Hongera Lionel Messi lapulga

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Baada ya Messi kufunga goal 2 leo dhidi ya Espanyol. Na Barcelona kuibuka na ushindi wa goal 2-0. Hatimaye Messi amefikisha goal 31 na assist 12 .Hii ni ktk mechi 27 tu alizocheza Kwenye Laliga. Bado mechi 9 ligi kuu ya Hispania imalizike..Kwa sasa messi ndiye mfungaji bora wa Laliga na mfungaji bora kwa zile ligi 5 bora za bara la Ulaya.

Ktk michuano yote msimu huu mpaka sasa, Messi ameichezea Barcelona mechi 38 kaifungia goal 41, nakatoa pasi za mwisho assists 18.

Kwa messi huu ni msimu wa 10 mfululizo. Ktk michuano yote Anaifungia Barcelona goal 40+ kwa kila msimu..Hii Shughuli ya kuizawadia Barcelona magoal 40+ kwa kila msimu. Lionel Messi aliianza kuanzia msimu wa 2009/2010. Hadi leo msimu wa 2018/2019 bado anaifanya.

Msimu bora kwa Lionel Messi ktk maisha yake, ulikuwa msimu wa 2012. Messi aliweka record 3 za kutisha. Record ambazo mtu yoyote akiambiwa Messi sio kiumbe wa sayari hii lazima asadiki.

Record ya kwanza ilikuwa ni kwenye uefa champions league. Alifunga goal 5 peke yake ktk mechi moja. Goal 5 bila penalty. Ilikuwa mechi ya mtoano dhidi ya Bayerleverkusen. Kufunga goal 5 Ktk mechi 1. Mpaka sasa hakuna mtu aliyefanya hivyo Kwenye usiku wa ulaya. Isipokuwa tu Lionel Andres Messi lapulga.

Record ya pili aliiweka ktk ligi kuu ya Hispania Laliga. Messi alichukua kiatu cha ufungaji bora. Baada ya kufunga GOAL 50 Ktk mechi 38 tu. Hii ni record inayoogopesha mno.

Record ya tatu ilikuwa record ya dunia. Messi alifunga goal 91 ktk michuano yote aliyocheza akiwa Barcelona na timu ya Taifa Argentina .. Alifunga goal 91ndani ya mwaka mmoja tu. Hii records ni uthibitisho wa mwisho kuwa, huenda Lionel Messi alikuja ndani ya hii sayari kwa bahati mbaya.

Ashukuriwe Mungu wetu juu aliyetuwezesha tukakiona kiumbe hiki.



'When you’ve been an Arsenal fan as a kid, you will be one your whole life in some way.” David Alaba
 
At least you differed with most punteorist fans who whenever they talk of Messi they must compare with Ronaldo as if they are two sides of a coin. You are definitely unbiased fella!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo akili za arsenal fans sishangai
Kuna mtu anaenda kubeba ligi kwnye nchi sjui ya ngapi tofauti,hatihati pia kubeba uefa sjui kwny nchi ya ngapi tofauti,
Shupaza shingo tu,uefa na scuddeto znaweza zkawashangaza watu kwny tuzo

Sent using Brain
 
Umeeleza vizuri kabisa,

Lakini hapo uliposema amefikisha goli 31 katika mechi 27 na zilizobaki ni 9 ligi imalizike bado sijaelewa,

Kama zilizochezwa ni 27 basi zilizosalia nilitaraji ziwe 11 au ligi siku hizi inazo timu 18......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hayo maajabu ayahamishie timu ya taifa. mchezaji mwoga kuhama timu huku akiogopa rangi yake kuonekana. wanaume wamecheza ligi tofauti tofauti na bado wanang'ara
 
hayo maajabu ayahamishie timu ya taifa. mchezaji mwoga kuhama timu huku akiogopa rangi yake kuonekana. wanaume wamecheza ligi tofauti tofauti na bado wanang'ara

Hoja dhaifu sana kuwahi kutokea👆

Umejuaje akihama hatong'ara? Kama akina pogba,hazard,mbape,mohamed salah,kane na Aguero wameweza, Messi ashindwe nini! Wakati hao hao alikutananao na akawafunga,huko ujerumani, ufaransa na italia pia hivyo hivyo kawakung'uta....

Sasa unataka ahame aende tim ipi? Kama mahitaji Barca inamtimizia yote ayatakayo, sasa unataka aende wapi?

Sometimes muwe mnafikiria cha kukomenti mkuu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…