Hongera Kenya kwa kutinga hatua ya robo fainali ya CHAN

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,476
Wote tuliguna pale makundi ya CHAN yalivyotangazwa. Kenya alipangwa kundi ambalo tulidhani asingetoboa ila mwisho wa siku ameshinda mechi mbili akiwa anacheza pungufu na kamaliza hatua ya mwanzo kwa kuongoza kundi. Kenya wanacheza pia kiufundi. Hawachezi tu jihadi, unaona kabisa wanacheza kitimu.

Huko majukwaani, mashabiki wao wanajaza viwanja. Kuna maneno huko yanasambaa kwa nini wao wanaenda viwanjani halafu sisi hatuendi. Bila kumung'unya maneno, sababu kubwa ni kwamba Wakenya wameshatoa madukuduku yao ya moyoni na mioyo yao ni myepesi kwa taifa lao. Kwa upande wa Watanzania, mioyo yao ni mizito na imebeba mengi na hakuna anayetaka kuwasikia, wala kuwapa nafasi ya kuyatoa.

Kama mnataka Watanzania waonyeshe shauku katika michezo kwa jinsi mnavyotaka, wapeni fursa watoe yao ya moyoni bila kubughudhiwa, kutishwa wala kudhuriwa. Siyo hivyo tu, wasikilizeni na yale wanayotaka yatekelezwe. Siasa za kishamba tuachane nazo.
 
Mwachieni Lissu,period!!
 
Back
Top Bottom