Hongera JWTZ kwa kumiliki Humvee

gari la kawaida tu na halina maajabu yoyote na ukizingatia na uhalisia kuwa kwetu matumizi yake ni madogo kuliko vile tunadhani ni bora tujikite utengenezaji wa silaha zetu
 
Dah!kweli bado tupo nyuma,yani ukiangalia gari ambazo wanajeshi wa south Afrika wanatembelea mjini,hakika ni mara kumi zaidi ya hizi.
 
naam
 
Hiyo picha ya juu siyo humvee ila ni mRAP.Humvee ni hiyo ya chini.
 
Mbona miguu yake ni ya mpira sasa? Risasi moja pancha
 
Wata niruhusu kulitumia hapa bongo ni kuli sajili! Vip bei yake mkuu! Nina bajeti ya 200m
Usihofu nitakusimamia,mimi ni mtu mkubwa ndani ya system,kesho andaa milioni 5 nitakupa namba uingize kwa ajili ya kuprocess vibali..
 
Usihofu nitakusimamia,mimi ni mtu mkubwa ndani ya system,kesho andaa milioni 5 nitakupa namba uingize kwa ajili ya kuprocess vibali..
Poa mkuu ila system isije poteza mpunga wangu chonde chonde!!
 
Tatizo la bongo hata hiyo humvee nayo ya uchina kama ndege vita zetu
Tumejitaidi kwenye helicopter za mfaransa.et hatupendi show off tunapenda sana sema vitu vya mchina.
 
Sisi tunajisifia kwa kumiliki kagari kamoja wakati wenzetu wanapimana ubavu kwa kumiliki mitambo heavy ya kulinda anga + makombora ya masafa marefu achilia mbali drones!

Kweli safari yetu bado ndefu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…