Ni kweli Mheshimiwa Lukuvi,amejitahidi kuchapa kazi wizara ya Ardhi.
-Lakini Kwa kipindi chote ambacho Lukuvi amekaa wizara ya Ardhi,ameshindwa kuajiri maafisa ardhi na wapimaji wa ardhi wa kutosha,ili kukomesha ujenzi holela ,
-wizara imetoa vibali kwa taasisi binafsi (ambazo nyingi ni kampuni za makamishina au wakuu wa idara za ardhi) kupima ardhi kwa gharama kubwa.
-Kampuni nyingi za urasimishaji makazi ni za wakubwa hao.
Ushauri kwa Waziri Mabula na Riziwani
- Ni kuhakikisha kuwa wizara ya Ardhi inaajiri maafisa wa ardhi na wapimaji wa ardhi na mipango miji wa kutosha kwenye halmashauri za wilaya zote.
-wizara inapima viwanja vya kutosha,ili watu wajenge kwenye viwanja vilivyopimwa.
-wizara inaweka mfumo mzuri wa kugawa viwanja na kutoa hati miliki bila mikingamo, ili kuondoa migogoro ya ardhi nchini.