Kwa kuwa umasikini wa lugha umekuganda kama shati lililoloa, nakupa tafsiri ya kilichofanyika nchini Kenya...
Alhamisi tarehe 31/5/2018: Mapema leo asubuhi wakati wa Sara ya Kitaifa jijini Nairobi, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amemuomba msamaha muhasimu wake Raila Odinga na kutaka tofauti zao za kisiasa walizokuwa nazo kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa Kenya ziweze kuisha na waijenge nchi yao. Naye Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto amefanya hivyo hivyo kwa Kalonzo Musyoka.
Sisi hapa Tanzania tumefuzu katika kuupa msogo ustaarabu, tunawindana kama wanyama wa mwituni...
Utakuwa na matatizo Bure ,ya kuzaliwa au ya kurithi
Humu ndani ,unajua nafahamu lugha ngapi? Unajua nafahamu vitu vingapi?
Umeona hiyo ya sasa toka mchakato wa *Handshake* umeanza Kenya ,hii ndio umeona kwako ni cha kujifunza
Hujui lolote kuhusu siasa za Kenya na Tanzania haina ya kujifunza Kenya , unaongea sababu ya kudanganywa kwenye media lakini Mimi naweza kushusha nondo za field kuhusu Kenya unayoina kwenye media na Kenya halisi
Narudia hujui lolote kuhusu Kenya , hujui lolote kuhusu Handshake ya Kenya ,hujui lolote internal strife , ya serikalini nchini Kenya , hujui lolote kuhusu kinachofanya kila Mara Uhuru na odinga iwepo handshake Ili Ku ceasefire , hujui lolote kuhusu Kenya na count zake ,
Unachojua ni kulishwa mambo ya kwenye media
Sisi tunajua mambo ya ndani ya Kenya na tunajua kwa nini Kenyatta na Uhuru wanaonesha kupatana
Na huelewi maana ya hii kauli ya Uhuru kuwa *Naomba kaka yangu Raila unisamehe kwa yote yaliyotokea* hii kauli huwezi jua maana yake
Nakushauri endelea kuandika andika na kujifanya unajua kumbe hujui lolote na pia hicho kiingereza chako kibovu kawatafsirie kijijini kwenu , na usifikiri humu jukwaani watu wanafaham lugha moja au mbili kama wewe