Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Karibuni karne ya 21, wenzenu bado tuko zama za mawe!
Yaliyojiri...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewataka radhi wote aliowakosea na kumtaka naibu rais William Ruto pia kufanya hivyo ambapo Ruto alikumbatiana na Kalonzo Musyoka pamoja na Raila Odinga.
Naye kinara wa chama kikuu cha Upinzani, ODM, Raila Odinga amewaomba radhi rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kufuatia kutoelewana haswa wakati wa siasa za uchaguzi uliopita.
Kwa upande mwingine naibu rais William na Kalonzo Musyoka nao wameombana msamaha na kuahidi kuweka tofauti zao kando. Haya yamejiri kwenye maombi ya 16 ya kuliombea taifa yalio andaliwa jijini Nairobi.
Viongozi wote hao wanne wameahidi kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kushikana katika kuendeleza taifa lao na kuwaunganisha Wakenya. Hongereni sana Wakenya kwa kuona mwanga na kufungua ukurasa mpya!