Hongera Kenya , Hongereni wakenya , Nakulilia Tanzania

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Naangalia game ya Timu ya Gor-Mahia ya Kenya dhidi ya Timu kali ya Everton kutoka Uingereza kupitia EATV hapa kwenye uwanja wa maonesho wa sabasaba , Hakika mna kila sababu ya kutembea kifua mbele .

Timu yenu ni nzuri na kiukweli inastahili kuiwakilisha East Africa kwenye game hii , hongereni sana wakenya .

Huku kwetu Tanzania mpira unachezwa zaidi na viongozi , ndani ya uwanja , nje ya uwanja na mahakamani , kwetu kununua mechi ni jambo la kawaida sana ! Waamuzi kununuliwa siyo siri tena .

Soka la Tanzania limedumaa mithili ya MTOTO ALIYEBEMENDWA ! hivi ninavyoandika haya viongozi wa TFF wako mahakamani kwa sababu zinazofahamika kama FITNA ZA UCHAGUZI ! Yaani viongozi wa soka wanapangwa kutoka nje ya soka lenyewe , aibu sana !

Wakenya endelea kuongoza , sisi tutaendelea kuburuza mkia .
 


Mtoto mrembo hujambo?, Mashaalah!
 
TZ mpira ulikufa toka miaka ya 1970 kilichobaki ni ubishi na mazoea tu. We umeona wapi mtu kama Mze Akilimali asiye na mchango wowote ndani ya timu eti anaogopewa na kama abugiii ugoro basi timu haiendi kucheza.
 
Simba na yanga na azam wapz sana wangekaza wangecheza na everton team zetu zingejengeka Kwa jina duniani .....
OvA
 
Reactions: MC7
Weka matokeo acha kelele

Sent from my Lenovo A2010-a using JamiiForums mobile app
 
TZ mpira ulikufa toka miaka ya 1970 kilichobaki ni ubishi na mazoea tu. We umeona wapi mtu kama Mze Akilimali asiye na mchango wowote ndani ya timu eti anaogopewa na kama abugiii ugoro basi timu haiendi kucheza.
Nimecheka sana !

Huku simba kuna mtu aliitwa Bamchawi , Full vitisho vya uchawi !
 

.....Siyo tu kwamba huku kwetu tunanunua mechi, waamuzi na hata washangiliaji pia siku hizi tunanunua hata Madiwani!!
 
Simba na yanga na azam wapz sana wangekaza wangecheza na everton team zetu zingejengeka Kwa jina duniani .....
OvA
Alafu tumechukulia haya mashindano ya sportpesa poa, ila kwa mfano simba ndo tungekomaa au haya yanga ikashinda na kucheza na everton, imgekuwa ni silaha moja kubwa sana ya kumtania mtani wako kuwa sisi tulicheza na everton, nyie je! Ila upuuzi wa kuchukulia mambo poa yametuponza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…