ESPRESSO COFFEE
JF-Expert Member
- Sep 6, 2014
- 6,170
- 7,665
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Imekuwa ni nadra sana kumuona msanii wa Kitanzania akijitokeza katika jamii na kuchangia mambo mbali mbali kwa kigezo kuwa kazi zao hazina masilahi! Hii imekuwa tofauti kwa kijana wetu mpendwa Diamond Platnumz! Amekuwa akijitokeza sana katika mambo ya kijamii na kusaidia kadri awezavyo na kadri alivyo barikiwa!!!
Kujituma katika kazi zake ni kigezo kinacho nifanya nimpende Diamond, lakini Hata moyo wake wa kujitolea na kujituma kunanifanya nizidi kumpenda Diamond! Ikumbukwe juzi juzi tuu alichangia madawati 600, alimchangia kipepeo alie kuwa anatangazwa Clouds million 5, Diamond amewasaidia vijana wengi na anazidi kuwasaidia hakika huu ni moyo wa kipekee!!!
Leo amechangia millioni 20 (20,000,000) kwa GSM foundation kwa ajili ya matibabu ya watoto wenye vinchwa vikubwa wanao fanyiwa upasuaji!! Huu ni moyo wa kipekee na si kawaida kwa Wasanii wa Kibongo kufanya hivi kwa madai kuwa kazi zao hazilipi!!! Lakini kupitia Diamond tunajifunza mengi sanaaaa na Hapa ndio Tofauti ya Diamond na wasanii wengine huonekana!
Mungu amjalie huyu kijana aongezewe pale alipo toa! Ni wakati wa wasanii wengine kuiga mfano huu
Hakika Diamond ni mfano wa kuigwa na kila msanii!