Wale wawili, kwa sababu walikuwa jikoni, wakijua uharamia ambao ulikuwa ukipangwa dhidi ya wananzengo, mapema kabisa waliamua kujiweka mbali. Makamu aliamua kuachia ngazi. Kiranja wa mawaziri licha ya kutangaza kuwa angegombea tena, baada ya kujua kilichokuwa kikipangwa, aliamua kujiweka mbali. Huyu wa sasa alichelewa, akidhani yasingetokea yaliyokuwa yamepangwa dhidi ya haki za wananzengo.
Yalipotokea matukio yale ya mauaji ya halaiki, na wauaji kujipachika madarakani, wakati wote yeye ilionekana kutokuwa na amani moyoni mwake. Na leo ameamua kuachana na ukuu uliopatikana kwa kumwaga damu za wanadamu wenzake.
Katika uhalisia hakuna mtu ambaye yumo ndani ya utawala wa wauaji anayeweza kuaminika na yeyote mwenye akili timamu, anapotoa kauli yoyote ya kuonesha anajali uhai wa binadamu na haki za binadamu wenzake. Ndiyo maana hata huyu bwana akiwa pamoja na wauaji, hata pale alipotamka umuhimu wa masuala ya haki na umuhimu wa katiba mpya, hakuna aliyemwamini.
Wananzengo kwa sasa wanajua kuwa mdhulumaji mkuu wa haki zao ni kundi la watawala madhulumati, halafu umo ndani ya madhulumati unajifanya ni mpenda haki! wenye akili wote watajua kuwa ni hadaa. Sasa huyu amejitenga na wadhulumu haki, na kuthibitisha kuwa alichokuwa akikisema, alimaanisha, haikuwa hadaa.
USHAURI.
Wale wote waliopo ndani ya kundi wabeba madaraka kwa nguvu, lakini wao binafsi, dhamira zao hazikubaliani na vitendo vya kuwaua, kuwateka na udhulumati wa haki dhidi ya binadamu wenzao, ni muhimu wote wakatoka na kujitenga na wauaji, ili ndani ya utawala wa mauaji wabakie madhulumati wa haki pekee. Na wananchi wakiwaona hao walio ndani ya utawala wa wauaji, wajue kwa uwazi bila shaka kuwa hawa ndiyo wauaji na madhulumati wa haki zao.
Tamaa ya madaraka na utajiri, visitufanye kuwa viziwi na vipofu wa dhamira zetu. Mtu yeyote mwenye dhamira iliyo hai kamwe hawezi kuungana wala kukaribiana na wauaji. Vyeo na utajiri ni vitu vya kupita. Ubinadamu wetu unatakiwa kuwa juu ya vitu vyote. Hatutakiwi kuwa wafu wa dhamira, hata tukashindwa kujua kuwa juu yetu na juu ya vyote, kuna mkuu zaidi ya chochote, ambaye ni Mungu aliyetuumba.
Shetani hutumia sana tamaa ya madaraka na utajiri kama kishawishi kikubwa cha kumtenga mwanadamu na Mungu ili mwisho wa yote, mwanadamu apate kuangamia