Hongera Kenya kwa mrejesho wa kazi za Infrastructure

 
 
 
Siyo kweli Tobaa, nimevutiwa na ule mrejesho wa hao watu kuhusu kazi wanazozisimamia na kuzitekeleza. Mimi siyo mtu wa Local News tu, huwa pia natembelea ulimwengu kwa njia ya media zinazopatikana kwenye vingamuzi ninavyomiiliki. Nini habari za Kenya wewe, watu wanashabikia za Marekani leo hii ukiuliza kuhusu Trump na Mrs Clinton wanawajua kuna ubaya gani kujua habari za nchi nyingine ikiwa dunia sasa ni kijiji? Nchi yangu naipenda, naijua kuliko unavyodhani, nitafia hapa ila kama kuna mazuri yanafanywa kwingine ningependa tuyaige ili tuzidi kuendelea.
 
ahsante kwa kuwa mkweli katika hili.....

hakuna kitu kizuri kama kuijua vyema nyumba ya kwenu kabla ya kuanza kulinganisha na nyumba nyinginezo kwa uzuri....

ukiongelea miradi ya miundombinu aliyoifanya Kikwete nchini utaogopa lakini kwa kuwa haina publicity itakuwa ni unknown kwako.

HATA KAMA HUFUATILII HABARI ZA NCHINI PAKO LAKINI JARIBU KUTEMBELEA MAENEO MBALIMBALI NCHINI ILI UJUE HATUA ZA KIMAENDELEO ZILIZOPO....

sintoongea zaidi kwa kuwa tupo nje ya mada husika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…