sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,344
- 9,066
Anaandika Jokate kupitia twitter.
"UWT kwa kutambua waathirika wakubwa wa majanga kama haya ni akina mama na watoto, leo tumefanya kikao cha dharula na kuanza zoezi la kutafuta vifaa vya kuwasaidia wakina mama na watoto walioathirika na maafa Hanang, Manyara.
"Kwa siku ya leo tumeanza na kuweza ku-mobilize kutoka kwenye mfuko wetu na marafiki zetu;
- Magodoro mapya 200
- Pair za khanga mpya 1000
- Madera mapya 520
- Mashuka mapya 400
- Mablanketi mapya 150
- Mikeka mipya
- Vikoi vya kujifunika, sabuni, mafuta, nguo za watoto, vyombo vya kulia na kupikia nk.
"Tunawakaribisha watakaoguswa kuleta michango ya vifaa kwenye ofisi zetu."
Hongera sana kwa kuwashika mkono ndugu zetu awa wakati huu ambao hata kipande cha sabuni kinawafaa sana.
Katesh watakukumbuka maisha yao yote, akufaae kwa dhiki ndio rafiki wa kweli.