Rorscharch
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 878
- 2,014
Niwe muwazi, Tangu viongozi mbalimbali CHADEMA walivyoanza kukiri kwamba bila katiba mpya hawawezi kuchukua uongozi wa nchi kusema kweli imani yangu na mapenzi yangu kwa chama hichi imeporomoka sana maana nilikua najiuliza kichwani .... "Miaka yote hii wana "front" mgombea urais walikuwa wanatuigizia wanachi au ?"
Ndani ya miaka hii miwili mitatu nikajiweka mbali kabisa na ufuatiliaji wa siasa za nchi hii, sio tu kwasababu nilikua disappointed bali pia ilinibidi nipanue mitazamo yangu kwa kufocus kidogo katika mifumo ya siasa za kimataifa na kusema kweli imeisaidia sana kuelewa kinachoendelea nchini hapa kwenye nyanja ya siasa zetu na maeneo mengine pia, yafuatayo ndio niliyojifunza kwa ufupi:
1. Kwa asilimia kubwa upinzani sio mbadala wa chama tawala bali ni backup inayoguarantee muendelezo wa tamaduni za kiuongozi zilizopo, chama tawala kikipoteza influence basi system ile ile iliyopo hutumia upinzani kama jahazi la kujiokoa (umewahi kujiuliza katika nchi zote za Afrika ambazo upinzani umefanikiwa kuangusha vyama tawala kongwe nini tofauti kimefanyika kama sio kuendeleza sera zile zile kwa asilimia kubwa )
2. Nchi nyingi dhana ya Uhuru (sovereignty/autonomy/independence) ni geresha maana ukoloni umebadilika kutoka mabavu kwenda kwenye diplomasia ya misaada ya vipengele vya kiuchumi; hivyo watanzania wenzangu kaeni mkijua kwamba tutatifuana ndanindani CHADEMA, ACT, CCM na ukurutu mwingine lakini atakayetokea mshindi kwenye kinyang'anyiro hicho atakaa kwenye "mifumo" ile ile "inayokubalika" kimataifa; mabenki yataendelea kuchochea mfumuko wa gharama kwa maelekezo kutoka world bank, tutaendelea na geresha za kisiasa kama kawaida (wapinzani watabadilika kuwa watesi na wezi) na kadhalika na kadhalika
Funzo kwa CHADEMA na wanachama wake
Ili chama kiwe "exceptional" inabidi kifanye kazi na kujipambanua kwenye macho ya watanzania kwa njia tofauti. Kura zisitafutwe kwa propaganda za kuikosoa CCM kwa mambo ambayo hata CHADEMA yenyewe ikiingia itayafanya (rekodi za vyama pinzani vilivyochukua nchi barani hapa tunazo), bali kura zitafutwe kwa kujenga mahusiano mapya katika nyanja mbalimbali na wananchi ambao ndio wapiga kura wenyewe; imani kwamba kinaweza kuongoza inabidi ianze kujengwa kabla hata madaraka yenyewe hajakabidhiwa
Vijana wana changamoto ya ajira
Barabara ni mbovu na haitengenezwi na gari zetu zinaharibika
...na kadhalika na kadhalika
Kwa scenario kama hizo hapo juu chama kiwe na mikakati madhubuti inayotekelezeka ambayo inaweza kufanywa na jamii yenyewe bila mkono kutoka serikalini (Wachagga wanarekebisha barabara za vijijini kwao wakahesabiwe vizuri)
Badala ya kuendekeza kizazi cha betting imagine chama kikaja na hata vikoba vya kilimo kwa wakazi wa mijini, kutoa support kwa vijana wenye ujuzi wa kuandaa maombi ya pesa za miradi ya kimataifa na nyanja nyingine mbalimbali
Ndugu zangu, uhusiano wa wananchi na upinzani kwa sasa hauna tofauti na ushabiki wa Simba na Yanga, inabidi chama kioneshe umuhimu kwenye maisha ya watanzania kabla hata hakijakabidhiwa mikoba ya uongozi