Hongera Diamond kwa release ya Utanipenda, umenishika Nifah!

Nifah

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2014
Posts
34,020
Reaction score
79,098
Kwanza kabisa naomba niwajuze wale wasiomfahamu nifah...
Mimi ni mkweli na mwenye msimamo mkali.
Huwa nasimamia katika kile ninachokiamini bila kuogopa wengine watapinga vipi au kunichukulia vipi.

Back to topic... Ni ukweli ulio dhahiri kuwa Diamond kafanya vizuri,na mimi kutokana na aya ya kwanza hapo juu sitaki kuwa mnafiki au kumung'unya maneno.....UMENISHIKA Diamond.
Nimependa Audio,video yaani kila kitu.
Tokea ulivyoutoa huu wimbo jumamosi nimekuwa nauangalia mara nyingi sana,na mara zote nimekuwa natikisa kichwa na kusema naam....hapa jamaa kaweza.

Ni unafiki na kuendeleza ubishani wa kipumbavu kwa kuponda vizuri kwa mwamvuli wa team, tuachane na huu ujinga na kuukubali ukweli.

Mimi kama mdau wa muziki mzuri,nasema huu wimbo wa Diamond ni mzuri sana.

#Note
Nimetoa hii post kwa mapenzi yangu mwenyewe,haina maana kwamba sasa nimekuwa team Diamond hapana,penye ukweli lazima niseme.
Sasa sitaki unafiki na kejeli kuwa nimesanda sijui na nini maana nawajua mashabiki wa Diamond vizuri tu.
Msilolijua ni kwamba nilikuwa shabiki mzuri tu Diamond, ila alikuja kunikera sehemu fulani (hata sasa simpendi ila nimeupenda wimbo wake).

Wale fans wa Kiba wenzangu bado nipo nanyi,ila tujifunze kusema ukweli.
Hata nyie majirani zetu pia....sio mnapenda wimbo lakini mnachokisema huku ni tofauti.
Period
 
Last edited by a moderator:
Hallelujah msema kwel ni mpz wa mungu
 
Amen! Mungu akupe hekima zaidi na zaidi
 
Inaonekana huu song utasumbua mwakani yaani Nana utapikuliwa na JE UTANIPENDA??
The Truth will tell us Fans of all Teams in TZ.
 
Last edited by a moderator:
Kabisa mkuu,nimeshindwa kuvumilia kwakweli.
Huu wimbo haukauki machoni mwangu,leo nitautia kwenye flash nizidi kuukosha moyo wangu.
Siuchoki kabisa.

A love ur true spirit wote tubadilike tuwe wa kwel kwenye ukwel,,, ila mwambie blaza asikae kimya Sana Na yeye
 
Inaonekana huu song utasumbua mwakani yaani Nana utapikuliwa na JE UTANIPENDA??
The Truth will tell us Fans of all Teams in TZ.
Huu wimbo ni noma,Nana haukunishtua kama huu.
Sijui ni vile napenda miziki ya taratibu?
Au sababu niko emotional na Diamond alivyolalamika kanimaliza kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Hadi nifah kashikwa!!!
Hatariiiiiiii,hatari sana.
Sipatii picha nikiusikiliza kwenye hiki kiredio changu cha mchina,maana mpaka sasa naangalia video tu niliyonayo kwenye simu na kanishika namna hii!!!!
 
A love ur true spirit wote tubadilike tuwe wa kwel kwenye ukwel,,, ila mwambie blaza asikae kimya Sana Na yeye
Asante sana.
Kwa huu wimbo kaka yetu ajipange vizuri,japo namuaminia hawezi niangusha kabisa.
Imagine angeimba yeye na ile sauti yake......uwiiiiiii!
 
Asante sana.
Kwa huu wimbo kaka yetu ajipange vizuri,japo namuaminia hawezi niangusha kabisa.
Imagine angeimba yeye na ile sauti yake......uwiiiiiii!

Tatzo mondi kwenye kulalmika tu mmmh wallah yuko vzur japokua blaza Ana saut taamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…