Hongera Kidunda Ila Umetuaibisha Kwenye Wimbo wa Taifa

ule wimbo Jana ulipigwa kwa vyombo na sio sauti ni ngumu kujua Kama umeisha au la
Na baada ya kumaliza ubeti wa kwanza ni Kama kuna kimya kikatokea alafu ndo wimbo ukaendelea.
Na vile alikuwa na presha.
Sidhani Kama ni ISHU KUBWA.
Kikubwa katompa kachezea ngumi za kutosha.kutoka round ya 1 mpaka ya 5
 
Mkuu Safi nimekubali uchambuzi wako. sina vingi huku kwenye masumbwi uwanja wangu Futiboli kule ila Safi umeeleza vizuri nimekuelewa.
 
Mkuu Safi nimekubali uchambuzi wako. sina vingi huku kwenye masumbwi uwanja wangu Futiboli kule ila Safi umeeleza vizuri nimekuelewa.
Yes yes no body knows everything but anybody can learn something, hata mimi football siyo sana kama masumbwi nadhani ni mapenzi niliyo nayo tangu nipo standard 5 nilijifunza kwa mapenzi sana nadhani isingekuwa juhudi za mzazi wangu na kwenda shule ningekuwa bondia mana hata shule nilosoma kulikuwa na mabondia wengi na wengine ni wakubwa tu kwa sasa though sijaacha mazoezi mpaka sasa tena hata marafiki nilonao ni wengi hawa hawa mabondia ts passion to me.
 
Huu wimbo wetu umeshawaaibisha watu wengi sana kama kiduku,Mbabe na wengine ila jana nimeshangaa sana mpaka mwanajeshi wakati kila siku wanauimba kambini huko na wakiona bendera ya taifa wanajifanya kupandisha midadi

Ila sikutegemea kama Kidunda angempiga Katompa,kumbe kidunda yupo vizur
 
mchizi wetu alituhaibisha kwa kweli,ila refarii naye mzushi asingesimamisha pambano

Bora Refa alivyomaliza pambano, vingnevyo Mandonga angebebwa na machela maana alishaanza kuona nyota nyota baada ya kupigwa jab mbili zilizompeleka chini mara mbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…