Hongera Kenya kwa kufuzu AFCON; Tanzania na Mtego wa Sierra Leone

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2015
Posts
26,021
Reaction score
79,710
Baada ya FIFA kuifungia nchi ya Sierra Leone kutokushiriki mashindano yoyote yanayosimamiwa na bodi hiyo ya soka duniania, shirikisho la mpira wa miguu Afrika, CAF limeipiga chini Siera Leone katika mechi za hatua ya makundi za kufuzu kwenda AFCON kutokana na serikali kuingilia masuala ya soka jambo ambalo ni kinyume na sheria na taratibu za FIFA.

Kenya inayoongoza Kundi F imejikusanyia point 7 huku ikifuatiwa kwa karibu na Ghana yenye point 6 na Ethiopia yenye point 1. Kufuatia kuenguliwa kwa Siera Leone kumeipa Kenya tiketi ya moja kwa moja na wataungana na wenzetu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, Uganda ambao tayari wameshafuzu.

Lengo la uzi huu ni kuikumbusha 'sirikali' kuwa mambo ya siasa hayana nafasi kwenye soka la sivyo rungu la FIFA litatushukia na kutupasua vipande vipande.

Baada ya Taifa Stars kufungwa na Lesotho kuna kauli za viongozi wa 'sirikali' zilizokuwa na utata kuhusiana na kufuzu kwa timu yetu ya taifa kwenda AFCON.

Nashauri sirikali isifanye jambo lolote litakalokuwa nje ya sheria za FIFA kwakuwa tutaharibu zaidi. Tucheze na Uganda na kama tukishinda tushinde kispoti au kufungwa kispoti. Nje ya hapo itakuwa ni majanga kwetu.

Nashauri mapema kwakuwa viongozi wa hii awamu wana maamuzi ya kustaajabisha sio ajabu ukashangaa matamko yasiyoeleweka na kutendeka mambo ambayo yatachafua ramani ya soka hapa nchini.

Nawasilisha.
 
Sisi tutabaki na kufungiana tu,hakuna safari na hatuna timu ya kumfunga Uganda labda watuonee huruma tu
 
Yaani tumefungwa na timu ya Wasambaa wa Lushoto, ndio tutawaweza the Cranes? Haya tusubiri muujiza wa football tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…