Hongera Kenya(Kenyatta na Odinga) kwa kuuona mwanga na kufungua ukurasa mpya!

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,413
Reaction score
23,592
Karibuni karne ya 21, wenzenu bado tuko zama za mawe!

Yaliyojiri...
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewataka radhi wote aliowakosea na kumtaka naibu rais William Ruto pia kufanya hivyo ambapo Ruto alikumbatiana na Kalonzo Musyoka pamoja na Raila Odinga.

Naye kinara wa chama kikuu cha Upinzani, ODM, Raila Odinga amewaomba radhi rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kufuatia kutoelewana haswa wakati wa siasa za uchaguzi uliopita.


Kwa upande mwingine naibu rais William na Kalonzo Musyoka nao wameombana msamaha na kuahidi kuweka tofauti zao kando. Haya yamejiri kwenye maombi ya 16 ya kuliombea taifa yalio andaliwa jijini Nairobi.

Viongozi wote hao wanne wameahidi kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kushikana katika kuendeleza taifa lao na kuwaunganisha Wakenya. Hongereni sana Wakenya kwa kuona mwanga na kufungua ukurasa mpya!
 
Alianza mamvi kwenda ikulu we bwege. Raila anafuata nyayo.
Haya ya Kenya yalifanyika hadharani yakishuhudiwa na wananchi wote wa Kenya.
 
Acha kupotosha...Lengo la UHURU NA RAILA kukutana hapo HALIPO KISIASA KABSA bali hapo wamekutana kwenye siku maalumu nchini kwao ya KULIOMBEA TAIFA ambayo huwa inaandaliwa na BUNGE LA KENYA...
Ungeonekana wa maana na thread yako kama LENGO KUU LA UHURU NA RAILA LINGEKUWA NI HILO LA KUSAHAU NA KUSAMEHANA KAMA THREAD YAKO inavyojieleza...
 
Huku kwetu wanagoma kuoeana mikono kusalimiana [emoji848][emoji848]
 
Alianza mamvi kwenda ikulu we bwege. Raila anafuata nyayo.
Kwenda ni upande mmoja na matendo ni upande mwingine, wewe unaona kwenda kwa lowassa ikulu kumebadilisha chochote si ndio rais anazidi kuubinya upinzani?
 
Mwambieni MAMVI arudi tena na media ziwepo.
Usiwe mpumbavu, rudi porini ulikotoka. Binadamu tulipewa akili na si kama wanyama wa porini!
 
Tatizo lugha, bila shaka umetoka kapa na Kiingereza chako cha fenti ford...pole sana! Tafuta mtu akutafsiriye kinachoongelewa kwenye video.
 
UHURU anafata nyayo za JAKAYA

IPO SIKU HUYU UHARU ATACHKUWA TAJI LA BEST PRESIDENT IN AFRICA
 
Wacha kejeli kisa mmetofautiana mtazamo na hoja....Kwaiyo ulileta mada ili watu wote wawe upande wako( wakuunge mkono) mkuu?

 
Tatizo lako inaweza kuwa lugha au ujinga,

"I ask for your forgiveness and I tender my apology", President Uhuru tells Raila and all Kenyans.

Rais Jiwe anaweza kujishusha hivyo na kusema hivyo mbele ya watanzania?
 
Haya ya Kenya yalifanyika hadharani yakishuhudiwa na wananchi wote wa Kenya.
Kwa maana hiyo kumbe hamumuamini lowassa akiingia ikulu mpaka atoke hadharani na JPM ndio mnapata Amani?

Sasa ilikuaje mkamuamini ghafla na kumpa heshima ya kugombea urais kama tu hamna imani nae kiasi hiki?
 
Kwahyo wewe peke yako ndio umeelewa sisi wengine vilaza hata kusikia hatusikii ama vipi??
Acheni siasa za ujima,mnafanya mambo kama uncivilised people's. Your at stone age
 
Tatizo lako lugha au ujinga, "I ask for your forgiveness and I tender my apology". Uhuru tells Raila, Rais Jiwe anaweza kusema hayo mbele ya watanzania?
Usiwategemee hao mabinamu wa jiwe kuelewa kinachoongelewa kwenye hizo video. Lugha ndio tatizo.
 
Kwenda ni upande mmoja na matendo ni upande mwingine, wewe unaona kwenda kwa lowassa ikulu kumebadilisha chochote si ndio rais anazidi kuubinya upinzani?
Acha kumsingizia Rais mambo ya uongo nyie ni wananchi wanawanyuka bakora JPM yupo busy na mambo yake

Tumeona mkinyukwa kwenye zile Kata kwenye Kata zaidi ya 15 mliambulia moja, Tumeona mkinyukwa kwenye maandamano yenu uchwara mpaka yule dada mnaemuita professor kapata stroke watanzania walivyompuuza, hayupo tena mitandaoni

Sasa 2020 ndio mtatafutana
 
Nimemsingizia nini we pimbi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…