imani wengi wameshafikisha malalamiko yao kwake na sidhani kama wote wamepigiwa simu.
 
Hata hao kina KASESERA NA ALLY HAPI watu wa HAKI ZA BINADAMU WATANGAZIENI WALIOONEWA NA KUDHULUMIWA WAJITOKEZE MAANA NINA UHAKIKA KASESERA NI KIONGOZI MUHUNI SANA HAYO MATENDO YAO WANAYAFICHA KWA MUDA TUU SI UMEONA PEMBE LA NG'OMBE HALIFICHIKI CHALAMILA KALIONESHA NA JANA NIMEONA HAPPY NAE ANALITOA KWA MBALI
 
Napenda kutumia fursa hii kumpongeza kwa dhati Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni kwa kumpigia simu mzee Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi.

Mzee Lyimo ni mfanyabiashara ambaye aliporwa TZS 25M na aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya. Inaelezwa kuwa Sabaya alikua na desturi ya kufuatilia akaunti za wafanyabiashara wakubwa na kujua kiasi walichonacho bank.

Baada ya kufuatilia akaunti ya mzee Lyimo na kujiridhisha kuwa ana "mzigo wa kutosha" bank, alimvamia nyumbani kwake akiwa na mabaunsa, pamoja na askari polisi wa kituo cha polisi Bomang'ombe. Askari hao walibaki nje ya geti wakiwa kwenye gari. Inadaiwa Sabaya aliambatana na Juma Rahibu ambaye kwa sasa ni Meya wa Moshi.

Waliingia ndani wakiwa na mabegi mawili. Walitoa silaha na kuwaweka chini ya ulinzi familia nzima. Kisha wakamchukua mzee Lyimo na kuzungumza nae. Sabaya akamwambia "nahitaji 25M sasa hivi, ama nikukabidhi haya mabegi yawe yako"

Akafungua kumuonesha begi moja lina bangi na jingine lina mirungi. Mzee Lyimo akaona anatengenezewa kesi ya madawa ya kulevya ambayo haina dhamana. Na ukizingatia umri wake anaweza kufia gerezani. Basi akakubali kutoa kiasi hicho cha pesa.

Sabaya akaagiza polisi waliokua nje na "difenda" wamsindikize bank, ambapo alienda kutoa kiasi hicho cha pesa na kuja kumkabidhi Sabaya. Matukio yote yalirekodiwa kwenye CCTV za nyumbani kwa mzee Lyimo lakini Sabaya wala hakujali. Alijua mamlaka inayomlinda ni kubwa sana.

Hata hivyo mzee Lyimo hakuridhika na akaamua kutafuta haki yake kimyakimya. Akaenda kuripoti TAKUKURU lakini hawakumsaidia, akaripoti polisi hawakumsaidia. Baadae akamwambia Godbless E.J. Lema ambaye alilifikisha kwa Waziri mkuu lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Sasa baada ya Sabaya kukamatwa, Lema akaamua kuandika tweet ya kukumbushia haki ya mzee Lyimo. Baada ya kuona tweet hiyo mamlaka zimeanza kuchukua hatua. CP Hamduni amempigia simu mzee Lyimo na tayari TAKUKURU Kilimanjaro wameshafungua jalada. Hongera sana Hamduni, naamini mzee Lyimo atapata haki yake.

View attachment 1818470
abaya ni mwanaCCM mwenzangu. Lakini simuungimkono kwenye hizi kadhia alizowafanyia wananchi aliopaswa kuwalinda na kuwawekea mazingira bora ya kuishi kwa mujibu wa Katiba.

Kuna shughuli ya kuchangishana fedha inaendelea huko FaceBook ambapo wanaCCM wenzangu wanaendesha kampeni ya kuchangisha fedha za kusaidia kesi ya Sabaya aweze kuwekewa wakili na kadhalika.

Nasema hivii, Kila mtu ashinde mechi zake.

CCM Hoyeee
 
Napenda kutumia fursa hii kumpongeza kwa dhati Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni kwa kumpigia simu mzee Lyimo na kuagiza maafisa wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro wafungue jalada la uchunguzi.

Mzee Lyimo ni mfanyabiashara ambaye aliporwa TZS 25M na aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya. Inaelezwa kuwa Sabaya alikua na desturi ya kufuatilia akaunti za wafanyabiashara wakubwa na kujua kiasi walichonacho bank.

Baada ya kufuatilia akaunti ya mzee Lyimo na kujiridhisha kuwa ana "mzigo wa kutosha" bank, alimvamia nyumbani kwake akiwa na mabaunsa, pamoja na askari polisi wa kituo cha polisi Bomang'ombe. Askari hao walibaki nje ya geti wakiwa kwenye gari. Inadaiwa Sabaya aliambatana na Juma Rahibu ambaye kwa sasa ni Meya wa Moshi.

Waliingia ndani wakiwa na mabegi mawili. Walitoa silaha na kuwaweka chini ya ulinzi familia nzima. Kisha wakamchukua mzee Lyimo na kuzungumza nae. Sabaya akamwambia "nahitaji 25M sasa hivi, ama nikukabidhi haya mabegi yawe yako"

Akafungua kumuonesha begi moja lina bangi na jingine lina mirungi. Mzee Lyimo akaona anatengenezewa kesi ya madawa ya kulevya ambayo haina dhamana. Na ukizingatia umri wake anaweza kufia gerezani. Basi akakubali kutoa kiasi hicho cha pesa.

Sabaya akaagiza polisi waliokua nje na "difenda" wamsindikize bank, ambapo alienda kutoa kiasi hicho cha pesa na kuja kumkabidhi Sabaya. Matukio yote yalirekodiwa kwenye CCTV za nyumbani kwa mzee Lyimo lakini Sabaya wala hakujali. Alijua mamlaka inayomlinda ni kubwa sana.

Hata hivyo mzee Lyimo hakuridhika na akaamua kutafuta haki yake kimyakimya. Akaenda kuripoti TAKUKURU lakini hawakumsaidia, akaripoti polisi hawakumsaidia. Baadae akamwambia Godbless E.J. Lema ambaye alilifikisha kwa Waziri mkuu lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Sasa baada ya Sabaya kukamatwa, Lema akaamua kuandika tweet ya kukumbushia haki ya mzee Lyimo. Baada ya kuona tweet hiyo mamlaka zimeanza kuchukua hatua. CP Hamduni amempigia simu mzee Lyimo na tayari TAKUKURU Kilimanjaro wameshafungua jalada. Hongera sana Hamduni, naamini mzee Lyimo atapata haki yake.

View attachment 1818470
Je baada ya hili kubainika ni ama tulikuwa hatuna serikali ama tulikuwa na serikali ya kiharamia. Na sasa Waziri Mkuu baada ya dudu hili kuanikwa anapaswa kujiuliza je bado anastahiki kuendelea kuwepo katika nafasi hiyo au anapaswa kuomba radhi hadharani na kukemea uovu ule...?
Mwenyezi Mungu atunusuru na hawa waovu kurejea katika hizi nafasi.
Haya shime wapambe wa mtuhumiwa shikeni brashi mpambane na ushahidi wa CCTV
 
Back
Top Bottom