Hongera kwa tuliohusika kwenye Dar heart marathon.....halafu Arusha mpo juu

Hongera kwa tuliohusika kwenye Dar heart marathon.....halafu Arusha mpo juu

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Hii hafla ya 'Heart run' imekua ikitangazwa humu na JF, nawapa hongera tuliohusika sote jana ikiwemo baadhi yetu Wakenya tuliosafiri hadi Dar ili kuhusika ukizingatia sio wanariadha ni utashi tu, nawapa pia hongera waandalizi japo natoa wito wawe makini kwa suala la muda, kama imepangwa tunakimbia kuanzia 6am, iwe kweli, sio muda unasonga watu hatujui kulikoni ukizingatia joto na jua la Dar huwa balaa, kupasua kwenye hilo joto kilomita 21 sio mchezo.

Kwa yote, shukrani maana ni jambo nzuri sana tunapokusanyika hivi kwa ajili ya kusaidia watoto wenye matatizo ya moyo, halafu duh kuna makundi ya kutoka Arusha yanakimbia Kikenya aisei, hongera yenu mkiendelea hivyo ipo siku mtasikika.

My Strava time -
  • 21.32km

  • 2:25:26
    Moving Time
  • 6:49/km
 
Mshindi wa 1 anapata sh ngapi?
Watanzania bana, hii ni charity hivyo hatukuenda kushindana, kila mmoja alilipia 30,000Tsh japo ni kweli namba moja hadi tatu huwa wanapewa zawadi.
 
Back
Top Bottom