Hongera Fid Q na Ally Kiba kwa kufanya live show

Hongera Fid Q na Ally Kiba kwa kufanya live show

Deo Corleone

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2011
Posts
17,006
Reaction score
13,281
Play back zimepitwa na wakati. Jumapili Fid Q alifanya show Billz kwa kutumia band na jana Ally Kiba huko Moshi naye kafanya the same. Inavutia kushuhudia show za mtindo huo.

Wasanii wengine, nanyi fanyeni hivyo!

Si nimeeleweka?!
 
Ngoja niende insta mie najua King atakua keshatupia clips za show ya jana.
 
Live band ni hatua nyingine mbele kwenye bongo flava industry nadhani Banana na wengine wachache wanaonyesha mfano ila tatizo ni ubora wa vyombo unawaangusha ila jana Kiba alivomleta yule Paci Aloso yule wa gitaa nilimuelewa sana,nadhani wengine inabidi wajaribu live band tupate burudani.
 
Playback haiwezi pitwa na wakati,inategemea na aina ya Show unaingiza pesa ngapi. Tumeshuhudia wakina Rickross,Fat Joe,Eve,TI na wengineo wakikandamiza walivyokuja bongo. Halafu kuna aina ya mziki wa kuimba live, mi nikionaga live band za Hiphop huwa sipatagi mzuka kabisa, nataka kuisikia beat nzito ikidundwa na CD,msanii atambae na beat kavu
 
Kweli biti kavu nayo mzuka ila hata hilo halifanyiki huku kwetu
 
point!!
 
Kweli biti kavu nayo mzuka ila hata hilo halifanyiki huku kwetu

mara nyingi mi naona wanamuzik wa hip hop wakitumia band inazingua, ladha inabadilika kabisa. inabidi wapiga vyombo wajifunze kusikiliza vyombo na kuiga kila kilichopo ktk track halis

wenzetu wanaojua muziki wanaelewa ndo maana niliwahi kuuliza bongo kuna "music directors?" au tunafanya tu, wale wanasaidia kuweka mambo sawa

nyimbo kama high school ya lil wayne na yule anaconda bby inapigwa live hadi unahisi wameweka cd
 
Kupiga live ni nzuri sana,ila inategemea na hela uliyolipwa, show ni yako au umealikwa (hapa namaani labda watakiwa kuimba nyimbo 2-3 -4) huwezi chukua live band
 
Playback haiwezi pitwa na wakati,inategemea na aina ya Show unaingiza pesa ngapi. Tumeshuhudia wakina Rickross,Fat Joe,Eve,TI na wengineo wakikandamiza walivyokuja bongo. Halafu kuna aina ya mziki wa kuimba live, mi nikionaga live band za Hiphop huwa sipatagi mzuka kabisa, nataka kuisikia beat nzito ikidundwa na CD,msanii atambae na beat kavu

Ni kweli kabisa, ila mimi kwa muziki wowote ule vyombo vikipigwa live sielewi kitu bora wag0nge biti tupu kwenye cd afu mambo mengine yaendelee.
 
hongera ya nini kwani msanii kupga live ni maajabu ya dunia? wao si wametimiza wajibu wao ?
 
Ni kweli kabisa, ila mimi kwa muziki wowote ule vyombo vikipigwa live sielewi kitu bora wag0nge biti tupu kwenye cd afu mambo mengine yaendelee.
Lazima usielewe coz' kibongo bongo live performance tuko bado sana... tatizo ni vyombo na sound engineers, in short hakuna, matokeo yake mara nyingi ukishuhudia live music, unakosa ile ladha ya wimbo husika!

Mara nyingi kama sio zote muziki wetu unatokea studio ambako unakuwa computer made! Kule studio kuna lots of tricks-- vocal effects, background vocals, vyote hivi vinasimama kwenye same package!! Haya mautundu yanayofanyika studio kibongobongo huwezi kuyarudisha live halafu ukatarajia the same taste unless uwe na full orchestral; yaani wataalamu wenye uwezo wa kupiga vyombo mbalimbali na hivyo vyombo viwepo! Huwezi kulinganisha computer made guitar rhythms na live made guitar rhythms wakati hata guitar yenyewe inayotumika haina ubora! Kwahiyo ili ufanye live performance yenye same taste na studio made music ni lazima kwanza uwe na full orchestral yenye vyombo vyote muhimu... I hate to say this but kwa wasanii wetu, bado sana! Lakini pamoja na yote hayo, lazima uingize live performance-techs kama vile live software sequencers... kinyume na hapo usitarajie kupata ladha ile ile hususani kama muziki uliasisiwa na kutengenezwa studio with more than 90% computer assistance!

Lakini pamoja na yote hayo, bado kuna umuhimu wa wasanii kujifunza kupiga live ingawaje kutokana na mazingira yeyewe live music yenyewe inaweza kutuboa kuliko wanavyofanya playback! Lakini ni muhimu tu kufahamu ili pale inapotokea ulazima wa kufanya live performance wawe na uwezo wa kufanya hivyo lakini isiwe ndo fasheni yenyewe kwamba lazima wapige live coz' hata huko US kwenye kila kitu bado wanapiga show kwa kutumia CD!
 
Live performance sio kitu kidogo. Sio kuwa na ngoma zako zilizotoboka na gitaa lililokatika nyuzi na wapigaji waliofundishwa na kukulia kwenye dansi utaishia kuwaibia watu.

Kwa Africa hapa wakali wa live performance za band huu muziki wa kizazi kipya ni P2 na yote ni sababu vifaa vyao ni vya kisasa ngoma,guitars, matalumbeta na vikorokoro vyote ni vya umeme.

Sielewi mtu anainjoi nini kusikiliza rnb inayosaund kama bolingo, na bado sijaona watu wakupiga beat ya Majani au Pancho kwenye live band hapa bongo na ukafeel.

Live band kibongobongo labda Jazz, rhumba chakacha na mitindo hiyo wanajaribu.
 
Playback haiwezi pitwa na wakati,inategemea na aina ya Show unaingiza pesa ngapi. Tumeshuhudia wakina Rickross,Fat Joe,Eve,TI na wengineo wakikandamiza walivyokuja bongo. Halafu kuna aina ya mziki wa kuimba live, mi nikionaga live band za Hiphop huwa sipatagi mzuka kabisa, nataka kuisikia beat nzito ikidundwa na CD,msanii atambae na beat kavu

sikiliza kitu cha rock boys cha jay z...lazima upate mzuka...

''look on how I'm chillin I'm killin this ice.''
 
Last edited by a moderator:
sikiliza kitu cha rock boys cha jay z...lazima upate mzuka...

''look on how I'm chillin I'm killin this ice.''

Huyo ni exceptional Tyta , pia Nas na Eminem wanapiga live nzuri sana, but wengi wanaharibu
 
Last edited by a moderator:
Huyo ni exceptional Tyta , pia Nas na Eminem wanapiga live nzuri sana, but wengi wanaharibu

ni kweli,,,japo namkubali Rick Rozay,linapokuja suala la on stage performance,ni aibu,kama vile kaishiwa pumzi...
 
Back
Top Bottom